Nani aliyemuumba Mungu?

Sipingi Mungu ambaye hayupo.

Kwahiyo unapinga mungu ambaye yupo???!!, thats nonsense.

Katika huo mfano wako, Kumbuka pia kuna madaktari vilaza wasiojua taaluma yao na kujifanya wanajua huku upeo wa ufahamu wao umefikia mwisho.

Kumbuka sio kila kitu mtu anaweza kujua kwa akili yake binafsi bila kufundishwa na ndio maana kuna taaluma mbalimbali ikiwemo taaluma ya kumjua Mungu.

Jifunze kumjua mungu kwa watu wanaomjua na pia muombe huyo mungu kwa unyenyekevu ajidhihirishe kwako weka kiburi na majivuno yako kando kwani Mungu ni the Most supreme being, asiyehitaji chochote kutoka kwa yeyote na ni yeye aliyekupa hiyo akili kiduchu unayojivunia kumkufurisha.
 
Hakuna mahali nimezungumza maamuzi. Lakini hatahivyo, kabla ya mtu kufanya maamuzi hupitia uthibitisho.
Sijahoji juu ya wewe kutumia neno maamuzi

Neno maamuzi nilimelitumia mimi mwenyewe katika kuelekeza kile nilichokusudia, huna sababu ya kuliwekea mkazo

Najaribu tu kulielewa neno Akili kwa namna ya sifa ulizoweka na kwa mfano nilioweka

Sasa sifahamu ni wapi unakwama katika kunielewa mpaka urudie kutumia neno uthibitisho wakati ulishaliorodhesha kwenye vile vigezo mwanzo vya mtu mwenye Akili anatakiwa awe vipi.!
 
Hujanielewa. Sala hapa nilikuwa nataka kukuthibitishia kuwa swala la kuota huwa linafanyika kwenye ulimwengu wa roho, kiasi kwamba huwezi uka-prove kwa mtu mwingine kwamba huwa unaota, kwa kutumia empirical tools, kwa sababu they (emperical) do not work in the spritual world, so are spritual tools in the empirical realm
Siyo kweli. Kwanza nilikwambia hakuna atakae taka ushahidi wa ndoto kama unaota au hauoti, sababu ndoto ni jambo halisi. Ni sawa na kutaka ushahidi wa Jua liko juu yako au chini yako ? Hili kila mtu mwenye macho analidiriki, na ni sawa na Ndoto.

Pili unaposema ulimwengu wa kiroho, ulimwengu huu una husisha ni na nini ?
 
Anayethibitisha ni yule ambaye hana uhakika. Mungu anapothibitisha anakuwa hana uhakika?
Uhakika ni nini?
Neno "yule" hapo linaeleza nini?
Na neno "Mungu" hapo linaeleza nini?

Changanua maneno "yule" na "Mungu" kila moja katika hoja yako kuonesha "anayethibitisha" na "uhakika."
 
Kabla ya kubishana nani alimuumba Mungu ungeanza kwa kusema Mungu yupi...kama ni Allah tunamjua aliumbwa na Muhammad nk. N.k
Labda ungeanza kwa kutuonesha kwa thibati kabisa huyo mungu unayemzungumzia
Mkuu umelewa asubuhi?
 
Sasa sifahamu ni wapi unakwama katika kunielewa mpaka urudie kutumia neno uthibitisho wakati ulishaliorodhesha kwenye vile vigezo mwanzo vya mtu mwenye Akili anatakiwa awe vipi.!
Hivyo neno "uthibitisho" kujirudia ndio limekufanya usielewe?
 
Hivyo neno "uthibitisho" kujirudia ndio limekufanya usielewe?
Hii nayo ni aina ya ugonjwa..!

Unajiuliza kisha unajipa jibu halafu unadhani aliyeuliza ni mwengine na kisha umemuelewesha.!

Hebu niambie ni kwa kiasi gani unahisi kwa maneno yako ya kujirudia unanielekeza kitu..?
 
Kutoka kwa yeyote yule, hususan asiyeamini ila anayejua.

Anayeamini kuthibitisha, kimantiki, hawezi, ndiyo maana anaamini.Kuamini ni kukubali kitu bila uthibitisho.

Ukiweza kuthibitisha, umeondoka kwenye kuamini, uthibitisho wako unasema kwamba wewe unajua.

Ila hata anayeamini anaruhusiwa kujaribu kuthibitisha.

