Nampenda boss wangu aliyeniajiri

Nampenda boss wangu aliyeniajiri

Habari za jioni guys,

Tafadhari naomba mnisaidie katika ili, naomba niseme wazi mimi siyo timbulo.

Miezi mitatu iliyopita nimeajiliwa na kampuni moja hivi hapa mjini, hiyo kampuni ni ya wahindi na huyo dada ndo HR wa hii kampuni. Baada ya kuajiliwa nilimtumia ujumbe (txt) kumshukuru kwa kuona mimi naweza kufanya nao kazi, akanijibu kwa text akinileza ni jambo la kawaida katika maisha kikubwa ni focus kwenye kazi.

Katika mazingira ya kawaida nimejikuta naanza kumpenda kimapenzi na ninahisi hata yeye ananipenda pia, kwanini nasema na yeye ananipenda pia? Kuna siku tulikuwa na event hapa ofini kwetu mialiko ikatolewa kwa watu mbalimbali na nikamwalika rafiki wangu mmoja wa kike siyo mpenzi wangu wakati wa hafla ikiendelea nilikuwa na huyo rafiki yangu muda mwingi akanifata na kuniuliza mbona umemganda sana huyu dada, kuna mfanyakazi mwenzangu wa kike akamjibu ni wifi yetu huyo, akajibu muwe mnasema jamani akaondoka.

Kesho yake ofisini ikawa story kuhusu mimi na huyo wifi yao waliyenipatia.

Siku nyingine ikatokea safari nje ya mjini ya siku mbili tukatoka mimi, yeye na dereva jioni sasa wakati wa kutafuta hoteli ya kulala, bahati mbaya hotel tulipoenda tukakuta nafasi moja tu yeye akaichukua mimi na dereva tukaenda kutafuta mahali pengine tukaagana turudi pale tukishapata ili tukale chakula pamoja tukakubaliana hivyo.

Muda mchache akanipigia simu akakuta simu inatumika naongea na mtu, baada ya kukata akanipigia tena na akaniuliza ulikuwa unamuaga wifi nini? Na siyo mara moja kuniuliza hivyo nikamjibu mimi nipo single akacheka akaniuliza mmepata room nikamwambia yah! Akasema mje basi.

Nisiwachoshe ni mambo mengi sana, naomba mnisaidie ni jinsi gani ya kumfikishia ujumbe kuwa nampenda maana naogopa maana naweza kumweleza hilo jambo likazua mambo mengine mabaya maana natafuta maisha, niliwahi kumwalika chakula cha jioni akaniambia amechoka siku hiyo ana kazi ya ufuaji hivyo haitowezekana kwa siku hiyo

Uwa nachat nae na kumpigia simu nikitaka kuongelea hayo mambo uwa ananirudisha kwenye maswala ya kazi hata kama hamko kazini

Kuna siku nikamtext wasup kuwa kuna zawadi nimekununulia akataka kuijua zawadi nikamwambia no utaijua siku nikikupatia akasema poa!

Na uwa ananiambia anajua kupika sana, nikamuomba apike siku moja anialike akasema atapika siku ya kuzaliwa kwake na atatualika staff nzima nikamuuliza itakuwa lini? Hakuniambia akasema ni suprise, sasa nikawaza niifanye siku hiyo ya kumweleza hisia zangu kwa kumpelekea zawadi itakayokuwa inasema hisia zangu kwake je ni ipi wadau nisaidieni nampenda sana.
Sasa wewe unaogopa? au mambo hayo ni mageni kwako?.we mwambie kiume,tena atakuheshimu na kukuona wewe ni dume kweli,mwambie "sikiliza wewe mremb,nimetokea kukupenda na nataka tuwe wapenzi,je inawezekana au haiwezekani?,yes or no? nijibu sasa hivi hakuna kuremba we binti",unasita kwani ni dada yako huyo?,mwanamke lazima apandwe tu,isipokuwa damu yako eboooooooooooo.
 
Well said Mshana Jr. Na zaidi epuka mapenzi ya ofcn yatakupotezea focus ya kazi na utaregret maisha yako yote
 
Anza na dinner mengine yatajipa menyewe mtajikuta tu shetani kawapitia mpo kitanda kimoja kama mlivyotoka kwenye matumbo ya mama zenu
Cute shy katika ubora wako!.......na mimi nataka![emoji24]
 
Niliwahi kuhis mtoto wa jaji mkuu wa Tanzania mstaafu ananipenda, kwa jinsi alivyokuwa muda wote niwe naye, tulivokuwa tunawasiliana n.k mi nikajipinda kumwambia!!!! Weewwew mpk Leo najuta, hatuelewani KBS, aliniambia kwa upole X mi nilikuchukulia kama kaka , sasa unafanya nini hiki!!! Sitaki kukumbuka tena.

Mwache atajilengesha mwenyew
Nipe namba ya hiyo dadako aliyekumwaga nimtokee mie ....wewe naye umetoka wap kukuongoza dadako.
 
Mfungukie tu ....
Ishu sio kufunguka ila madhara baada ya kufunguka na hasahasa nafasi ya muajiriwa yeye hapo ofisini iwapo atapigwa kibuti na bosi itabidi BREXIT ihusike......ahahaaaaa
 
dah what if kama boss wako yuko huku na anasoma ulichokiandika?
Namjua boss wake...kajaa telee...he alipoharibu dogo alivyosema party ya oficn alimualika rafiki yake wa kike ....mitoto ya sikuhizi ndio maana waalimu wanaipiga migumi na mibao hovyohovyo....kichwani zero kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom