MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,563
wakuu nina tatizo nimekaa nalo muda mrefu sana moyoni mwangu'
tumezaliwa wanne kwenye familia yetu' sisi ni wachaga na tumekulia na kulelewa na kusoma uchagani'
lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'
baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'
lakini hicho kitendo kilijidhiirisha hata kwa watu wanaotufahamu kijijini kwetu na ilileta matatizo makubwa'
kwa kweli kutoka moyoni mwangu nimejikuta simpendi kabisa mama yangu lakini bado namweshimu kama mzazi wangu'
nikienda nyumbani mara moja kwa mwaka sijisikii kabisa hata kukaa naye hata kwa dakika 10 inakuwa ngumu sana,
niliumia sana kwa kuwa mimi ndiye maskini kabisa na ndiye ambaye sipewi heshima kabisa
naombeni kujua kama kuna mtu mwenye matatizo kama haya na naombeni kujua kama kunaweza kutokea matatizo yoyote katika maisha yangu kwa hilo
nawakilisha.
Kuna somo moja alifundisha alifundisha Mwalimu wa neno la Mungu Mwakasege, linalosema LANGO LA MZALIWA WA KWANZA, ungepata kitabu au CD, ungejifunza kitu kikubwa. Hata hivyo kaka huna option, nikunyenyekea tu, kutubu kwa Mungu, nakuomba hicho kiambaza kiondoke kati yako na mama yako.
Mungu hawezi kukunyima vyote, Yeye ni mwaminifu kwao wamchao na hakika siku moja atasikia sala yako atakuinua kwa wakati wake
Jina la Bwana lihimidiwe

wakuu nina tatizo nimekaa nalo muda mrefu sana moyoni mwangu'

tumezaliwa wanne kwenye familia yetu'

sisi ni wachaga na tumekulia na kulelewa na kusoma uchagani'

lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'

baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'

lakini hicho kitendo kilijidhiirisha hata kwa watu wanaotufahamu kijijini kwetu na ilileta matatizo makubwa'

kwa kweli kutoka moyoni mwangu nimejikuta simpendi kabisa mama yangu lakini bado namweshimu kama mzazi wangu'

nikienda nyumbani mara moja kwa mwaka sijisikii kabisa hata kukaa naye hata kwa dakika 10 inakuwa ngumu sana,

niliumia sana kwa kuwa mimi ndiye maskini kabisa na ndiye ambaye sipewi heshima kabisa

naombeni kujua kama kuna mtu mwenye matatizo kama haya na naombeni kujua kama kunaweza kutokea matatizo yoyote katika maisha yangu kwa hilo

nawakilisha.

hiyo tabia ya mama yako imekuwa kawaida tu siku hizi kwa wazazi wengi. nakushauri msamehe huyo mama kwani naye ni binadamu kama wengine. endelea kumheshimu hivyohivyo na ikibidi uongeze heshima lakini pia uwe na bidii kutafuta kujitegemea kwanza na kisha kama ni mapenzi ya Mungu uwe na mali ya ziada na hata uwezo wa kuwasaidia wengine akiwemo mama yako huyo.

kumbuka kuwa kama hujajitegemea, hilo ndo kikwazo cha kwanza cha wewe kuheshimiwa na watu. jitahidi ujitegemee kwanza. kama tayari unajitegemea, ni vyema lakini usiwe unaomba kusaidiwa na ndugu zako au kupeleka mashitaka nyumbani kwenu kuwa ndugu zako hawakusaidii. jitahidi kupigana peke yako na ikiwezekana shirikiana kwa karibu na marafiki wema ili kuangalia namna ya kunyanyuka kimaisha kwani siku utakaponyanyuka, utaheshimiwa na wote.

mwisho usipuuze haja ya kujiendeleza kwa kutafuta elimu kubwa zaidi. wengi walishindwa kupata maisha mazuri kwa kuyatafuta mitaani, wakayapata kirahisi kupitia darasani. kuna mtu namfahamu ana zaidi ya miaka kumi (10) hajafika kwao kwa sababu kama hizi zako, heri wewe unakwenda kila mwaka! ila yeye alijikita katika elimu na hata sasa yuko nje akipasua kitabu na hiyo imemletea tena heshima katika familia kwani kila mtu anakubali kuwa his future is brighter!

Mungu hawezi kukunyima vyote, Yeye ni mwaminifu kwao wamchao na hakika siku moja atasikia sala yako atakuinua kwa wakati wake

Jina la Bwana lihimidiwe

Pole sana Episodes kwa kufikiria hivyo..Labda kweli na kwa asilimia kubwa labda si kweli.

Michango mizuri imetolewa hapo juu na utakuwa umemsoma "Boss, na pia wengine. Kwanza kabla hujamuhukumu mama yako tafakari vigezo unavyochukua kumuhukumu mama yako. Kuna uwezekano wewe ndiye tatizo au jamii inakufanya uamini mama yako ni tatizo.

Asilimia 98% bila kujali kabila, utaifa, rangi, au unatoka machame upendo wa mama ni wa pekee. Kumbuka moyo wa mama unauwezo wa kutoa machozi ndani kwa ndani kwa miaka mingi..Asilimia kubwa ya kina mama wanashindwa kuwahukumu hata wale watoto wao waliowasaliti..wanawakubatia.lakini mioyo yao inaendelea kulia kwa kushindwa kuwapa furaha. Asilimia kubwa ya kina wanishia kubeba machungu ya maisha ya watoto wao.."mtoto hakuwi kwa mama" kina mama wanajiona wao ndio tatizo kwa jinsi watoto wao wanavyoteseka.

Kuna nafasi kubwa kubwa mama yako anasikitika sana na maisha yako kiasi cha kutoweza kukwambia. Kuna uwezekano mkubwa mama yako hapati usingizi kwa ajili yako akiona wadogo zao wana maisha mazuri..Je wewe unawezaje kujua hili? Kwa kumwangalia jinsi anavyotabasamu wakija wadogo zako?

Kabla hujakata tamaa na kumuhukumu mama yako..Jaribu kujirudi..Mpende mama yako hata kama unajihisi yeye akupendi..ukiweza kujishusha kwa hilo utaweza kusikia kilio cha moyoni cha mama yako na siyo kile kinachotoka mdomoni kwake.

Na isimlaumu sana mama yako.....

Huwezi jua maisha yame mfunza kitu gani...

Inawezekana life haikuwa kind kwake.....

Life was so cruel......so na yeye anatoa kile ambacho life imempa....

Hakuheshimika labda na society kwa umasikini...

So na yeye kwa kuuchukia umasikini,anawachukia mpaka watoto masikini..
watanzania ni watu wenye upendo sana
nashukuru wote mnaochangia hili,na kila wakati ninapata kitu kipya kutoka hapa
nilimtembelea rafiki yangu mmoja na kuona jinsi mama yao anavyoongea nao vizuri japo wao sio matajiri nikatamani ningekuwa ni mimi
ndugu zangu elimu niliyo nayo inanisaidia sana kwenye kazi zangu lakini mimi ni mtu mwenye maisha ya kawaida kabisa na sina mpango wowote wa kutafuta utajiri ili mzazi wangu aniheshimu
mimi namwamini mungu mkuu na ninaamini ninaishi na kumtegemea yeye
huyu mungu akipenda kunipa mali atanipa na hakuna wa kupinga
kila nikisoma comment zenu ninalia machozi
nimeamua kuchukua likizo labda kwenye mwezi wa kumi na nitakwenda kukaa na mama yangu nione kama naweza hili
UMEJAA HEKIMA NA UZOEFU WA MAISHA MISS JUDITH,ANA HERI YEYE ALALAYE AU ATAKAYELALA KWENYE KIFUA CHAKO!!
Such a Wonderful Woman!!
JF Senior Expert Member
Re: kumbukumbu ya siku CHOZI LA DAMU lilipochuruzika jamani, machozi yananibubujika kwa fadhili hizo kuu za Mungu wetu. hakika jina la Bwana ni la kusifiwa sana.napenda niwashirikishe wimbo wa NITAMHIMIDI BWANA ulioimbwa na kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama. wimbo huu umetokana na Zaburi ya 34.
ni wimbo mzuri sana wa sifa na kwa habari ya mtu huyu, sikiliza kwa akini ubeti wake wa pili, hakika utabubujikwa na machozi jinsi Bwana anavyotenda ajabu na ishara nyingi, lol, asante sana Akili Kichwani kwa kumtukuza Mungu kupitia ushuhuda wa rafiki yako. ubarikiwe sana
wimbo: NITAMHIMIDI BWANA
kwaya: Uinjilisti Kijitonyama
Albam: sina hakika
1.
Nitamhimidi Bwana kila wakati, mimi ii,
sifa zake zi kinywani mwangu daima X 2
Katika Bwana nafsi yangu itajisifu,
wanyenyekevu wasikie wakafurahi,
mwimbieni Bwana ninyi pamoja nami,
na tuliadhiishe jina lake pamoja X 2
Kiitikio
Nalimtafuta Bwana akanijibu, milele
Akaniponya na hofu, Milele X2
Onjeni muone,
onjeni, ooh omjeni
onjeni muone, Bwana Yu mwema X2
2.
Nitamhimidi Bwana kila wakati,
sifa zake zi kinywani mwangu daima X 2
Masikini alimuita, Bwana akajibu,
Akamuokoa kwenye tabu, akawa huru,
malaika wa Bwana aja fanya kituo,
Kumzunguka kumuokoa,
Mtu wa Mungu X2
Nalimtafuta Bwana, milele ……………
Glory to God
mkuu mimi ni mwanaume na ni wa kwanza kuzaliwa,wadogo zangu wana uwezo lakini mimi sina uwezo sana ila mungu amenisaidia kuridhika na hali niliyo nayo
mkuu nafikiri mimi ni mtu mwenye moyo laini sana
mtu akishaniudhi inakuwa tabu sana kusahau,lakini nafikiri uwezo nilio nao ni mungu peke yake anaweza kuniongezea
namtegemea muumba wangu najua siku moja nitakuwa na mali kama wanavyotaka lakini kamwe sitaweza kulazimisha hilo