Nampenda lakini nashindwa kumwambia

Nampenda lakini nashindwa kumwambia

thomas_360

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2015
Posts
1,454
Reaction score
1,436
Habarini wakuu

Daaah kuna binti mmoja nampenda sana ila sasa nashindwa kumtokea maana nimetoka kufahamiana naye kama week mbili hivi zimepita na natamani aje kuwa mama wa watoto wangu changamoto iliyopo ameshaniambia kuwa ana boyfriend wake ila kwa anavyosema anatamani apate mwanaume atakaye muoa maana huyo boyfriend wake hana uhakika kama atamuoa ingekuwa wewe ungefanyaje?
 
...hlo mbona jepesi mkuu,si unamwambia tu nataka nikuoe,au kama kisungu kinapanda kupunguza ukali wa maneno na udomo zege unasema plz,I wanna marry u..are u ready?

Au nalo linahtaji ndumba!!!
 
Mbona huelewiki? mbona inaonekana mmeshazungumza vya kutosha tu mpaka akakuambia ana boyfriend na anataka kuolewa ila hana uhakika na huyo b.f wake kama atamwoa. Hapo ndipo ungepaswa uchomeka haja ya moyo wako.

NASIKITIKA SANA KAMA UMEFAHAMIANA NA MTU NDANI YA WIKI MBILI TAYARI UNATAKA KUMWOA
 
Moyo huwa mdanganyifu kuzidi vitu vyote, tena una ugonjwa wa kufisha, wiki mbili ni chache mno kusema kwa hakika kuhusu mtu unayetaka awe mkeo/mmeo, Kama unahisi hivyo kwa sasa muendelee na urafiki, kwa kadri muda unavyoenda mfahamishe nia yako hiyo, ila muombe muda zaidi wa kuchunguzana , mengine yatakua historia!
 
Habarini wakuu...
Daaah..kuna binti mmoja nampenda Sana Ila sasa nashindwa kumtokea maana nimetoka kufahamiana naye Kama week mbili hivi zimepita na natamani aje kuwa mama wa watoto wangu.
Changamoto iliyopo ameshaniambia kuwa anaboyfriend wake Ila kwa anavyosema anatamani apate mwanaume atakaye muoa maana huyo boyfriend wake Hana uhakika Kama atamuoa...ingekuwa wewe ungefanyaje?
Sasa mkuu hapo unashindwa nini
Wakati binti amekupa nafasi ya kumuoa kabisa

Peleka posa alafu uone kama atakataa.
 
Mdomo unakuwa mzito niongee nn cha maana kivipi nimkazie jicho wakati binti kasimama
 
Sasa mkuu hapo unashindwa nini
Wakati binti amekupa nafasi ya kumuoa kabisa

Peleka posa alafu uone kama atakataa.
Daaah...kupeleka posa mapema nayo ni issue nyingine hiyo lazima nimsome kwanza tuone Kama tutakuwa na bright future
 
Back
Top Bottom