Expedito Mduda
JF-Expert Member
- Sep 22, 2009
- 522
- 240
Tanganyika iliyopata uhuru tarehe 9/12/1961 ni ya Watanganyika. Watu wanaotakiwa kuhakikisha nchi inaenda sawa ni Watanganyika wenyewew. Kosa letu kubwa tunalolifanya sisi kusubiri watu wengine watufanyie kazi na sisi tulio wengi tunakaa tukiongea sana bila kushiriki kuleta mabadiliko.
Ili kufanikisha nia yetu ya kuleta mabadiliko ni lazima kila mpenda maendeleo ashiriki kikamilifu katika suala hili.
Wananchi wote tuhakikishe tunaelimishana na kila mmoja wetu ajue umuhimu wa mabadiliko tunayotaka. Cha msingi sana tunachotaka ni mabadiliko ya katiba. Tukibadilisha katiba, demokrasia katika nchi yetu. Katika hilo tutafanikisha kuleta tume huru ya uchaguzi, kupunguza madaraka ya raisi maana madaraka ya sasa yanamruhusu yeye kuteua viongozi wengi mno na hivyo kuminya demokrasia ya nchi yetu.
Katiba mpya itazuia wezi wa kura unaolalamikiwa mpaka sasa. Angalia kama yale yanayosemwa yametokea Tandahimba,Segerea na kwingineko. Demokrasia ikishamiri maendeleo yatakuja si muda mrefu!