DAR: Hili eneo limeshindikana kwa matumizi ya madawa ya kulevya

Itzmusacmb

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
1,531
1,133
Wana JF,
Inaonesha kwamba Polisi wa kanda maalumu ya Dar es salaam chini ya Kamanda Sirro wameshindwa kudhibiti matumizi ya waziwazi ya Madawa ya Kulevya Eneo la Mwenge Jijini Dar es salaam

59a85575643d92180229080b5d86aab9.jpg


Eneo la Mwenge kwenye uwanja wa mpira karibu na Kanisa la KKKT Mwenge ukiiangalia hyo Ramani hapo huo mtaa umepita Upande wa Kushoto wa Kanisa la KKKT (upande huo ni kama unaingia kanisani kupitia lango kuu),hapo mateja ndyo kituo chao maana pembeni ya kanisa hilo kuna Mama mmoja wa Kichaga ananunua chupa za plastic zilizotumika na kuna bwana mmoja ananunua vyuma chakavu na wala hawashtuki kwa Madawa ya Kulevya kutumiwa Hadharani, na IKUMBUKWE eneo hilo ni Nyuma ya Pharmacy ya Nakiete eneo ambalo lina Tuition nyingi ( BRITISH SCHOOL inatazamana macho na eneo hilo) sana za wanafunzi na hii ni hatari sana tena sana ,kama una kijana wako anasoma "eneo hilo" kuwa makini maana halifai kwa Makuzi ya mtoto wako


NOTE: Kesho Nitapiga Picha Mjionee hali halisi

Asante


Picha Hizi Hapa


231605f643691b13c23898d2dafdaa66.jpg



32c4deeee43ca5a0f7cfd828e14bfc9c.jpg



Hao waliosimama ni mateja na hapo "wanasinzia wima " kutokana na arosto ya Unga


71934a38da8eded993ab6d350e2b3244.jpg

4f3a5fc82d9108a7db2c371abb27c5f3.jpg


Hapo chini ndpo wnapokaa na Kutengeneza unga vzuri ili uwe tayari kuvutwa

0814bf53fd3a0e81c2603b1336681cc3.jpg
 
Ile vita ya makonda kiuhalisia nilikuwa ni Sana'a tu na wala isingeweza kuzuia madawa ya kulevya, siku hizi sisikii habari za madawa tena, hii nchi kwa matukio ni balaa.
 
Hizi biashara za watu wa tanga, wadigo wanapenda sana, siwapondi siwachukii ila naamini hata magerezani wamejaa wadigo kwa kesi za unga, wanapenda sana kupiga hela njia za mteremko. fanyeni research mtakubaliana na mimi
 
Si walileta uzi humu kuwa mateja eti wamepungua . Nikasema nyie mnajidanganya na vita yenu feki
 
Napafahamu hapo. Ukitaka ujue hapo ni DRUG FREE ZONE, siku kuwe na mechi hapo uwanjani! Mateja kama wapo Mexico vile!
 
Back
Top Bottom