Nani aliyemuumba Mungu?

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,445
2,000
Maswali mengine unaweza kuchizika kwa kuumiza ubongo kutafuta majibu.
 
Nundu_Tanzania

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
705
500
Kwa nini hukubali?

Unaelewa ukiulizwa mwanamke ni nani, ukajibu mwanamke ni mtu, umejiachia nafasi ya kukosea kwa sababu hata mwanamme naye ni mtu?
Kwasababu hilo nimeshalieleza.

Neno "unaelewa" haliambatani na neno "kukosea"; anaelewa hawezi kukosea. Hivyo swali hilo hapo ni batili.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
55,377
2,000
Kwasababu hilo nimeshalieleza.

Neno "unaelewa" haliambatani na neno "kukosea"; anaelewa hawezi kukosea. Hivyo swali hilo hapo ni batili.

Unaelewa kwamba kuna kuelewa kukosea na hapo neno kuelewa linaambatana na kukosea?

Kwa nini neno "unaelewa" lisiweze kuambatana na neno "kukosea"?

Umekubali mambo mawili yanayopingana kuhusu mantiki.

That is a contradiction.

Unashindwa hata ku define mantiki, sitegemei uweze kufikiri na kujenga hoja kwa mantiki.
 
Nundu_Tanzania

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
705
500
Umekubali mambo mawili yanayopingana.
Kosa lako ni kwamba unakosa uelewa.

Mantiki ni kipengee cha sayansi; hivyo ni sayansi.

Sayansi haya ni maarifa, kwanza yanayokua pia yanayochunguza "Kweli zilizobainishwa", ambazo bado hazijathibitishwa.

Kwahiyo "kile kinachosemwa; neno, wazo au kinachofundishwa": au ni kweli au siyo kweli, kinakuwa mantiki kwasababu mantiki ndiyo inashughulika na hayo yote.

Kama kipengee cha sayansi; hivyo nacho ni sayansi, kile kinachosemwa; neno, wazo au kinachofundishwa kinapothibitika hakiwi tena mantiki, ila kinakuwa kweli.

Jambo lililothibitika kisayansi haliwi tena suala au jambo la sayansi, bali huwa kweli/ ukweli.

Kukinzana kwa mambo (contradiction) ndiyo mantiki yenyewe. Kinyume chake hakiwi mantiki, bali kinakuwa kweli.
 
Nundu_Tanzania

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
705
500
Unaelewa kwamba kuna kuelewa kukosea na hapo neno kuelewa linaambatana na kukosea?

Kwa nini neno "unaelewa" lisiweze kuambatana na neno "kukosea"?
Hakuna kuelewa kukosea, lakini kuna kujifunza baada ya kukosea.

Kwani palipo na uelewa haiwezekani kukawa na kukosea.

Kwa sababu "Uelewa" ni intellectual knowledge na " "Kukosea" ni sense knowledge.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
55,377
2,000
Hakuna kuelewa kukosea, lakini kuna kujifunza baada ya kukosea.

Kwani palipo na uelewa haiwezekani kukawa na kukosea.

Kwa sababu "Uelewa" ni intellectual knowledge na " "Kukosea" ni sense knowledge.
Ukishasema "hakuna kuelewa kukosea" tayari ushaambatanisha kueleewa na kukosea.

Pia, unakataa kwamba hakuna kuelewa kwamba hapa nimekosea?

Hujawahi kuelewa kwamba umekosea?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom