Nani aliyemuumba Mungu?

Nani aliyemuumba Mungu?

Mfano matatizo ya kiafya kwa maana wapo watu ambao wameumwa na kuzunguka sana mahospitalini na kushindwa kuonekana matatizo yanayowasumbua hivyo kushindwa kupata tiba na mwishoe huishia kuamua kwenda kwenye imani na hupata tiba, haya yapo sana kwenye jamii zetu na si story za kufikirika. Huo ni mfano mmoja tu ila yapo mengi matatizo ya kimaisha ambao tunaona watu wakienda kutatua matatizo yao kwenye kutumia imani.
Hekaya za abunuasi...ukifuatilia kwa undani hao watu sio wewe, nawewe unasikiaga tu...wengine wanalipwa huko wanakodai wanapona wengine wanaenda hawaumwi...wengine hawaponi ila "kwa imani" wana'declare wamepona.

Ingekuwa kweli kwanini watu mtaani wahangaike na ARV?? Kwanini nchi zihangaike na UKIMWI??
Kwanini watu wasipelekwe kwenye imani huko wakapone?
 
Bora masuala ya kiimani hujulikana ni imani na husisitizwa hilo ila kwenye sayansi huwa jambo halielezwi kama kama maoni au mtazamo wa wakati huo Bali huchukuliwa ndio ukweli wenyewe kwamba limefanyiwa utafiti wa kisayansi ila ajabu baadaye unakuja utafiti mwengine na kuonesha ule ukweli wa kisayansi haukuwa kweli maana una makosa.
Toa mfano
 
Zurri bado nasubiria jibu langu.
Mungu akiamua kuumba simu sasaivi huko alipo,anaweza hawezi?
 
Amini mungu yupo.
Kama kuonekana hata upepo hauonekani lakini tunaamini upo.
Uthibitisho sio mpaka 'kuona'
Hata kuhisi ukienda baharini utahisi upepo.

tukija kwa Mungu...wewe unamuongelea Mungu yupi?Maana wako wengi kila jamii ina Mungu wake
 
The question: "If God is the creator, then who created the creator?" is illegitimate because by definition, the Creator is uncreated. He is eternal, without beginning, without end and all affairs return back to Him: (وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلْمُنتَهَىٰ) "And that to your Lord is the return (of all beings and affairs) (and of all perfections in attributes)." (53:42).

Thus to ask who or what created something that is uncreated is the way of:
a) an ignorant person devoid of intellect,
b) a lying deceiver, a sophist.

Note : Maelezo haya mafupi nime "copy" na ku "paste" toka kwenye tovuti iitwayo "www.aboutatheism.net", mnaweza tembelea huko mpate faida.

Tujadili hili, kwa wale wote ambao huuliza swali hilo, waje watuambie kwanini wanauliza swali hilo.

Ahsante.

Jurjani (Zurri)
Binadamu ndio waliomuumba Mungu
 
Nijuavyo Mimi ni kuwa mungu muumba mbigu na nchi si mtu mwenye umbo ila ni roho,kwa mtazamo wa biblia tunaambiwa mungu ni roho nao wamwabuduo wapaswa kumwabudu katika roho na kweli,

Tuje kwenye dhana ya roho,roho ni kitu chenye uhai kisicho na mwili wala mfupa,kwahiyo mungu hana mwili wala mfupa,roho ni sawa na upepo

Katika roho ya uungu(mungu) tunaona kuwa ndiyo roho kuu yenye uwezo wa kutenda miujiza kuliko roho zote ziwazo hapa ndio tunapata dhana ya super natural power,yaani nguvu iliyo kuu,kwa dhana hii watu wengine wanamwita mungu nguvu iliyokuu,yaani the super natural power

Kwa hivyo hii roho ya uungu ilitokea tu na kati ya roho nyingi na ikawa na nguvu na mamlaka kuliko roho zote hivyo ikapata nafasi ya kuzitawala na kutaka ziende katika utashi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kwanza nyoosha Kiswahili chako.

Unapoongelea kiujumla, halafu unarudia tena kuandika "huwezi" kwangu mimi, unaonekana hujui kutumia mantiki na hujui lugha.

Na kama hujui mantiki na lugha, hatuwezi kuelewana.

Kama hunizungumzii mimi binafsi, unazungumzia kiujumla, unachotakiwa kuandika ni "Mtu hatakiwi kudai uthibitisho". Siyo "huwezi kudai uthibitisho".

Unaelewa tofauti?

Sasa nitajadiliana nawe vipi falsafa ya dini wakati hata Kiswahili na mantiki hujui?

Unaelewa tofauti ya kuuliza "May I help you?" na "Can I help you?".

Naona unanipaka shombo la mawazo tu kubishana nawe.

Inawezekana unatakiwa kuoga kiakili kwanza kabla ya kujadiliana nami.

Moron.

Sent from my typewriter using Tapatalk
Nilijua tu ulikuwa unatafuta upenyo uanze kunishambulia binafsi maana ulishashindwa kutetea hoja yako.
 
Nilijua tu ulikuwa unatafuta upenyo uanze kunishambulia binafsi maana ulishashindwa kutetea hoja yako.
Hoja ukiiona utaijua?

Wewe usiyejua kutenganisha cha jumla na binafsi leo unaniambis nakushambulia binafsi?

Define Mungu ni nini.

Thibitisha yupo.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Bora masuala ya kiimani hujulikana ni imani na husisitizwa hilo ila kwenye sayansi huwa jambo halielezwi kama kama maoni au mtazamo wa wakati huo Bali huchukuliwa ndio ukweli wenyewe kwamba limefanyiwa utafiti wa kisayansi ila ajabu baadaye unakuja utafiti mwengine na kuonesha ule ukweli wa kisayansi haukuwa kweli maana una makosa.
Lini hii sayansi ilijipinga?
 
