Nampongeza Aweda kwa kujilipua na hoja ya madawa ya kulevya ya (Mengi vs Nzowa )ITV , lakini....

Polisi ni janga la kitaifa...ni wauza unga na washirika wa wauza unga wakubwa! Ni juzi polisi wamekamatwa huko Arusha wakisindikiza wauza bangi wakiwa na magunia 8 ya bangi....na inawezekana ile bangi ilikuwa ni kizibiti ambacho polisi waliwauzia raia, na wakaona kuwauzia tu haitoshi hadi wakawasindikiza, tena kwa ku2mia gari la serikali! Shame on policcm!
 
Madawa ya kulevya yanaangamiza watoto wetu.
Hata mimi niliangalia, je, mada ya jana madawa ya kulevya kuendelea kuangamiza vijana wetu, nini kifanyike? AWEDA alimwuliza Nzowa kuwa wewe unatuhumiwa kubambika kesi ya mtoto wa Mengi je, jibu hoja. Yule dada alitaka kumsaidia tu Nzowa. Ukweli swali lilikuwa ndani ya mada kabisa, tena sana.

Nini kifanyike??? sidhani kama swali la AWEDA lilikuwa ndani ya Mada.
 
Ivi umri wa kustaafu Nzoa haujafika? Naona ka vile ni mtu anayesinzia sinzia na kupoteza kumbukumbu.
 
mi niliangalia kipindi toka mwanzo hadi mwisho.aliyemwokoa ni yule mtangazaji wa kike aliyesisitiza asijibu swali lisilotokana na mada hisika

Kwa mantiki hiyo nachelea kusema muongoza kipindi siyo mwoga mwoga bali ni "mpu-mba-vu". Maana tulisubili kusikia kutoka kwa muhusika, lakini yeye akavuruga hoja, kama siyo upumbavu ni nini?
 
Ntoto wa kike yule.Bado anapenda reception yake.Si unawafahamu hawa jamaa kwa acid?Hawafai kabisa.
 
Madawa ya kulevya yanaangamiza watoto wetu.
Hata mimi niliangalia, je, mada ya jana madawa ya kulevya kuendelea kuangamiza vijana wetu, nini kifanyike? AWEDA alimwuliza Nzowa kuwa wewe unatuhumiwa kubambika kesi ya mtoto wa Mengi je, jibu hoja. Yule dada alitaka kumsaidia tu Nzowa. Ukweli swali lilikuwa ndani ya mada kabisa, tena sana.
UTAWALAUMU BURE HAWA WATANGAZAJI WETU FORM FOUR WALIPATA ZERO AU FOUR, hawana upeo wowote, kila mara wanapwaya, yule wa Dk 45 ndo hakuna mtu kabisa, anaandaa kipindi wakati kipindi ndo kinamwandaa yeye
 
Aweda huwa anatuwakilisha wapenda haki na watetea kweli vizuri sana kwenye malumbano ya hoja,ushiriki huu unamjenga kihoja na kumuongezea ujasiri.sijamuona ben saanane kwenye mijadala hii,natamani kumuona pia
 
Jana Aweda alinifurahisha sana kwenye ile kipindi yao ya malumbano ya hoja ya kwenye ITV kuliko mtu mwingine yeyote.
Mada ilikuwa inasema, MADAWA YA KULEVYA KUANGAMIZA VIJANA WETU NA WATANZANIA, NINI KIFANYIKE?

Kamanda wangu Aweda aliibua bifu la Reginald Mengi na Godrefy Nzowa. Nzowa alikuwa amekaa kwenye kiti cha mchokozo mada. Aweda alimwaliza Godfrey Nzowa swali gumu ambalo halikujibiwa. Godfrey Nzowa ni bosi wa kuzuia madawa ya kulevya tena akajisifia kuwa yeye ni bosi wa Tume ya kuzuia madawa ya kulevya kwa miaka saba.

Swali la AweDA,
kuna mtu moja anayeheshimika sana kwenye jamii ya watanzania anaitwa Reginald Mengi na alimtaja wazi. Miaka 2 iliyopita alikutuhumu wewe Nzowa kuwa ulikuwa umetega mtego wa kumbambikia mtoto wa Bwana Reginald Mengi kwa madawa ya kulevya. Je, ni kweli? Halafu akawekaga na chumvi kweye kidonda kwa kuongezesha kuwa ninavyo jua mimi, wewe bado hujakanusha taarifa hiyo. akamalizia kwa kusema tunaomba utupe majibu leo.

Binafsi sijui habari ya Mengi kumtuhumu Nzowa kutaka kumbambikia mtoto wa Mengi kwa madawa ya kulevya ilishia wapi?.

Bahati mbaya Godfrey Nzowa hakujibu na alikaa kimya kama hajasikia na wasimamizi wa kipindi hawakumbana hata kidogo.

