mgoshawampasa
Senior Member
- Jul 30, 2014
- 105
- 27
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29. Nina kazi yangu nzuri, tu lakini mpaka sasa simjui baba yangu mzazi. Sijawahi kuonana naye na sijawahi ona hata picha yake na mama yangu alishafariki lakini kabla hajafariki alinambia baba yangu anaitwa Gerson Jacob Kasanga.
Yeyote anayemjua mtu mwenye jina hilo ambaye alishawahi ishi mkoa wa Tabora wilaya ya Sikonge naomba anitaarifu hapa hapa.
Natanguliza Shukrani zangu za dhati.
=============
Ndugu ajitokeza;
Akiri kumfahamu;
Yeyote anayemjua mtu mwenye jina hilo ambaye alishawahi ishi mkoa wa Tabora wilaya ya Sikonge naomba anitaarifu hapa hapa.
Natanguliza Shukrani zangu za dhati.
=============
Ndugu ajitokeza;
Karibu sana Ndugu yangu..
Mimi naitwa Onesmo Gerson Jacob Kassanga, ni mtoto wa Mr. Gerson Jacob Kassanga ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya magari iitwayo Nyumbu-TATC, iliyopo Kibaha katika kambi ya jeshi...
Ni wenyeji wa sikonge - Tabora na sifa hizo zote ulizozitaja ndizo za baba yetu...
Naomba tuwasiliane 0674329928..
Akiri kumfahamu;
Nashukuru kwa wote mliochangia mada hii. Nimechat na Onecmo na maelezo yake yanaoana na historia yote niliyokuwa nayo na hivyo nashukuru nimempata mzee niliyekuwa namtafuta. Nashukuruni sana.
Kwahiyo japo sifungi mjadala, lakini naamini msako wangu umefika tamati na mengine yatakayoendelea hayawezi kubadili ukweli kwamba nimempata niliyekuwa namtafuta.
Shukrani za dhati kwa Osaka, Onecmo, Jackline, na wengine wote mliojitoa na kutumia muda wenu kunisaidia kumtafuta na kwa kweli ndani ya muda mfupi nimempata baba yangu au at least wadogo zangu ambao nimechat nao.
Lini nitakutana na mzee ni matter of time. Thanks to you all for everything.