Mbeya: Mdude Nyagali agoma kupekuliwa na Polisi Nyumbani kwake adai mwanzo walimuwekea madawa ya kulevya

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,746
218,335
FB_IMG_1689424295857.jpg

Mdude Nyagali, mmoja wa wazalendo waliokamatwa na polisi mamluki jana wakati wamemsindikiza Wakili Mwabukusi, bado angali anasota rumande kwa makosa yasiyofahamika.

Bali taarifa zilizotufikia ni kwamba Kamanda Mdude amekataa amri ya Polisi kwenda kumpekua nyumbani kwake hadi pale amri hiyo itakapotolewa na Mahakama.

Ikumbukwe kwamba Jeshi la Polisi liliwahi kudhalilika Mahakamani baada ya kubainika kumbambikia Mdude madawa ya kulevya kwa lengo la kumkomoa.

Msiondoke JF kwa sababu mtumishi wenu Erythrocyte nitaendelea kuwaletea kila kitu kutoka kituo cha Polisi Mbeya.
 
View attachment 2688967

Mdude Nyagali , mmoja wa Wazalendo waliokamatwa na Polisi Mamluki jana wakati wamemsindikiza Wakili Mwabukusi , bado angali anasota Rumande kwa makosa yasiyofahamika

Bali Taarifa zilizotufikia ni kwamba Kamanda Mdude amekataa amri ya Polisi kwenda kumpekua nyumbani kwake hadi pale amri hiyo itakapotolewa na Mahakama .

Ikumbukwe kwamba Jeshi la Polisi liliwahi kudhalilika mahakamani baada ya kubainika kumbambikia Mdude Madawa ya kulevya kwa lengo la kumkomoa .

Msiondoke JF kwa sababu mtumishi wenu Erythrocyte nitaendelea kuwaletea kila kitu kutoka kituo cha Polisi Mbeya
Sema Mdude anamisi sana dhakari ya nyampala wake. Anyway muache a enjoy maisha anayoyapenda
 
Ikumbukwe kwamba Jeshi la Polisi liliwahi kudhalilika mahakamani baada ya kubainika kumbambikia Mdude Madawa ya kulevya kwa lengo la kumkomoa .
RAIS SAMIA: SHIDA YANGU NI JESHI LA POLISI, LINATAKIWA KUTAZAMWA VIZURI
-
Akipokea Taarifa ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za #HakiJinai Nchini, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuna mambo mengi ya kutazamwa na kwenda kurekebishwa ndani ya Jeshi la Polisi japo haungi mkono ushauri uliotolewa wa kuliunda upya Jeshi hilo
-
Amesema “Ningependa Jeshi la Polisi lisimame vizuri kama ni stahiki zao, mishahara, vikokotoo na vingine vingi viangaliwe kwa kuwa lenyewe ndilo lipo kwenye jamii.”
-
#JFUwajibikaji23 #KemeaRushwa #SocialJustice #JamiiForums
 

Attachments

  • jamiiforums-20230715-0001.mp4
    5.2 MB
Sikio linalookoa mali za nchi haliwezi kufa
Mkuu ,
Namuhurumia Mdude,
Naihurumia familia yake pia,

Watu tupo jamii forum tukiandamana nyuma ya keyboard.
Tukitumia fake I'Ds,huku tukipongeza maamuzi ya mdude nyagali ambaye, ukifuatilia posts zake tu utagundua kuna kitu hakipo sawa.

Unadhani kungekuwa na akina mdude elfu tano wenye uthubutu wa kweli kama yeye,nchi si ingefika mbali?

Tuache unafiki,watu wanatakiwa wakae na mdude wamweleze ukweli kuwa , harakati anazofanya ni sahihi,
Lakini anafanya kwenye nchi gani?

Hii nchi ya wanafiki wa Twitter ambao walitengeneza maandamano kisha pale posta wakajitokeza watu kiduchu?

Yaani mdude yupo Selo hujui hata amekula nini, familia aliyoiacha inaishije,wewe unatuambia utatusogezea updates kila kinachojiri,halafu tukijua itasaidia nini wakati hakuna atakayejitokeza akafanya hata mpango wa dhamana.

Naitwa Jack Daniel nimechagua maisha yaliyonyooka sipendi unafiki,napenda ukweli na amani,nipo Yombo,Sigara hapa Pade bar& lounge nakula beer na kuku karibuni.

Pia ongeeni na Mdude kuwa ayafanyayo ni sawa,lakini kwa nchi hii ya watanzania ambao wakiwa mitandaoni ni wakubwa mithili ya Goliathi lakini kwenye ground na maisha halisi ni wadogo kama piriton.

Kama nimekuudhi nisamehe Erythrocyte Mida mibovu hii bia nazo zimechukua nafasi yake.
 
Back
Top Bottom