Namtafuta baba yangu anaitwa Gerson Jacob Kasanga

Status
Not open for further replies.
Dah!! Hongera sana Mgoshawampasa kwa kumpata baba yako na shukrani za kwanza ni kwake m/mungu kukupa mawazo ya kumtafuta kwa wadau wa jf akijua hakika kuna ndg yako huku atakukutanisha nae na hatmae kumpata baba.
 
Kasanga family ni kweli wanafahamika sana Sikonge. Mwenyewe nilisoma na Mtoto wa Mzee William Kasanga aitwaye Gerard. Mzee William alikuwa katibu wa kanisa la Morravian kama sikosei.

Wengine wanadhani ni wa Iringa ni kweli kabisa. Hili jina kama sikosei ni la Wangoni. Ndiyo maana hata Zambia na Zimbabwe jina hili na Kalonga yapo mengi tu.
Maadamu ndugu mmepatana hongereni sana. Nategemea Wazee wa pande zote mbili watazipokea hizi habari vyema.

Nawatakieni familia nzima ya Kassanga sikukuu njema na mwaka mpya mwema. Good lucky young Men.

Karibu sana ndugu yangu...
Mimi naitwa Onesmo Gerson Jacob Kassanga..Ni mtoto wa mr.Gerson jacob kasaanga,ambaye ni mfanyakazi katik kampuni ya magari iitwayo Nyumbu-TATC,ILIYOPO katika kambi ya jeshi ya nyumbu kibaha...sifa zote ulizozitaja ndizo alizonazo baba yetu...
Tuwasiliane sasa : 0674329928

Thanks, nimechukua namba yako nakupigia ili tuongee vizuri coz the details ulizotoa zinawiyana sana hope ni mwanzo mazuri.
 
Kwa kweli ni kama movie hivi, nmefuatlia koment zote, hakika nimepata uchungu mno!, hope mdau aliyeleta uzi kuna mambo makubwa Mungu amemwandalia mbele yake, nashauri pia mods waanzishe uzi maalum kwa ajili ya watu wenye mikasa kama hii, humu jf wapo wengi sana wenye mikasa kama hii, ila wengine wanakuwa waoga hivi kuanzisha uzi juu ya hili, hongera sana mgoshawampasa kwa uthubutu!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom