Namuheshimu mama yangu lakini simpendi

kwa kweli mama ni mama usimchukie iko siku atarudi kwako atakupenda hamna mama anayemchukia mwanawe aliyemzaa uchungu wake alipokuzaa anajua mama
 
mkuu baba yangu hakuwa tajiri,tuliishi maisha ya kawaida kabisa,lakini waliweza kutulea
kwa kweli jambo la kusema tulazimishe kupata mali mimi nipo kinyume kabisa
naishi maisha ya kawaida nina nyumba,kazi na kausafiri,na nina watoto wangu wazuri sana
jamani nifanye nini mimi ili niheshimike?
haaaaaa kumbe we tajir kabisa yani una nyumba na usafiri kabisa? hayo ndiyo maisha mbona hukuna mengine kaka usiwaze...
 
tafuta mali mzee ili uheshimiwe, mama yako anataka utafute mali uwe kama wenzio...hataki kukulea OK!
 
mkuu mimi ni mwanaume na ni wa kwanza kuzaliwa,wadogo zangu wana uwezo lakini mimi sina uwezo sana ila mungu amenisaidia kuridhika na hali niliyo nayo

Lkn tabia za kichaga ndivyo zilivyo.Ukirudi kijijini kama huna kitu ni lazima utakuwa mdogo tu...... ..hata kama uwe na ndevu hadi miguuni.Fight kaka ili heshima irudi. siku zingine utaenda unaweza ukatumwa maji ya kunywa na mdogo wako...kisa huna chapaa mjini.....!
 
Aisee hii ipo sana hata kwa waha kwani baba yangu naye alidharaulika wakati mambo hayajanyoka hivi sasa wanataka ushauri kwake kama wewe ni mkiristn bibria inasema mawazo ya masikini hayasikilizwi kata kama mazuri jipe moyo ipo cku watatia heshima
 
Kila mtu ameumbwa na mapungufu mengi tu wala hakuna hata mmoja aliyemkamilifu katika maisha yake, ni kwa neema ya Mungu tu tunaishi bila kuangamizwa kwa mapungufu yetu.

Wahenga walisema "Nani kama Mama?".
Kitendo cha Mama yako mzazi kukubeba tumboni mwake miezi 9, akikupatia damu na nyama zake, hatimaye akapitia uchungu mkali pengine aliumia vibaya sehemu za siri katika kukuzaa, akavumilia ujinga wako wote wa utotoni akakulea akikufundisha mambo mengi ikiwamo kumfahamu baba yako mzazi na ndugu zako wengine: Yote haya yanadhihirisha kuwa upendo wake kwako ni mkuu sana ingawa wewe unaona anakuchukia eti kwa vile huna mali! Kuwa makini usije ukawa unaongozwa na hisia zisizo sahihi.

Pamoja na mapungufu unayoyaona kwa mama yako mzazi zingatia dondoo hizo hapo juu, umpende mzazi wako toka moyoni na siyo juu juu tu, endapo unaona huwezi kubadilika nakushauri uende kwa Yesu atakubadilisha na kuwa mtu mpya kabisa, baada ya muda utasema "Ya kale yamepita, tazama yamekuwa mapya". Kama biblia imeagiza kuwapenda majirani na adui zetu na kwamba asiyewapenda hao hawezi kuuona ufalme wa mbinguni, itakuwaje kwako wewe usiyempenda mama yako mzazi?
 
wakuu nina tatizo nimekaa nalo muda mrefu sana moyoni mwangu'
tumezaliwa wanne kwenye familia yetu'
sisi ni wachaga na tumekulia na kulelewa na kusoma uchagani'
lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'
baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'
lakini hicho kitendo kilijidhiirisha hata kwa watu wanaotufahamu kijijini kwetu na ilileta matatizo makubwa'
kwa kweli kutoka moyoni mwangu nimejikuta simpendi kabisa mama yangu lakini bado namweshimu kama mzazi wangu'
nikienda nyumbani mara moja kwa mwaka sijisikii kabisa hata kukaa naye hata kwa dakika 10 inakuwa ngumu sana,
niliumia sana kwa kuwa mimi ndiye maskini kabisa na ndiye ambaye sipewi heshima kabisa
naombeni kujua kama kuna mtu mwenye matatizo kama haya na naombeni kujua kama kunaweza kutokea matatizo yoyote katika maisha yangu kwa hilo

nawakilisha.

Mmmh, Wachagga bwana!
 
hiyo tabia ya mama yako imekuwa kawaida tu siku hizi kwa wazazi wengi. nakushauri msamehe huyo mama kwani naye ni binadamu kama wengine. endelea kumheshimu hivyohivyo na ikibidi uongeze heshima lakini pia uwe na bidii kutafuta kujitegemea kwanza na kisha kama ni mapenzi ya Mungu uwe na mali ya ziada na hata uwezo wa kuwasaidia wengine akiwemo mama yako huyo.

kumbuka kuwa kama hujajitegemea, hilo ndo kikwazo cha kwanza cha wewe kuheshimiwa na watu. jitahidi ujitegemee kwanza. kama tayari unajitegemea, ni vyema lakini usiwe unaomba kusaidiwa na ndugu zako au kupeleka mashitaka nyumbani kwenu kuwa ndugu zako hawakusaidii. jitahidi kupigana peke yako na ikiwezekana shirikiana kwa karibu na marafiki wema ili kuangalia namna ya kunyanyuka kimaisha kwani siku utakaponyanyuka, utaheshimiwa na wote.

mwisho usipuuze haja ya kujiendeleza kwa kutafuta elimu kubwa zaidi. wengi walishindwa kupata maisha mazuri kwa kuyatafuta mitaani, wakayapata kirahisi kupitia darasani. kuna mtu namfahamu ana zaidi ya miaka kumi (10) hajafika kwao kwa sababu kama hizi zako, heri wewe unakwenda kila mwaka! ila yeye alijikita katika elimu na hata sasa yuko nje akipasua kitabu na hiyo imemletea tena heshima katika familia kwani kila mtu anakubali kuwa his future is brighter!

Mungu hawezi kukunyima vyote, Yeye ni mwaminifu kwao wamchao na hakika siku moja atasikia sala yako atakuinua kwa wakati wake

Jina la Bwana lihimidiwe

Ms Judith nimekumiss kweli jukwaani.
Karibu tena.
 
Last edited by a moderator:
wakuu nina tatizo nimekaa nalo muda mrefu sana moyoni mwangu'
tumezaliwa wanne kwenye familia yetu'
sisi ni wachaga na tumekulia na kulelewa na kusoma uchagani'
lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'
baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'
lakini hicho kitendo kilijidhiirisha hata kwa watu wanaotufahamu kijijini kwetu na ilileta matatizo makubwa'
kwa kweli kutoka moyoni mwangu nimejikuta simpendi kabisa mama yangu lakini bado namweshimu kama mzazi wangu'
nikienda nyumbani mara moja kwa mwaka sijisikii kabisa hata kukaa naye hata kwa dakika 10 inakuwa ngumu sana,
niliumia sana kwa kuwa mimi ndiye maskini kabisa na ndiye ambaye sipewi heshima kabisa
naombeni kujua kama kuna mtu mwenye matatizo kama haya na naombeni kujua kama kunaweza kutokea matatizo yoyote katika maisha yangu kwa hilo

nawakilisha.

Hii tabia ya dharau toka kwa mzazi kwenda mtoto hua naichukia sanaaaa (yan sumtyms my blood boils) !!! Dharau toka kwa mzazi kwenda kwa mtoto si kwenye mambo ya kipato tu... ni kitu ipo sehem nyingi i.e age differences, kiwango cha elimu, life experiences na hata sumtyms naona ni kitu kama upendeleo flan hvi. Unakuta kijana mdgo anatoa mchango mzuri tu kwenye familia lakn mzazi anakua anamletea matusi na dharau tena in public mbele za wadogo zako, ndugu na jamaa wengine. Haileti heshima u kno.

(Baba yangu mzazi zamani alikua ana tabia hzi kuna siku nlimchenjia hakuamini macho yake, sikumtusi au kumkosea heshima ila kuna namna nilimchana kwa maneno nahisi mpaka anakufa hatosahau maneno yangu, naweza sema kwa namna moja au nyingne ananiogopa na yuko makini sana hata akiongea na mm ever since). Ilinikera in such a way hata nikiwa naona wafanyakazi wa mzee wana muibia na kumfilisi kwenye business zake nilikua nafurahia and i didn't care at all. (I was like wacha waibe tena sanaaa si anajikuta mjuaji, mama alikuja niambia si vizuri navyofanya hata kama baba yako anaku kwaza. Mi nikawa nakula ganzi tu)
Saa hvi na run my stuff of my own and life z great...na make income yangu ya kutosha sanaa. Nawatumiaga pesa za matumizi and give them all the care in tha world (My mum is always greatful, mzee achukie asichukie, aniletee dharau asilete i really dnt care u kno, mi naangalia mbele tu. Nacho epuka kwa mzee ni mdomo m baya na laana cz najua vitani cost otherwise sina habari.)

Kitu nlicho apa kwa Mungu kamwe sitokaa nimdharau mwanangu kwa namna yeyote ile hata kama kuna vitu flan ana lack kwenye maisha yake cz najua madhara yake na hakuna aliye kamilika duniani. Ukiona mwanao anapungukiwa na kitu/vitu flan u have to be there and very concerned about him/her na kumpa support inamjaza a lot of energy hata ya yeye kujituma na kufanya vizuri. Mtoto akifanikiwa ni furaha na heshima kwa wazazi vice-versa is true. Nakuelewa sanaa unavyo feel. Hata mimi ni mchagga kama wewe, hawa wazee wana ukoloni wa kipumbav sanaa.
 
<br />
<br />


UNAJUA MAGONJWA MENGINE YA WAGANGA YANAITAJI KUTATULIWA NA WANGA WENYEWE KWA ULICHOANDIKAHATA WAKUPELEKE MISIKITI KUMI NA MAKANISA 40 UGONJWA WAKO
NI HATARI ANAUTIBU ALIEKUGAWIA PEKE YAKE

Mbona katoa ushauri mzuri sana!
Ni ww tu hujamuelewa.
 
Ndio tatizo la wazazi wa Kichagga..

Aisee wazazi wote wanapenda sana mtu anaye wawezesha ila wengine huficha hisia ila inabainika inapokuja katika kushirikishwa kutoa maamuzi maana we unakua wa mwisho.


Pia wazazi wana waheshimu wakwe wenye pesa balaa na ni makabila yote yaan kama dasa kaolewa ba muwezeshaji wanamconsider katika family issues utadhani nae kazaliwa huko.All in all tusichoke kutafuta.
 
Hivi wew Ni mwanamke ee...una kizazi ee,beba mimba jifungue lea mtotohadi afikishe miaka 7....alafu leta majibu ya uzi wako...nitakuchangia mawazo maana nikichangia sasa ivi hutanielewa gema..
 
Mungu atunusuruu na vizazi vyetu....


"The truth is hard to swallow when you're choking on your pride."
 
Tatizo wewe hujalijua! Nikwasababu ya kuzaliwa kwenye ukoo wa Panya eti nyie huwa mnafundishwa mkingali waoto wachanga "Principles" za kumiliki hela na kuzitafuta.Sasa kama mamayako alikufundisha zikapita sikio la kulia hadi kushoto basi acha mamayako akuone 'fyatu' maana hukumsikia alichokufundisha Waliomsikia wanakula 'lockcity'.
 
mkuu hata mie mchaga
kwanza hata siendagi moshi kwa sababu sina hela
acha wakae na roho zao za kupenda pesa kuliko jambo lolote
nimetulia na muhehe wangu tunakula maisha,niwe na pesa nisiwe nazo bado napata heshima kutoka kwake
kwanza sitaki demu wa kichaga

Wewe siyo mtoto wa mzee Woisso?
 
Pole mleta mada.
Mi sishangai kabisa, coz sio mama yako tu.. wapo wazazi wengi wa aina hii. Na kinachomfanya akuchukie ni huo huo umaskini (njaa ni mbaya sana monowama).

Jitahidi kutomwonyesha hisia zako lakini pia ni muhimu ukimsamehe.
 
Back
Top Bottom