RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Afisa Polisi mstaafu aliyekuwa mkuu wa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya(ADU) Godfrey Nzowa amesema kuwa baada ya miaka 10 ya kuongoza kitengo hicho cha kupambana na madawa ya kulevya, ametengeneza maadui wengi, ambao kuna kipindi walipanga kumuua.
Bw. Nzowa ambaye alijizolea sifa kutokana na kupambana na wauza madawa ya kulevya kwa kuwakamata baadhi ya wauzaji na kukamata shehena nyingi za madawa hayo.
Bw. Nzowa ambaye kwa sasa anaishi mkoani Arusha amesema kuwa amepata vitisho vingi vya kuuawa katika harakati zake za kupambana na madawa ya kulevya.
Amesema kuwa wauza madawa ya kulevya walijitahidi sana kumshawishi awe kwenye upande wao bila mafanikio, anasema kuwa anakumbuka kipindi muuza madawa ya kulevya mmoja alitaka kumpa hongo ya shilingi bilioni 3.
Kikosi hicho cha kupambana na Madawa ya Kulevya wakati wa uongozi wa Nzowa kilifanikiwa kukamata jumla ya kilo 1,173 za heroini na kilo 395 za cocaine.