Nani aijenge na kuipigania Tanganyika kama siyo Watanganyika!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani aijenge na kuipigania Tanganyika kama siyo Watanganyika!?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Expedito Mduda, Dec 12, 2010.

 1. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tanganyika iliyopata uhuru tarehe 9/12/1961 ni ya Watanganyika. Watu wanaotakiwa kuhakikisha nchi inaenda sawa ni Watanganyika wenyewew. Kosa letu kubwa tunalolifanya sisi kusubiri watu wengine watufanyie kazi na sisi tulio wengi tunakaa tukiongea sana bila kushiriki kuleta mabadiliko.

  Ili kufanikisha nia yetu ya kuleta mabadiliko ni lazima kila mpenda maendeleo ashiriki kikamilifu katika suala hili.

  Wananchi wote tuhakikishe tunaelimishana na kila mmoja wetu ajue umuhimu wa mabadiliko tunayotaka. Cha msingi sana tunachotaka ni mabadiliko ya katiba. Tukibadilisha katiba, demokrasia katika nchi yetu. Katika hilo tutafanikisha kuleta tume huru ya uchaguzi, kupunguza madaraka ya raisi maana madaraka ya sasa yanamruhusu yeye kuteua viongozi wengi mno na hivyo kuminya demokrasia ya nchi yetu.

  Katiba mpya itazuia wezi wa kura unaolalamikiwa mpaka sasa. Angalia kama yale yanayosemwa yametokea Tandahimba,Segerea na kwingineko. Demokrasia ikishamiri maendeleo yatakuja si muda mrefu!
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2010
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,611
  Trophy Points: 280
  hatuezi kuendelea bila elimu au kwa kutoa shahada za kujipendekeza kwa viongozi.maprof wawe makini na taruma zao...!!
   
 3. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,159
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Watanganyika tumegeuzwa misukule na Wazenj tumekatwa ulimi tupo darini sasa tunatumikishwa na kuburuzwa usiku! Habari ndio hiyo!
   
 4. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Inaniuma sana mimi Mtanganyika ambae nchi yangu haijulikani imekwenda wapi, ni lazima tuidai na irudi kwa kuanzia ningeomba wanaoujua wimbo wetu wa Taifa la tanganyika watuwekee hapa ili nianze kuukariri na kumfundisha mwanangu Brian.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Muda si mwingi tutaipata Tanganyika. Muhimu tukubali kuidai kwa nguvu zetu zote. Alilianzisha Mtikila, mkamuona mwehu, sasa mmeanza kujionea jinsi mke wetu Zanzibar alivyoanza kujibaraguza, anadai haki sawa kwa mke na mume. Enheheheheheheheeeeee
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  tatizo maprofessor wenye maamuzi katika vyuo vyetu ni wapumbavu (sorry) vibaraka wa CCM.
   
 7. Z

  Zenj Empire New Member

  #7
  Dec 13, 2010
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ugonjwa wenyewe ulianzia hapa, Watanganyika mulipoaminishwa na mtu muliyemuamini kuwa ana akili nyingi kuwashinda nyote, Mwalimu Julius Nyerere, kwamba amewapatia kisura cha kuoa, yaani Zanzibar. Mukawa tangu hapo munajiaminisha kuwa nyinyi ni waume na sisi ni wake na Muungano wetu ni ndoa. Masikini, hamukuzingatia kwamba hata kama ingelikuwa hivyo (ambavyo sivyo), basi bado kuna makabila mengine huko kwenu Tanganyika, ambapo mke huwa ndiye mwenye sauti na mali, kauli, na influence hutoka kukeni.

  Bahati nyengine mbaya ni kuwa mulitumia nguvu sana kuliimarisha hilo lionekane na liaminike hivyo. Hivi munajua Mkoa wa Mjini Maghribi peke yake, ambao haufikii hata ukubwa wa wilaya ya Temeke, una kambi ngapi za kijeshi na ambazo zaidi ya nusu na robo ya wapiganaji wake mumewaleta kutoka huko Tanganyika? Ulizeni mutaambiwa, lakini mimi nitakachowambia ni kuwa huko kulikuwa ni kuifanya njozi ya Nyerere kuilazimisha hii aliyowaamisha kuwa ni ndoa.