Na asipoweza kuthibitisha, habari ya kuwepo kwa Mungu inakuwa imani tu kama imani nyingine ambazo hazina uthibitisho.
Suala la uwepo wa Mungu ni imani yani ndio ipo hivyo yeyote mwenye kusema kuna Mungu basi anaamini na si vinginevyo.

Na kuamini si kinyume cha kutokujua maana hata unapotaka kuamini jambo sharti ulijue kwanza hilo jambo, tofauti na hivyo utakuwa unaamin usichokijua. Na kujua hakuna mahusiano ya moja kwa moja na uthibitisho kama ambavyo wewe unavyoeleza.
 
Hii nayo ni aina ya ugonjwa..!

Unajiuliza kisha unajipa jibu halafu unadhani aliyeuliza ni mwengine na kisha umemuelewesha.!

Hebu niambie ni kwa kiasi gani unahisi kwa maneno yako ya kujirudia unanielekeza kitu..?
Kwenye jibu la kwanza kuhusu akili ni nini, niliandika neno "kuthibisha." Na neno unalosema nimelirudia ni " uthibitisho".

Sasa tazama hayo maneno mawili (kuthibitisha na uthibitisho), kisha sema yanaonesha nini.
 
Suala la uwepo wa Mungu ni imani yani ndio ipo hivyo yeyote mwenye kusema kuna Mungu basi anaamini na si vinginevyo.

Na kuamini si kinyume cha kutokujua maana hata unapotaka kuamini jambo sharti ulijue kwanza hilo jambo, tofauti na hivyo utakuwa unaamin usichokijua. Na kujua hakuna mahusiano ya moja kwa moja na uthibitisho kama ambavyo wewe unavyoeleza.
Kuamini ni nini na kujua ni nini?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Planet was created 4,5 billions years ago ,Egyptians start believing in Ra 4,500 years ago and God was the last one 2000 years ago
History of Earth - Wikipedia
thats the best link ever ya jibu la swali lako........binadamu tuna kitu kinaitwa fear before ilikumcontol binadamu lazima akantroliwe ndio maana zikawekwa amri za Mungu,dini, etc...... now ndio maana kuna (sheria) mfano mzuri ngómbe anaaamini fimbo kwa mchungaji kuwa ndo vina mcontrol ili akae sawa
Sayansi, ambayo kwangu ni kitu cha kushikilia sana, kama ambavyo umeandika hapo juu, kwamba dunia inakadiriwa kuwa na umri wa miaka 4.5 bilioni na mtu anakadiriwa ameanza kuwepo duniani miaka milioni mbili (2) hivi.

Maelezo haya au uelewa huu wa sayansi sio kweli kwamba unapinga biblia kuhusu uumbaji (Mwanzo), bali yanafafanua vizuri suala la uumbaji.

Hivyo hoja ya sayansi na hoja ya biblia hazipigani hata kidogo.

Sasa basi, dini yaani Kanisa ambalo ndio mamlaka ya dini siyo utaratibu au sheria au mambo ya watu fulani; ila ni suala la akili au roho.

Hivyo dini, iwe ya kweli au isiyo ya kweli inamhusu kila mtu na popote.

Umakini unapaswa daima kuwa katika kutambua dini isiyo ya kweli. Kwani, bila ya dini ya kweli mtu atasumbuka na matatizo.
 
Umeandika kwamba sayansi kwako ni kitu cha kushikilia sana.

Vizuri.

Sayansi inakwenda na, na inaheshimu sana, uthibitisho. Uthibitisho usiopingika kimantiki.

Unaweza kutoa uthibitisho usiopingika kimantiki kwamba huyo Mungu unayesema yupo, yupo kweli, na si habari za hadithi tu?
 
Kwenye jibu la kwanza kuhusu akili ni nini, niliandika neno "kuthibisha." Na neno unalosema nimelirudia ni " uthibitisho".

Sasa tazama hayo maneno mawili (kuthibitisha na uthibitisho), kisha sema yanaonesha nini.
Hata Njiki na njeke zina utofauti japo zinafanana, kuliko neno uthibitisho na kuthibitisha

Sifahamu kipimo chako cha utofautishaji wa vitu ni wa kiwango gani au ni madesa gani unajaribu kucheza.! Maana tukiendelea hivi unaweza ukaniambia Malapa si Ndala.!

