21[SUP]st[/SUP] November 2013, Alhamisi
Sifahamu usingizi ulinipitia saa ngapi ila nilishtushwa na sauti ya mtu akilia. Alikuwa ni Brenda ameamka. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Sikuelewa ni kwa nini alikuwa akilia vile. Nilimbembeleza aniambie nini hasa kilichokuwa kikimliza. Nilimdanganya kwa ahadi nyingi za mapenzi na hata ndoa alimradi anyamaze. Lakini kadri nilivyotaja hizo ahadi ndipo alipozidi kulia. Baada ya muda alinyamaza na kunielezea.
Kumbe Brenda alizaliwa akiwa keshaathirika na virusi vya UKIMWI. Wazazi wake walifariki miaka mitano iliyopita kwa ugonjwa huo. Nakumbuka aliwahi kuniambia kuwa yeye ni yatima na kuwa alikuwa akilelewa na mjomba wake. Lakini kamwe hakuwahi kuniambia sababu za wazazi wake kufariki.
Hivyo Brenda alikuwa akiishi na virusi hivyo kwa muda wote huo. Mbe, nilianza kukumbuka kila kitu nilichokifanya usiku wa siku hiyo nikajua tu nimeshaupata. Nakumbuka mchana wa hiyo siku nilinyoa mavuzi na kwa hakika kuna sehemu mbili tatu nilijikata. Nilikumbuka kuwa pia sikutumia kinga yoyote na kwa vile alivyokuwa akikataa lazima kutakuwa na michubuko ambayo ama kwa hakika nisingeweza kuiona kwa macho lakini ipo.
Ghafla kichwani nilipata picha iliyonipagawisha. Nilijiona nikiwa nimekonda hadi mbavu zinaonekana huku nikiwa nimetuliwa na nzi kila mahali na sina mtu anayenihudumia kwani kila aliyepita alikuwa akisema yake; Huyu alikuwa player sana amevuna matunda ya uhuni wake Hata mama yangu nilimsikia akiniambia, huyu ndo mjukuu uliyeniletea mwanangu? UKIMWI?
Bila kujielewa nilijikuta nikienda kwenye kabati la dawa na sifahamu hata nilichukua nini na nini ila nilimeza vidonge vingi nikashushia na konyagi. Nahisi ni Brenda ndiye aliniwahi na kunileta hospitali la sivyo ningeshaondoka mbe.
Nilipata wazo la kumuuliza huyu Brenda yupo wapi lakini ghafla nikamuona mama yake akiingia wodini na nilipotupia macho saa yangu ya mkononi ndipo niligundua imeshafika saa sita za mchana na muda wa kuwaona wangojwa ulikuwa umewadia. Nilimsalimia na kuwaaga huku nikibaki na maswali mengi kichwani ya kumuuliza Nicas.
Kwa bahati mbaya nilitakiwa kupanda ndege ya jioni ile na kurudi Dar es salaam kuendelea na majukumu ya kujenga nchi. Nikiwa kwenye ndege niliwaza sana na kuogopa sana moyoni. Hakuna aliye salama tena katika nyakati hizi. Hata yale mananasi yaonekanayo masafi na mazima kwa nje kumbe yameozea kwa ndani.
Wasalaam wapendwa,
Mentor.