Polycarp Mdemu
Senior Member
- Jun 2, 2019
- 166
- 209
[emoji1542] Kasoro ya tabia ya mtu huwa na uwezo wa kuipunguza au kuifuta kabisa akiamua.
[emoji1542] Lakini, ili uweze kupunguza Kasoro yako kitabia, Lazima ujue je upo katika kundi lipi katika "Silika" za kawaida za Binadamu,
Katika makala hii ukiona nimeandika neno SILIKA basi jua lina maana kabisa na TABIA KUU ya binadamu.
[emoji1542] Katika somo la Saikolojia "ElimuNafsia" kunakitu huitwa "Silika Nne za Binadamu" Kwa mujibu wa wagiriki yaani "Four Personal Temperaments "
[emoji1542] Tunasema kwa mujibu wa wagiriki kwakuwa wagiriki ndio wagunduzi wa silika Nne, wapo wengine pia kama CARL GUSTAV JUNG huyu alisema binadamu anasilika Mbili, (Wandani na wasiondani)
Pia Kuna silika kadiri ya SUFII, hawa walisema binadamu anasilika 9, ambazo kitaalamu waliziita "enneagram"
Pia kuna silika kadiri ya Warumi ambao wao waligundua Silika kupitia Mwandiko wa mtu, Hivyo mtu alipokuwa akiandika wao walikua wakisoma hasa moyo wake na kupata tabia zake.
TUANZE.............
[emoji1542] LAKINI nini hasa maana ya neno silika?
[emoji1542] Silika ni uinje wa Nafsi, Yaani maelekeo ya ndani mwa binadamu, ambayo huonyesha namna yake maalumu ya Kuwaza kunena mpaka Kutenda. Kiufupi silika ndio huonyesha tabia kuu za binadamu.
[emoji1542] JE silika Hutokana na nini?
Silika huanzia sana katika Either Kurithi kutoka kwa ukoo au familia, Mazingira mtu ambayo amekulia au Utashi wake binafsi.
[emoji1542] Msingi wa Silika ni jinsi yanavyochanganyikana kwa namna tofauti mambo mawili:
[emoji637] WEPESI WA KUHEMKA na
[emoji638] ELEKEO LA KUTENDA
[emoji1542] Silika kadiri ya Wagiriki huwa ni NNE ambazo ni:
[emoji637] Hasira (Choleric,)
[emoji638] Huzuni (melancholic)
[emoji639] Uchangamfu (sanguine)
[emoji640] Upole (phlegmatic)
[emoji1542] Nani hasa ni Mgunduzi wa Silika hizi?
[emoji1542] Mgunduzi hasa ni Mganga wa zamani sana aliyeitwa HIPOKRATE.
[emoji1542] LAKINI Silika ni nyingi, kiasi kwamba toka zamani wataalamu wamejaribu kuzipambanua wasikubaliane.
[emoji1542] Baadhi yao wanasisitizia mwili kama msingi wa silika (kwa Mfano ya watu warefu wembamba, ya watu wafupi wanene, ya watu wenye umbo la wastani).
[emoji1542] Mtazamo huo [emoji1483] una
ukweli fulani, yaani umoja wa binadamu kama changamano la mwili na roho, lakini nafsi inaundwa zaidi na matukio ya maisha, hasa ya utotoni: Ndiyo yanayomuathiri mtu zaidi, pamoja na kwamba anapaswa kurekebisha daima silika yake.
Kwa ajili hiyo ni muhimu ajifahamu ili akuze sifa njema na kupunguza kasoro zake.
[emoji1542] Katika kazi hiyo ategemee sana msaada wa Mungu: Neema ina nguvu kuliko maelekeo yoyote ya umbile na inatenda maajabu, tunavyoona katika maisha ya waliofikia utakatifu kuanzia silika tofauti kabisa.
NEEMA HAIKOMESHI UMBILE, BALI INALIKAMILISHA.
[emoji1542] TUANZE UCHAMBUZI WA SILIKA.
[emoji637] SILIKA YA HASIRA (CHOLERIC)
[emoji1542] Mwenye Silika hii anaitikia mambo kwa kusisimka mara Moja na kwa nguvu, HALAFU athari yake inadumu muda mrefu nafsini mwake.
[emoji1542] Sifa njema ya silika hii tajiri sana ni:
+ Akili kali yaani akili yenye uwezo wa kukamata mengi (ingenuity)
+ Ana uwezo wa kukusanya mawazo mengi
+ Utashi imara,
+ Udumifu na utendaji mwingi,
+ Moyo mkuu na ufadhili.
+ Anachukia Kupumzika na upotevu wa muda.
+ Ana nia na mambo kila mara anavutiwa na mipango mikubwa na kuanza mara kuishughulikia bila woga asirudi nyuma mbele ya matatizo.(decisive and goal-oriented)
+ Mara nyingi anakuwa kiongozi, mtawala au hata mtume mkubwa.
[emoji1542] KASORO ZAKE:
+ Msimamo wake unamuelekeza kuwa mgumu, kutojali, kutakabari, kuwa kaidi, kukasirika.
+ Mara nyingi ana uchu wa madaraka na ukuu.
+ Katika mafungamano hana ulaini wala haelewi sana uchungu wa wengine.
+ Msisimko wake katika utendaji na hamu kubwa ya kufanikisha mipango yake vinamfanya akanyage vipingamizi vyovyote na kuonekana hana moyo.
+ Akipingwa anaweza akawa katili; akishindwa anaweza akatunza chuki hadi saa ya kulipa kisasi.
+ Miguso yake inazama katika ukali wa hisia zake.
[emoji1542] KAMA WW UNA SILIKA HII, FANYA HIVI KUIEPUKA......
+ kwanza usitende harakaharaka, usiamini misukumo ya kwanza kutoka moyoni.
+ Tekeleza unyenyekevu halisi, hurumia walio dhaifu, usimdhalilishe yeyote, usitawale kwa mabavu .
+ Ukifaulu kuratibu milipuko ya hasira yako na kuelekeza vizuri nguvu zako unajipatia upole bora na kuwa wa thamani sana.
+ Kazi ngumu zitafanikiwa mikononi mwako kutokana na utashi na udumifu uliionao.
+ Kwa urahisi fulani unaweza akafikia
utakatifu mkuu.
[emoji638] SILIKA YA HUZUNI (MELANCHOLIC).
[emoji1542] Mwenye tabia au silika hii, anaitikia mambo kwa msisimko ambao mwanzoni ni dhaifu kama anasuasua hivi, na wa shida, lakini unakuwa wa nguvu rohoni na wa dhati akiendelea kuathiriwa;
tena kwa kawaida ni wa muda mrefu yaani hasahau kwa urahisi.
[emoji1542] SIFA NJEMA
+ Miguso yake ni ya ndani, lakini haijitokezi sawasawa na watu wengine tukaona.
+ Kwa kawaida ana akili kali na ya kina, akiivisha mawazo kwa kutafakari kwa utulivu.
+ Anaelekea kukaa pweke (Hupendelea kukaa peke yake) na kufuata ibada na maisha ya kiroho.
+ Hivyo Jambo hili [emoji1483][emoji1483]linaweza mfanya akawa msomi mkavu anayejifungia kutafuta
elimu au mwanasala anayezama katika mambo ya Mungu.
+ Watu kama hawa huvutiwa na masomo ya sanaa ila huufaa upande wa sayansi.
+ Watu wa silika hii ni wagumu kujiingiza kwenye Uhusiano kimapenzi, Lakini akijiingiza hukosa nguvu ya kujitoa, Pia si mwepesi kukata upendo kwa mpenzi wake wa kwanza.
+ Ni mwepesi kuhurumia na kufadhili (hasa wagonjwa), akijitolea hadi ushujaa.
+ Anapatwa na uchungu akiona watu baridi (waliozubaa) na wasio na shukrani.
+ Utashi wake unategemea hali ya mwili: ni dhaifu sana akiishiwa nguvu, kumbe una juhudi akiwa na afya na kupata furaha kidogo.
+ Ni mtu wa kiasi , havurugwi na maono.
[emoji1542] KASORO ZAKE.
+ Hasa ni elekeo kubwa mno kwa huzuni, Matukio ya huzuni humuathiri zaidi kuliko matukio ya furaha.
+ Anaweza akatarajia daima mabaya, akaona magumu tu, akazidisha ukubwa wa matatizo.
+ [emoji1483][emoji1483] Kwa hiyo anakwepa watu, hajitokezi katika kadamnasi, ana aibu, hajiamini, ana wasiwasi juu ya maadili yake yaani hata akitenda zuri huwaza lazima kuna watu huona anajikweza, Hushindwa kuamua, Na hukata tamaa.
+ Katika kuamua Anasitasita sana kwa kuogopa atashindwa, hivyo anapoteza fursa nyingi, Anateseka na bila ya kukusudia anasababisha wengine pia wateseke. Anaweza akapatwa na donda baya nafsini mwake, anapoonja peke yake uchungu wote, kwa kukosa ari ya kuutokeza.
