Nampenda Rais Magufuli ila kwa sheria hii ya fao la kujitoa, nakosa ujasiri wa kusema " MITANO TENA" kwake

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
Kwa wale tunaofanya kazi sekta Binafsi tunafahamu ni kwa kiasi gani sheria hii inatumika Kama kitanzi katika maisha yetu kwani wengi wetu hatuna mikataba ya kudumu hivyo Ni wachache wenye uhakika wa kufanya kazi Mpaka wafikishe umri wa miaka 60 ambao ndo umri wa kustaafu kwa mjibu wa sheria.

Wengi wetu bado ni vijana wadogo na huwa tunategemea pesa inayokatwa kwenye mishahara yetu na kupelekwa NSSF ije itusaidie pindi mikataba yetu inapofikia tamati. Lakin Cha kushangaza, kwa sheria ya Leo hiyo pesa unaambiwa hauwezi kuipata yote Hadi ufikishe miaka 60.

Kweli kwa sheria hii iliyotungwa mwaka 2016 chini ya uongozi wa Magufuli, nakosa ujasiri wa kusema MITANO Tena kwa Magufuli, labada Kama ni miezi na siyo miaka.
 
Kijani na manjano....mbele mbele yao ...kumbe we ni sehem ya waliotuponza, ok acha mi nikomae na Bei ya mafta
 
Sheria hii ilitungwa na kusainiwa enzi za kikwete ila watu walilia Sana na JK akaona isiwe tabu akaamuru watu waendelee kulipwa nssf zao.

Akaingia Magufuli Sasa anaijua hii Sheria maana wakati inatungwa na kupitishwa yeye alikuwa waziri, alichokifanya ni kufata Sheria tuu.
Hapa NI kumwomba asitishe hii Sheria kwenye utawala wake Kama hataki kuifuta ili amwachie rais ajae nae tuone atafanyaje.
 
Sio fao la kujitoa tu,tatizo watu hawasomi hizi sheria kandamizi zinazotungwa na serekali dhalimu ya CCM.Nenda kasome ile sheria inayohusu kurudisha mikopo ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu ndiyo utajua ya kwamba CCM ni takataka!
 
Halafu Hadi ufike hyo sitini hela inakuwa haina thamani, mbona wao bodi ya mikopo wanatuongezea Deni uwe na ajira au lah. Viongozi wa Africa ni kichomi madudu yote haya wanafanya kwa vile hawategemei kura kushinda uchaguzi
 
Hiyo sheria ni kandamizi, watu wanatakiwa warudishiwe pesa yao yote na riba pale tu wanapopoteza ajira. Labda kama mtu mwenyewe aamue kuiacha endapo ana uhakika atapata kazi nyingine ya kumuingizia kipato. Vinginevyo, swala la kujiwekea akiba uzeeni liachwe kwa mhusika mwenyewe kuliko huu ujanja ujanja unaofanyika...
 

Attachments

  • IMG_20210112_150518.jpg
    IMG_20210112_150518.jpg
    86.3 KB · Views: 1
si uliogopa kuingia barabarani kudai haki zako za msingi, sasa pambana na hali yako, hakuna wa kutetea / kuhurumia
 
Nina haki ya kukuita mpumbavu,Yesu kristo mwenyewe alikataa kuitwa mwema Leo wewe unamuita binadamu kuwa ni mwema.Tubu usije mkosea Mungu zaidi ya hapo.
Ndugu kuna Binadamu wana wema
Mtu kua mwema maana yake huyo sio muovu
Rais wetu ni kipenzi cha Watanzania wote isipokua mawakala wa mabeberu
 
Back
Top Bottom