Nampenda boss wangu aliyeniajiri

Nampenda boss wangu aliyeniajiri

Mkuu, ujumbe wako nimeupata vyema, ila nimevumilia sana huu ni mwaka sijawa kwenye mahusiano hiyo hali pia inaweza kuwa inachangia.
Mwaka hujawa kwenye mahusiano au mwaka hujamvua pitchu kongolo kiumbe wa jinsia tofauti na yako?
 
Item?ukimaanisha nini?Ujue kizungu ndio kwanza unatakiwa unipeleke ist au umesahau?
Daah leo karanja naambiwa nijue kidhungu?,mrembo niliposema ni item nilimaanisha sisi ni kitu kimoja au kwa ligha ingine ni WAPENDANAO mamii, we are an item.
 
Daah leo karanja naambiwa nijue kidhungu?,mrembo niliposema ni item nilimaanisha sisi ni kitu kimoja au kwa ligha ingine ni WAPENDANAO mamii, we are an item.
Mie ndio sijui kidhungu ndio maana nimeomba kutafsiriwa.
Wakati unaongea na meneja wangu fanya mpango wa kuchukua form ist kabisa[emoji1]
 
Mkuu kwa nilivoielewa post yako niseme huyo Boss anakupenda amini hivyo mkuu...
Nilishawahi experience situation km hiyo,sikia sasa kwanza unatakiwa usiende mwendo kasi kabisa anza na dinner na zawadi zawadi si lazima ziwe kubwa hata ndogo tu,mademu wanapenda sana zawadi alafu kwa kipindi hiki unapochat nae jaribu kumjua zaidi yaani kujua nini anapenda nini hapendi hii itakusaidia hata siku ukipanda kumtoa out.Huna haja ya kumtamkia mapema mkuu fanya vitu hivyo nilivokwambia atajileta mwenyewe yaani hata km utamwambia hisia zako wala hutotumia nguvu nyingi mkuu

NB:Usije mtamkia hisia zako katka simu yaani through sms/voice call.
 
Kuna jamaa kaoa dean of students wakati tupo chuo kikuu kimoja hapa Tanzania. Haya mambo yanawezekana.kujiamini tu na wamefunga ndoa ya kanisa. Usitishike na cheo chake. Kikubwa akikubali mzigo ni wa kwako
 
Kwani huyo HR ni boss wako? Yawezekana mko rank moja tu tena yawezekana hata mshahara unamzidi. Si kila hr ni boss wako, boss wako ni yule unaripoti kwake
 
Habari za jioni guys,

Tafadhari naomba mnisaidie katika ili, naomba niseme wazi mimi siyo timbulo.

Miezi mitatu iliyopita nimeajiliwa na kampuni moja hivi hapa mjini, hiyo kampuni ni ya wahindi na huyo dada ndo HR wa hii kampuni. Baada ya kuajiliwa nilimtumia ujumbe (txt) kumshukuru kwa kuona mimi naweza kufanya nao kazi, akanijibu kwa text akinileza ni jambo la kawaida katika maisha kikubwa ni focus kwenye kazi.

Katika mazingira ya kawaida nimejikuta naanza kumpenda kimapenzi na ninahisi hata yeye ananipenda pia, kwanini nasema na yeye ananipenda pia? Kuna siku tulikuwa na event hapa ofini kwetu mialiko ikatolewa kwa watu mbalimbali na nikamwalika rafiki wangu mmoja wa kike siyo mpenzi wangu wakati wa hafla ikiendelea nilikuwa na huyo rafiki yangu muda mwingi akanifata na kuniuliza mbona umemganda sana huyu dada, kuna mfanyakazi mwenzangu wa kike akamjibu ni wifi yetu huyo, akajibu muwe mnasema jamani akaondoka.

Kesho yake ofisini ikawa story kuhusu mimi na huyo wifi yao waliyenipatia.

Siku nyingine ikatokea safari nje ya mjini ya siku mbili tukatoka mimi, yeye na dereva jioni sasa wakati wa kutafuta hoteli ya kulala, bahati mbaya hotel tulipoenda tukakuta nafasi moja tu yeye akaichukua mimi na dereva tukaenda kutafuta mahali pengine tukaagana turudi pale tukishapata ili tukale chakula pamoja tukakubaliana hivyo.

Muda mchache akanipigia simu akakuta simu inatumika naongea na mtu, baada ya kukata akanipigia tena na akaniuliza ulikuwa unamuaga wifi nini? Na siyo mara moja kuniuliza hivyo nikamjibu mimi nipo single akacheka akaniuliza mmepata room nikamwambia yah! Akasema mje basi.

Nisiwachoshe ni mambo mengi sana, naomba mnisaidie ni jinsi gani ya kumfikishia ujumbe kuwa nampenda maana naogopa maana naweza kumweleza hilo jambo likazua mambo mengine mabaya maana natafuta maisha, niliwahi kumwalika chakula cha jioni akaniambia amechoka siku hiyo ana kazi ya ufuaji hivyo haitowezekana kwa siku hiyo

Uwa nachat nae na kumpigia simu nikitaka kuongelea hayo mambo uwa ananirudisha kwenye maswala ya kazi hata kama hamko kazini

Kuna siku nikamtext wasup kuwa kuna zawadi nimekununulia akataka kuijua zawadi nikamwambia no utaijua siku nikikupatia akasema poa!

Na uwa ananiambia anajua kupika sana, nikamuomba apike siku moja anialike akasema atapika siku ya kuzaliwa kwake na atatualika staff nzima nikamuuliza itakuwa lini? Hakuniambia akasema ni suprise, sasa nikawaza niifanye siku hiyo ya kumweleza hisia zangu kwa kumpelekea zawadi itakayokuwa inasema hisia zangu kwake je ni ipi wadau nisaidieni nampenda sana.
Mkuu wewe kurupuka kama dume la ng'ombe lililokata kamba Muulize, bosi samahani una mpenzi/mume? Akisema ndio zuga kiaina, mwambie familia yako itakuwa nzuri sana coz una roho nzuri.
akisema hana mpenzi... endelea na hatua ya pili.. ila tambua kama mambo yakienda kombo unaweza kosa penzi na kibarua.
 
Back
Top Bottom