+ Hali hiyo ikizidi na kumfanya adaidai mambo ya pekee au hafai kuishi ki jumuia . Mwenye silika hiyo anapenda kujieleza vizuri katika uongozi wa kiroho, lakini hawezi kwa sababu ya kujikusanya mno kwa ndani yaani hujiona mwenye dhambi sana.
MWENYE SILIKA KAMA HII KUIEPUKA......
+ Kiongozi amuelewe hivyo kutumia busara na adabu sana.
Amsaidie kumtegemea Mungu, kukabili maisha kwa amani na kutarajia mema.
Pia aamini zaidi kuwa anafaa kwa makuu. Kwa kutumia elekeo lake kwa fikara aelewe hana sababu ya kuguswa mno, kuogopa na kujitenga.
+ Pengine apumzike na kula vizuri. Hasa aachane na wasiwasi na woga kwa kuweka maazimio imara na kulenga makuu kwa moyo na tumaini.
[emoji639] SILIKA YA UCHANGAMFU (SANGUINE)
[emoji1542] Mwenye tabia au silika hii anasisimka kwa urahisi na nguvu mbele ya chochote, lakini itikio hilo ni la muda mfupi tu.
+ Kumbukumbu ya mambo yaliyopita haisababishi msisimko tena, Hata akumbuke tukio la huzuni vipi haliwezi kumuathiri.
+ Silika hii ni kinyume cha ile ya huzuni: haina wepesi wa kuhemka, bali inaelekea utendaji.
[emoji1542] SIFA NJEMA YA SILIKA HII.
+ ni msemaji sana mfurahivu, mwenye
heshima kwa wote, msikivu na mtiifu kwa wakubwa, mnyofu na muwazi (pengine kupita kiasi).
+ Anaelekea kusifu mno kuliko hata kulaumu.
+ Hushangaa kuona watu wakichukia utani wake usiofaa, kwa kuwa anaudhani mzuri kabisa(Yaani wakawaida).
+ Hajui ukaidi Anaguswa na kutiwa huruma na matatizo ya watu, halafu anajitolea kweli. Wema wake unapendeza, ari yake inaambukiza na kuvutia wengi.
+ Kwa kuwa ana mapendo, ni mwepesi kufanya urafiki na kuufuata kwa bidii.
+ Akichukizwa anaitikia pengine kwa ukali na ma tusi, lakini anasahau yote mara moja tuu, hatunzi
kinyongo wala Kisasi.
+ Anajua kushughulika kwa kuwa anakabili maisha kwa utulivu, akitarajia daima mazuri, asirudi nyuma mbele ya matatizo.
+ Ana kumbukumbu na ubunifu mkubwa, hivyo hufaulu katika sanaa na mahubiri, lakini hawi mwenye hekima zaidi, kwa kuwa akili yake ni nyepesi, inadaka kwa urahisi, ila haina kina na hupotezea kwa dakika tu.
[emoji1542] KASORO ZA SILIKA HII.
+ Kasoro zake ni kubwa sana hukaa kama sifa njema:
+ Hasa ni ujuujuu, ugeugeu na tamaa za mwili.
- Ujuujuu unatokana na uerevu na urahisi wa fikra unaomfanya adhani ameelewa mara moja suala lolote, kumbe amelihisihisi tu.
+ Ndiyo sababu tathmini zake ni za harakaharaka, mara nyingi si sahihi, pengine hazina ukweli wowote.
+ Katika masomo ni mvivu, anapenda upana wa ujuzi unaoweza kumuonyesha ili kujipatia sifa mbele za watu, kuliko kina chake.
+ Ugeugeu unatokana na ufupi wa muda wa maitikio yake: mara anacheka, mara analia;
ghafla anaacha uchangamfu mkubwa na kupatwa na huzuni kubwa vilevile.
+ Anatubu makosa mapema na kwa moyo, lakini anayarudia katika nafasi ya kwanza, kwa kuwa anasisimka mno, hana nguvu na moyo ashinde tamaa za mwili zinazostawi kutokana na umotomoto wa silika hiyo.
+ Kwake ni vigumu kutawala macho ,
masikio na ulimi wake. Katika sala anatawanya mawazo kwa urahisi.
+ Hapendi sadaka, kujikana, kujitahidi kwa kudumu. Vipindi vya bidii kubwa vinafuatwa na vingine vya kuvunjika moyo.
[emoji1542] MWENYE SILIKA HII AFANYEJE KUIEPUKA.
+ Aelekeze umotomoto wa mapendo yake kwenye lengo bora akichanganyika na Mungu atakuwa mtakatifu mkubwa,
+ Lakini ni lazima ashinde kabisa kasoro zake, Dhidi ya ujuujuu azoee kutafakari na kupima mambo yote, aelewe masuala pande zote, kwa kutabiri matatizo yanayoweza kutokea, asitarajie mema tu.
+ Dhidi ya ugeugeu asitegemee maazimio tu, hata akiyaweka kwa moyo, kwa kuwa atayavunja mara.
+ Amtii kabisa kiongozi wa kiroho, ashike
ratiba ambayo iwe imekubaliwa naye na kupanga yote bila ya kuacha nafasi kwa utashi wake dhaifu.
+ Ajitafiti kwa bidii na kujiadhibu vikali kwa makosa. Katika sala asitafute faraja za kuhisi, bali adumu katika ukavu pia.
+ Dhidi ya tamaa mbaya awe mwangalifu daima, akikwepa nafasi yoyote ya hatari, akikusanya mawazo na kutawala hisi za ndani na za nje, akizuia hasa macho kwa kukumbuka mang’amuzi ya kusikitisha. Amuombe Mungu kwa unyenyekevu na udumifu neema ya usafi ambayo inatoka mbinguni tu.
[emoji640] SILIKA YA UPOLE (PHLEGMATIC)
[emoji1542] Mwenye tabia au silika hii anasisimka kidogo tu. Itikio lake kwa lolote ni dhaifu au halipo kabisa.
+ Haatiriki nafsini mwake kwa kuwa alama yoyote inafutika mara moja.
[emoji1542] SIFA NJEMA ZA SILIKA HII
+ Anatenda polepole lakini kwa mfululizo, mradi asihimizwe juhudi kubwa mno.
+ Hatawaliwi na maono. Hachukizwi sana na matusi, maradhi wala kutofanikiwa.
+ Anadumu kuwa mtulivu, mwenye kiasi na busara.
+ Anajua kukabili maisha, kwa sababu hutafakari sana na kutenda kwa hakika, hufikia malengo yake pasipo kutumia nguvu nyingi kwa kuwa anaondoa vipingamizi badala ya kuvivunja.
+ Anazungumza kwa haki na namna ambayo inaeleweka na kuvutia mbele za watu.
+ Ana moyo mwema, ingawa unaonekana baridi. Ikiwa lazima atajitolea hata kishujaa, lakini si kwa ari na kwa kusukumwa na mwili wake ambao huonekana wa uvivu.
+ Hajitokezi sana Kijumuiya, Kimwili ana sura ya kupendeza, Wengi huwa wanene, mwendo wake huwa wa taratibu sikuzote hata kama anahitajika haraka.
+ Pengine akili yake ni kubwa sana. Watu kama hawa hufaa kwa utafiti wa sayansi unaohitaji uchunguzi wa subira ya muda mrefu, lakini si kwa ubunifu wa mambo mapya.
+ Mwanateolojia Thoma wa Akwino kwa kufaidika na sifa bora za silika hiyo alifanya kazi kubwa kwa utulivu na utaratibu katika kanisa.
[emoji1542] KASORO ZA SILIKA AU TABIA HII.
+ Anapoteza fursa nyingi kwa kuchelewa kuzitumia.
+ Hata katika shida za haraka ni kama amesinzia
+ Hajali sana yanayotokea nje yake yaani hata katika familia yake, Yeye hujali yake tu.
+ Anaishi kama kwa ubinafsi Lakini hapana,
+ Hafai kuagiza(Kuongoza) wala kutawala.
+ Hapendi matendo ya toba na malipizi haamini hatari kuwa atajidhuru kwa hayo!
[emoji1542] MWENYE SILIKA HII AEPUKE KASORO KIVIPI?
+ Anahitaji kuwa na msimamo (wa imani) na kujilazimisha afanye juhudi za mpango na za kudumu. Polepole atafika mbali, mradi aache kusinziasinzia na kuwa mvivu.
+ Badala yake alenge makuu. Ajirekebishe si kwa kujizuia (yaani aige kidogo kutoka kwa mwenye silika ya Hasira na Uchangamfu)
Pia Ajichochee na kuamsha nguvu zilizosinzia.
MWISHO.
[emoji870] Basi Je unaweza kunitajia Kiongozi yeyote mmoja kwenye Kila Silika moja, Pia kama umejitambua, Wewe pia uko katika Silika Ipi?
AHSANTE.
Polycarp Mdemu
translated from the Books Titled "TEMPERAMENT IN HUMAN NATURE" and "PLEASE UNDERSTAND ME "
Link:
en.m.wikipedia.org

Four temperaments - Wikipedia
en.m.wikipedia.org