Namtafuta baba yangu anaitwa Gerson Jacob Kasanga

Status
Not open for further replies.

mgoshawampasa

Senior Member
Jul 30, 2014
105
27
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29. Nina kazi yangu nzuri, tu lakini mpaka sasa simjui baba yangu mzazi. Sijawahi kuonana naye na sijawahi ona hata picha yake na mama yangu alishafariki lakini kabla hajafariki alinambia baba yangu anaitwa Gerson Jacob Kasanga.

Yeyote anayemjua mtu mwenye jina hilo ambaye alishawahi ishi mkoa wa Tabora wilaya ya Sikonge naomba anitaarifu hapa hapa.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati.


=============

Ndugu ajitokeza;

Karibu sana Ndugu yangu..

Mimi naitwa Onesmo Gerson Jacob Kassanga, ni mtoto wa Mr. Gerson Jacob Kassanga ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya magari iitwayo Nyumbu-TATC, iliyopo Kibaha katika kambi ya jeshi...

Ni wenyeji wa sikonge - Tabora na sifa hizo zote ulizozitaja ndizo za baba yetu...

Naomba tuwasiliane 0674329928..


Akiri kumfahamu;

Nashukuru kwa wote mliochangia mada hii. Nimechat na Onecmo na maelezo yake yanaoana na historia yote niliyokuwa nayo na hivyo nashukuru nimempata mzee niliyekuwa namtafuta. Nashukuruni sana.

Kwahiyo japo sifungi mjadala, lakini naamini msako wangu umefika tamati na mengine yatakayoendelea hayawezi kubadili ukweli kwamba nimempata niliyekuwa namtafuta.

Shukrani za dhati kwa Osaka, Onecmo, Jackline, na wengine wote mliojitoa na kutumia muda wenu kunisaidia kumtafuta na kwa kweli ndani ya muda mfupi nimempata baba yangu au at least wadogo zangu ambao nimechat nao.

Lini nitakutana na mzee ni matter of time. Thanks to you all for everything.
 
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29 nina kazi yangu nzur tu lakini mpaka sasa simjui baba yangu mzazi, cjawahi kuonana naye na cjawahi ona hata picha yake na mama yangu alishafariki lakini kabla hajafariki alinambia baba yangu anaitwa Gerson Jacob Kasanga. Yeyote anayemjua mtu mwenye jina hilo ambaye alishawahi ishi mkoa wa Tabora wilaya ya Sikonge naomba anitarifu hapa hapa.
Natanguliza Shukrani zangu za dhati.

Sasa wewe hujasema jina lako nani na uko wapi, lakini subiri tu utampata dady wako kwamaana ushasema mambo yako swafi
 
Kuna kasanga mwenyeji wa tabora alikuwa dereva wa magari makubwa pale magomeni mapipa ila ndo kashafariki
 
Mdau ni vizuri kumjua baba yako. Ila naona kwa njia hii kama utaleta ugomvi kwa mke wake wa sasa. Just thinking out loud. Lakini kama mke wake ni mtu mzima ataelewa. All the best
 
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29 nina kazi yangu nzur tu lakini mpaka sasa simjui baba yangu mzazi, cjawahi kuonana naye na cjawahi ona hata picha yake na mama yangu alishafariki lakini kabla hajafariki alinambia baba yangu anaitwa Gerson Jacob Kasanga. Yeyote anayemjua mtu mwenye jina hilo ambaye alishawahi ishi mkoa wa Tabora wilaya ya Sikonge naomba anitarifu hapa hapa.
Natanguliza Shukrani zangu za dhati.

Nafesibuku usisahau kuweka tangazo!

Labda huyu hapa chini awe
za kuwa babu yako?


Ila pole bandugu!



 
Mtafute huenda akapatikana,lakini kama bado yuu hai na hakutafuti itakuwa ngumu hata ukionana nae.All the best ndugu.
 
Moja mimi kwa sasa nina miaka 30 kwahiyo yeye atakuwa around 50 and above, na hivyo cmtafuti anipe kitu maana ninajua kutafuta vya kwangu.
Kwa mwenye nia ya kusaidia miaka ya 2007 niliambiwa alikuwa Kibaha Jeshini, Kipindi yuko Tabora alikuwa mwalimu kwahiyo sio dereva. Niliambiwa ni mweupe na mkimya sana kwa tabia. Ni mwenyeji wa Tabora wilaya ya Sikonge.
Mwenye taarifa zozote zinazoweza saidia zitakuwa appreciated
 
Sasa wewe hujasema jina lako nani na uko wapi, lakini subiri tu utampata dady wako kwamaana ushasema mambo yako swafi

Atakayekuwa anamjua mtu mwenye majina hayo ambaye yupo kwenye early 50's ntampa jina langu then tutaongea zaidi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom