Nilifika Kibasila Secondary kabisa nikakutana na mwanamke mmoja ambaye nadhani ni Mwalimu pale. Yeye nilipomweleza shida yangu, aliguna tu na kuniomba nimfuate. Akanipeleka kwa Mwalimu mwingine wa kike ambaye kutokana na maandishi kwenye mlango ni Mwalimu mkuu msaidizi. Yeye aliniuliza nina uhusiano gani na huyu ninayemtafuta, nikamweleza. Mwisho alinifahamisha kwa urahisi tu kwamba aliisha hama pale na kwa sasa kadiri anavyosikia anafundisha kwenye shule moja huko Tanga.
Nilihisi kuna kitu walikuwa hawataki kunieleza!!!!!!!!
Tiba