Hekaya za abunuasi...ukifuatilia kwa undani hao watu sio wewe, nawewe unasikiaga tu...wengine wanalipwa huko wanakodai wanapona wengine wanaenda hawaumwi...wengine hawaponi ila "kwa imani" wana'declare wamepona.

Ingekuwa kweli kwanini watu mtaani wahangaike na ARV?? Kwanini nchi zihangaike na UKIMWI??
Kwanini watu wasipelekwe kwenye imani huko wakapone?
Tatizo huwa hata hamfanyi uchunguzi kama hapo unaongea tu kijumla jumla, niambie ni jambo gani ulifuatilia kiundani?

Et wengine wanaenda hawaumwi!! Wewe unazungumzia utapeli ule makanisani, ndio maana nasema huwa hamfanyi uchunguzi nyie mkisikia ule utapeli kanisani ndio mnakuja kujenga hoja humu wakati watu tumeshuhudia ndugu na rafiki zetu waliyokuwa na matatizo wakitatua matatizo kwa imani mbalimbali achana na huo utapeli wa kanisani.

Nyie sijui huwa mnaishi jamii gani ambazo hamkutani na haya tunayoeleza?
 
Lini hii sayansi ilijipinga?
Umeelewa lakini?

Nazungumzia jambo la sayansi siku zote huwa linachukuliwa kuwa ndio ukweli wenyewe hukuti wakisema haya ni maoni ya wakati huu kwamba yaweza isiwe sahihi, ila baadaye ukija utafiti mwengine unakuta unakuja kuonesha lile jambo halikuwa sahihi kuna makosa.
 
Hoja ukiiona utaijua?

Wewe usiyejua kutenganisha cha jumla na binafsi leo unaniambis nakushambulia binafsi?

Define Mungu ni nini.

Thibitisha yupo.

Sent from my typewriter using Tapatalk
Ndio unanishambulia kwa sababu hata mie ningetaka ningekushambulia kwa, kushindwa kutofautisha uthibitisho na definition.

Tatizo siku zote nakwambia unaupenda ubishi ila hauwezi na ndio maana unatoka nje ya mada na kuanza kuni attack hauwezi kusimamia hoja yako hadi mwisho, wewe ilimradi ubishane tu.
 
Umejuaje kama Mungu hayupo ? Usilete story za vijiweni.

Umesoma vitabu vya dini mpaka vikakuonyesha vimetungwa ? Kisha utupe mfano wa maandiko husika.

Mbona una hitimisha bila kuweka uthibitisho kijana ? Kwahiyo sifa ya kitu kutokuwepo kikiwa hakionekani si ndio ? Una uhakika watu hawakuona muujiza wowote ?

Aisee unaandika upuuzi sijapata kuona hapo kabla.

Hehe hivi umelewa?
Sihitaji unionyeshe mungu yuko wapi, nahitaji uthibitisho kua yupo, uthibitisho unaweza kua njia yoyote ila sio lazima macho. Hivi vilaza mna matatizo gani? Hamjui kuna sense zaidi ya macho? Em acheni kunipotezea muda
 
Maelezo yako yanaonyesha wazi ya kuwa :
1. Humjui Mungu unae kataa kuwa yupo
2. Huwezi kuthibitisha hilo ya kuwa Mola hayupo

Sasa nina swali la msingi umejuaje kama Mola hayupo na unawezaje kumjadili usie mjua ? Huu ujasiri unaupata wapi ?

Mimi sitakiwi kuprove kutokuwepo kwa mungu wewe unayesema yupo ndiyo unatakiwa kuprove, vilaza mnafikiria kinyume, nikikwambia nywele zako zina waka moto huku we huoni zinawaka moto nani atatakiwa kutoa proof kua zinawaka moto? Mi ndo nitakuuliza uprove kua haziwaki? Kilaza kabisa
 
Mzee kuhusu wachawi mimi siamini na hakuna mtu wa kuniroga mimi..
Kuhusu hewa ambayo kwa kingereza inaitwa air ambayo by definition ni mixture ya gases kama nitrogen , Oxygen na carbondioxide hatuwezi kuiona sababu ni colorless lakini kuna tests za kutest hizo gases na mtu una unakubali kabisa.. na personally nimetengeneza oxygen na nikaitest , nimeshuhudia carbondioxide nikaitest.. sasa unataka ushahidi gani kuhusu hewa.?
Hizo test baki nazo...!! Mimi pia nimesoma maandiko nikayaamini...pia nimeshuhudia maeneo ya kihistoria juu ya yote yaliyotokea kuthibitisha uwepo wa Mungu nikaamini. Ila wewe hayo huyaamini lakini unataka niamini test zako kuonesha hewa ipoo???? Ntaaminije test ambazo nazo pia zimetengenezwa kusupport Uongoo???? Mbona wewe huamini maandiko lakini unataka niamini procedure zako za kutest hewa.. Sitaki test nataka HEWAAA NIIONE
 
Hizo test baki nazo...!! Mimi pia nimesoma maandiko nikayaamini...pia nimeshuhudia maeneo ya kihistoria juu ya yote yaliyotokea kuthibitisha uwepo wa Mungu nikaamini. Ila wewe hayo huyaamini lakini unataka niamini test zako kuonesha hewa ipoo???? Ntaaminije test ambazo nazo pia zimetengenezwa kusupport Uongoo???? Mbona wewe huamini maandiko lakini unataka niamini procedure zako za kutest hewa.. Sitaki test nataka HEWAAA NIIONE
Ungekuwa unajua hata historia ya kanisa au hayo unayoyaita maandiko usingekuwa unaongea hivyo.
 
Back
Top Bottom