Hata ukisema ulichambue kisarufi hilo neno 'uthibitisho' bado mzizi ni mmoja na neno 'kuthibitisha' ni viambishi tu vinaweza kukupa viashiria kwamba moja ni mchakato na nyengine ni ukamili wa huo mchakato

Ni sawa na kusema kutembea na kukimbia, vyote ni vitendo vya kujongea ila kimoja ni kwa taratibu na kingine ni kwa haraka_hakuna tofauti

Unajua usinitoe kwenye reli

Mimi najaribu kulielewa lile neno Akili na jinsi linavyotofautishwa na neno fikra mpaka likapewa upekee wa kwamba ndipo kwenye hekima ya huyo anayeitwa Mungu.!

Nilidhani unaweza kuwa msaada Ila naona unaanza kuwa msumbufu
 
utofauti japo zinafanana, kuliko neno uthibitisho na kuthibitisha

Sifahamu kipimo chako cha utofautishaji wa vitu ni wa kiwango gani au ni madesa gani unajaribu kucheza.! Maana tukiendelea hivi unaweza ukaniambia Malapa si Ndala.!

Hata ukisema ulichambue kisarufi hilo neno 'uthibitisho' bado mzizi ni mmoja na neno 'kuthibitisha' ni viambishi tu vinaweza kukupa viashiria kwamba moja ni mchakato na nyengine ni ukamili wa huo mchakato

Ni sawa na kusema kutembea na kukimbia, vyote ni vitendo vya kujongea ila kimoja ni kwa taratibu na kingine ni kwa haraka_hakuna tofauti
Ndio. Neno "kuthibitisha" na "uthibisho" mzizi wake ni mmoja.

Lakini, je, neno "kuthibitisha" na neno "uthibitisho" yanaonesha nini? Hili ndilo swali la msingi.

Ukiwa makini utaona neno "kuthibitisha" na neno "uthibitisho" yanaeleza hali mbili tofauti katika maana moja.
 
Ni sawa na kusema kutembea na kukimbia, vyote ni vitendo vya kujongea ila kimoja ni kwa taratibu na kingine ni kwa haraka_hakuna tofauti

Unajua usinitoe kwenye reli

Mimi najaribu kulielewa lile neno Akili na jinsi linavyotofautishwa na neno fikra mpaka likapewa upekee wa kwamba ndipo kwenye hekima ya huyo anayeitwa Mungu.!

Nilidhani unaweza kuwa msaada Ila naona unaanza kuwa msumbufu
Chunguza vizuri mifano yako hapo utaona si rafiki kadiri ya maneno "kutibitisha" na "uthibitisho."

Naweza kusema, kimsingi kwamba hauko makini. Hivyo ni mtu usiyetaka kujifunza; mpingaji.
 
Umeandika kwamba sayansi kwako ni kitu cha kushikilia sana.

Vizuri.

Sayansi inakwenda na, na inaheshimu sana, uthibitisho. Uthibitisho usiopingika kimantiki.

Unaweza kutoa uthibitisho usiopingika kimantiki kwamba huyo Mungu unayesema yupo, yupo kweli, na si habari za hadithi tu?
Sawa.

Hapa umetaja mambo mawili msingi katika hoja hii; hayo ni: sayansi na Mungu.

Jambo la tatu na la nne ni vipengee vya sayansi kama maarifa.

Kwahiyo, ili hoja hii iwe ya manufaa pia kuonyesha utimamu wetu; ni vema tujadili katika msingi wa taaluma yenyewe na sio hisia au hadithi.

Hivyo, basi, katika hoja hii tunalazimika kwanza kujibu maswali msingi haya, kwa kuzingatia maana inayokubalika na wanasayansi wengi; kwanza ni sayansi yenyewe.

1. Sayansi ni nini?

1a. Mantiki ni nini?

1b. Uthibitisho ni nini?

Na

2. Mungu ni nini?

Sasa, unakubali twende katika mwelekeo huu wa kitaaluma?
Karibu.
 
Hili ndiyo tatizo lao, hawawezi kufikiri nje ya mawazo ya Wakubwa zao, ambao no wajinga mno.

Pili, huyu yuko nyuma sana, leo hii bado anajifaragua na Logic/Ilm al Kalaam/Ilm Mantiq (Mantiki) ,elimu ambayo ni dhaifu na kwa yenyewe haiwezi kukupa ukweli.
Uko sahihi mkuu Jurjani!
 
Back
Top Bottom