  Sasa, tumefika mahala pa sote kung'amua kwamba tulidanganywa na tulikandamizwa. Ni ama pawe na Muungano wa kuheshimiana na kutambuana kila upande na haki na stahiki zake, au pasiwe na Muungano kabisa. Sisi hatuna roho mbaya wala kiburi. Ikiwa muko tayari kwa hilo, karibuni tushirikiane.
   
 8. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Ugonjwa wenyewe ulianzia hapa, Watanganyika mulipoaminishwa na mtu muliyemuamini kuwa ana akili nyingi kuwashinda nyote, Mwalimu Julius Nyerere, kwamba amewapatia kisura cha kuoa, yaani Zanzibar. Mukawa tangu hapo munajiaminisha kuwa nyinyi ni waume na sisi ni wake na Muungano wetu ni ndoa. Masikini, hamukuzingatia kwamba hata kama ingelikuwa hivyo (ambavyo sivyo), basi bado kuna makabila mengine huko kwenu Tanganyika, ambapo mke huwa ndiye mwenye sauti na mali, kauli, na influence hutoka kukeni.

  Bahati nyengine mbaya ni kuwa mulitumia nguvu sana kuliimarisha hilo lionekane na liaminike hivyo. Hivi munajua Mkoa wa Mjini Maghribi peke yake, ambao haufikii hata ukubwa wa wilaya ya Temeke, una kambi ngapi za kijeshi na ambazo zaidi ya nusu na robo ya wapiganaji wake mumewaleta kutoka huko Tanganyika? Ulizeni mutaambiwa, lakini mimi nitakachowambia ni kuwa huko kulikuwa ni kuifanya njozi ya Nyerere kuilazimisha hii aliyowaamisha kuwa ni ndoa.

  Sasa, tumefika mahala pa sote kung'amua kwamba tulidanganywa na tulikandamizwa. Ni ama pawe na Muungano wa kuheshimiana na kutambuana kila upande na haki na stahiki zake, au pasiwe na Muungano kabisa. Sisi hatuna roho mbaya wala kiburi. Ikiwa muko tayari kwa hilo, karibuni tushirikiane.
  Mshirikiane na nani?


  HAKUNA SHA USHIRIKIANO HAPO WAKATI MNABENDERA YENU NA NYIMBO YENU YA TAIFA, NA KILA TUKIKUTANA NA NYINYI HUKU NJE YA TANGANYIKA NA ZANZIBAR(sitaki kuita tanzania),HUWA MNAJIITA WAZANZIBARI, NI SISI NDIO WAPOLE NA WAKIMYA, TUMECHOKA SASA TUNATAKA TANGANYIKA NA NYIE MUENDE KWA AMANI TUBAKI KUWA MAJIRANI, HAINA HAJA YA KUWA NA MUUNGANO WA AINA HII.
  rais mmoja ni amiri wa majeshi na mwengine yupoyupo tu, pamoja na mbo mengi tu ambayo SISI WATANGANYIKA ASILIA HATUONI UMUHIMU WAKE.

  MUNGU IBARIKI TANGANYIKA.
   
 9. t

  tufikiri Senior Member

  #9
  Dec 13, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zidumu fikra za mwalimu nyerereeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. g

  ganzel Member

  #10
  Dec 13, 2010
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh!kaka nyi wapemba mmeshtuka sasa.

  unajua kiuchumi mlikua juu kipindi tunaungana lakini sasa poleni.
  ata ivyo muungano kwa wapemba ulikua na maana kwa wakati ule sio sasa kwani ulikua unatuliza hali ya amani kwa kua serekali iliyokuwepo ni ya mapinduzi so kama tusingekuja sisi watanganyika ambao kwa sasa hatulitaki hilo jina mngekue mpaka leo mnapinduana tu.

  wapemba jipangeni tu na sisi tutaamka awa mafisadi kwetu wanakunyimeni hata hata haki zenu za msingi, hata rais wenu mafisadi ndi wanaamua nani awe rais wa wapemba?

  lakini na nyie nani hasa alofanya kosa la kuunganisha chama?
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nakwambia hapo wapemba hawawezi kukujibu jinsi walivyoolewa kwa ndoa ya mkeka na ccm. teh teh teh teh teh sasa hivi wasikilize wanavyojidai kwamba Zanzibar kuna amani. Iko wapi? kwa sababu rais na makamu wake wa kwanza ni wapemba. teh eh teh teh teh
   
