Tanganyika ina wenyewe na wenyewe ndiyo sisi

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Maji tumeshayavulia, hatuna namna isipokuwa kuyaoga! Tanganyika ni nchi yetu, tuanaitaka! Tunaweza kwenda pande zote za dunia, lakini Tanganyika itasalia kuwa nyumbani, turejeshewe.

Kwingineko kote tunaweza kuitwa wageni, lakini tuwapo Tanganyika tunajisikia kuwa nyumbani hata pasipokuambiwa hivyo. Tanganyika ni kwa ajili ya Watanganyika.

Taarifa iwafikie maadui wote wa Tanganyika; kama siku za nyuma walifanikiwa kuifunika, wasifikiri watafanikwa safari hii.

Watanganyika tumeamka, na hatutalala tena.

~ Tunaitaka bendera ya Tanganyika
~ Tunautaka wimbo wa Taifa la Tanganyika
~ Tunaitaka katiba ya Tanganyika
~ Tunamtaka Rais wa Tanganyika
~ Tunamtaka Msemaji wa Tanganyika
~ Tunataka mipaka ya nchi ya Tanganyika ibainishwe
~ Kama imewezekana kwa ndugu zetu, isiwe nongwa kwetu. Tunaitaka Tanganyika yetu.

Tanganyika ina wenyewe, na wenyewe ndiyo sisi. Tunaitaka Tanganyika yetu, Tanganyika ni urithi wetu, wa watoto wetu na wa vizazi vyetu.

Hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanganyika, tunaitaka nchi yetu, Tanganyika.
 
Maji tumeshayavulia! Hatuna namna isipokuwa kuyaoga!!!

Tanganyika ni nchi yetu, tuanaitaka!

Tunaweza kwenda pande zote za dunia, lakini Tanganyika itasalia kuwa nyumbani, turejeshewe!

Kwingineko kote tunaweza kuitwa wageni, lakini tuwapo Tanganyika tunajisikia kuwa nyumbani hata pasipokuambiwa hivyo. Tanganyika ni kwa ajili ya Watanganyika.

Taarifa iwafikie maadui wote wa Tanganyika! Kama siku za nyuma walifanikiwa kuifunika, wasifikiri watafanikwa safari hii.

Watanganyika tumeamka, na hatutalala tena.

Tunaitaka bendera ya Tanganyika!

Tunautaka wimbo wa Taifa la Tanganyika!

Tunaitaka katiba ya Tanganyika

Tunamtaka Rais wa Tanganyika!

Tunamtaka msemaji wa Tanganyika!

Tunamtaka mipaka ya nchi ya Tanganyika ibainishwe!

Kama imewezekana kwa ndugu zetu, isiwe nongwa kwetu. Tunaitaka Tanganyika yetu.

Tanganyika ina wenyewe, na wenyewe ndiyo sisi!

Tunaita Tanganyika yetu!
Tanganyika ni urithi wetu!

Tanganyika ni urithi wa watoto wetu!

Tanganyika ni urithi wa vizazi vyetu.

Hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanganyika! Tunaitaka nchi yetu, Tanganyika!!!
Huyo Libibi atalinywa akae kwa kutulia
 
Mm siitaki

Lete ushahidi
"Uchungu wa mwana...".
Mtanganyika ndiye mwenye uchungu na Tanganyika.

Huenda wewe si Mtanganyika!
Na kama ni Mtanganyika, sitashangaa pia. Si kila Mtanganyika ni Mzalendo kwa Tanganyika.

Lakini kwa sisi wengine tunaojua Tanganyika ni urithi wetu halali, Tanganyika haiwezi kutoka vinywani mwetu!

Hata kama tungefungwa vinywa tusiseme, Tanganyika haitatutoka mioyoni mwetu!

Hata tungezawadiwa uraia wa nchi nyingine, bado tungejua tu Tanganyika ni nyumbani.

Mtu anaweza kufanya afanyalo, lakini hataweza kututenga na Tanganyika.

Sisi ni Tanganyika, na Tanganyika ni sisi!!!
 
Ni kweli Tanganyika ni ya watanganyika sisi, na tuna uchungu nayo.
Lakini mwisho wa siku Royal families za Tanganyika ndio zitakua na maamuzi ya nini kifanyike Tanganyika, au mpaka tuamue kuamka na huchukua hatua.

Long Live Tanganyika.
 
Ww embu Acha mawazo finyu mnataka mgawanyo kwa faida ipi?
Mpaka sasa kuna mgawanyo, tena ulio wazi kabisa:

1. Rais wa Tanzania
2. Rais wa Zanzibar

Tanzania imetokana na nini?

Kwa nini Zanzibar na Tanzania na siyo Zanzibar, Tanganyika na Tanzania?
 
Back
Top Bottom