Namtakia afya njema Johnson Mbwambo

Namtakia afya njema Johnson Mbwambo

mfianchi

Platinum Member
Joined
Jul 1, 2009
Posts
12,231
Reaction score
9,088
Nikiwa ni msomaji wa makala ya mwandishi nguli ndugu Johnson Mbwambo napenda kumpa pole na kumtakia afya njema,nimesikia kuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo,namuombea apone haraka ili arudi kwenye kazi yake na ikitiliwa kuwa hiki ni kipindi cha uchaguzi mkuu,uchambuzi wa habari wa ndugu Johnson ni muhimu sana kwa jamii ya watanzania,na kwa hakika tuna umiss mchango wake,kila la kheri comredi Mbwambo Mungu akupe nguvu ili uje utumikie taifa lako katika wakati huu mgumu.
 
I wish you quick recovery J Mbwambo. Nami ni msomaji mzuri wa makala zako.
 
Ugua pole Bw.Johnson Mbwambo! Nakumbuka kusoma makala zake miaka ya tisini na 2000 mwanzoni!
Kipindi hiki alikuwa anaandika makala zake chombo gani cha habari?
 
mimi huwa nasoma kwanza makala zake...
ndio mengine yatafuata......

gazeti la raia mwema bila yeye ni kavu mno...
 
huyu bwana ni kichwa kizuri na amefanya kazi kubwa ya uandishi wa habari za mazingira kupitia JET, mara nyingi humalizia makala zake kwa kusema TAFAKARI, get well comrade.
 
Kuna taarifa zinasema amepelekwa India kwa matibabu zaidi? Mwenye uhakika atuhabarishe tafadhali.
 
Inshalaah tunamtakia afya njema. ni Mwanaharakati mzuri huyu. We miss him kipindi hiki cha hekeheka za Uchaguzi
 
Back
Top Bottom