Hongera Aweda, lakini taratibu kamanda wangu si unajua kuna tindi kali siku hizi??? Hivi kama wanapanga kumbambikia mtoto wa Mengi madawa ya kulevya, si watamdhuru na yeye Aweda? Namshauri tu kamanda wetu. Nampa Big up.

okey tumekupata bwana Aweda kwa kuja na Id yako nyingine kuja kujifagilia mwenyewe humu JF juu ya kuattend kwako ITV katika mdahalo
 
Kamanda Aweda ameonyesha ujasiri na umahiri wa hali ya juu,hata kama kwao Mbulu level yake ni huko Dar kwenye jimbo la akina "Zungu" wanao tuhumiwa kwa uuzaji "unga"
 
UTAWALAUMU BURE HAWA WATANGAZAJI WETU FORM FOUR WALIPATA ZERO AU FOUR, hawana upeo wowote, kila mara wanapwaya, yule wa Dk 45 ndo hakuna mtu kabisa, anaandaa kipindi wakati kipindi ndo kinamwandaa yeye

Mdau mimi pia nilikua nafuatilia kipindi ila SIKUFURAHISHWA na namna mtangazaji H.Mabumo alivyokuwa ana-interupt wazungumzaji nadhani bado ni mweupe sana kuongoza mijadala mizito ya aina ile,alichokuwa anataka wazungumzaji waongee kama wanajibu maswali ya True & False,hata hajui kuwa kabla huja-conclude issue ni lazima ujenge hoja ndio ufikie mahali pa kusema 'nini kifanyike'....mzee Masako wa kipima joto anajitahidi sana ila hawa wengine wajipange sana!!
 
Nini kifanyike??? sidhani kama swali la AWEDA lilikuwa ndani ya Mada.

Mdau mada controversial kama zile huwezi kurupuka tu ukahitimisha nini kifanyike lazima uipige pige mada kila upande na hapo ndipo utakapowagusa hata wale wenye tuhuma ili mwisho uweze kusema nini kifanyike,ni tofauti na majibu ya ndiyo na hapana!Aweda alikua anaunganisha nukta ili tuelewe kuwa unaposema nini kifanyike nani atafanya (ili sasa uone kuna uwezekano wa kutekelezwa kwa ushauri ukizingatia mtekelezaji ANATUHUMIWA na alipaswa aturidhishe usafi wake na ofisi ambayo Jamhuri imempa)...ndio kusema Aweda alikua sahihi ila tunatofautiana approaches za kujadili mada !
 
[/COLOR]

Naaaam, nimekukubali kwa kumjibu ipasavyo huyo mtu!
 
mfanyabiashara mkubwa kwa sasa ni RITZ1 na MALIMA na serikali inawajua ila watafanyaje
 
Ni kweli Aweda ni wa kupongezwa kwa kujitoa mhanga. Mh Rahis alisema majina ya wauza unga anayo tangu 2006, cha ajabu hadi leo kimya! Hii style yake ya kumaliza mambo kwa kukaa kimya ni ya aina yake na sioni kama inamsaidia yeye mwenyewe au hata Taifa lake analo ongoza! Na ndiyo maana Tanzania imekuwa nchi ya mtukio. Moja baada ya jingine. Leo kuna la madawa, wakazusha la Tindikali amabalo linaweza kuwa na nguvu kuliko la madawa. Waliona watumie tindikali kwa watu wa nje ili liwe na nguvu zaidi kuzima hoja ya madawa kwa vile nayo ni ya kimataifa! Tanzania!?
 
Polisi ni janga la kitaifa...ni wauza unga na washirika wa wauza unga wakubwa! Ni juzi polisi wamekamatwa huko Arusha wakisindikiza wauza bangi wakiwa na magunia 8 ya bangi....na inawezekana ile bangi ilikuwa ni kizibiti ambacho polisi waliwauzia raia, na wakaona kuwauzia tu haitoshi hadi wakawasindikiza, tena kwa ku2mia gari la serikali! Shame on policcm!

POLISI ni taasisi ndani yake kuna àskari. Kama ingekuwa ni dili za taasisi iliwezekana vipi wakamatane wao kwa wao?
 
Alimbana mapumbu almanusura aj_mbe hadharani!
Lile swali lilikuwa mahali pake pale tatizo watangazaji wetu hawako makini, wanaboa, wanajichekeshachekesha kama malay, mahali pa kukaza jicho wao wanalilegeza..

Kweli wewe ni mwenyenchi
 
Last edited by a moderator:
Uozo wa àskari baadhi, usihukum taasisi nzima. Wapo askari waliopo kazin na kazi zao znaonekana kila siku kama wale waliwakamata wenzao wakisafirisha bangi na kuna mamluki ambao kila siku wanatafta gap waharibu.
 
Back
Top Bottom