 12. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,159
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Tulikuwa kwenye Basi lililo jazana hata pa kupumua hakuna konda anapanga watu kwa kuwasukuma kama ng'ombe kituo kilicho fuata konda anaongeza abiria kwa madai kuwa gari haijai kinachojaa ni ndoo ya maji Mwana nyii vipi î£ýù@ö
  Kama sivyo kakodi taxi huku tupo kwenye foleni kubwa tukivuja jasho wote ndani ya basi tuliridhika na hali hiyo

  Tulipo shuka mama mmoja akanikabili akasema Tanganyika tumelaaniwa na hizi alama/dalili si zake bali za M/MUNGU Akasema;

  1-MUNGU atakutia woga hata ukiona unyasi utafikiri ni nyoka utatoka mbio.

  2-Kondoo wako atachukuliwa kuchinjwa na kuliwa machoni kwako wewe hutii neno

  3-Utaoa wewe mkeo atachukuliwa na wengine

  4-Utajenga wewe wataishi wageni wewe hutakaa humo

  5-Kutakuwa na mafarakano kama Babeli lete maji utapeleka moto lete mwiko utapeleka kalai jambo dogo utaliona kubwa utahaha jambo kubwa utalipuuza!

  6-Kila kitu utasema nitafanya kesho na kutumainishwa upepo!

  KWELI TUMELAANIWA?
  KAMA KWELI TUFANYE NINI?
  KAMA SIO KWELI TUMEJIKWAA WAPI?
  KARIBUNI JAMVI HILOO!
   
 13. j

  justina Member

  #13
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi bado siamini kama tumelaaniwa? kwani naamini kila mtu ana akili na anafanya kitu kwa akili yake, huku akijua anaharibu au anabomoa
   
 14. j

  justina Member

  #14
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua makonda ndo lugha zao za siku zote tumewazoea, so hata wakipata elimu awawezi kubadilika kwani nao wako kazini wanahitaji kujaza abiria wengi ili waweze kupata kipato
   
 15. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,159
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Epa hata wakipata elimu hawatabadilika
  Dowans
  elimu duni
  tangold
  richimond
  rushwa
  ufisadi nk nk nk
  wote waweze kupata kipato chao
  JIBU RAHISI KWA SWALI GUMU
  Ndipo penye LAANA Mwanangu!
   
 16. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuamsha (concietization) watu kuweza kujielewa wao wenyewe na kuwaelewa wenzao na hata taifa kwa ujumla ni mchakato (process). Hivyo, hakuna aliyelaniwa, ila watanzania wako kwenye mchakato wa kuelimika kutoka kwenye wimbi la mgando wa kifikra-unaoona uduni na umaskini wa watanzania kuwa ni mpango wa mungu. Watanzania wanazidi kuelevuka kuona kuwa mstakabari wa maendeleo yao unaletwa na jitihada za wao wenyewe (watu), ardhi au rasilimali nchi, na uongozi bora (siyo mapenzi ya Mungu).

  Hivyo tunatoka kwenye kuamini kuwa kila kitu ni mapenzi ya mungu-kuelekea kwenye-jitihada za watu, uongozi na rasilimali zilizopo. kadri tuelekeapo huko, ndo utaona watu wanazidi kuona ukweli wa DOWANS, Richmond, EPA, MEREMETA, TANGOLD, SHERATON/KEMPESKY ect. katika harakati zao za kulikomboa Taifa kutoka kwa wazungu weusi
   
 17. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,159
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  thanks!!
   
 18. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Wamelaaniwa masikini wa nchi hii wanaodhani kilaana-laana. Narudia tena. Wanaodhania kilaana-laana. Kwamba CCM na viongozi wake bado wanastahili kuiongoza nchi hii.

  Hii ni laana iliyokuu kupita zote, na kama hatutabadilika huko tuendako tutaanza kucharangana mapanga.
   
 19. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #19
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Good and difficult question.

  The succinct reply is Yes and No. Yes as a nation. No as individual citizen
   
 20. k

  kamsamba Member

  #20
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani hatujalaaniwa wote,waliolaaniwa ni washabiki wote wa CCM na wanachama wote,wanaoshobokea Tshirt na Kofia.
   
Loading...