Nampenda boss wangu aliyeniajiri

Nsumba ntale tz

JF-Expert Member
Apr 19, 2016
713
759
Habari za jioni guys,

Tafadhari naomba mnisaidie katika ili, naomba niseme wazi mimi siyo timbulo.

Miezi mitatu iliyopita nimeajiliwa na kampuni moja hivi hapa mjini, hiyo kampuni ni ya wahindi na huyo dada ndo HR wa hii kampuni. Baada ya kuajiliwa nilimtumia ujumbe (txt) kumshukuru kwa kuona mimi naweza kufanya nao kazi, akanijibu kwa text akinileza ni jambo la kawaida katika maisha kikubwa ni focus kwenye kazi.

Katika mazingira ya kawaida nimejikuta naanza kumpenda kimapenzi na ninahisi hata yeye ananipenda pia, kwanini nasema na yeye ananipenda pia? Kuna siku tulikuwa na event hapa ofini kwetu mialiko ikatolewa kwa watu mbalimbali na nikamwalika rafiki wangu mmoja wa kike siyo mpenzi wangu wakati wa hafla ikiendelea nilikuwa na huyo rafiki yangu muda mwingi akanifata na kuniuliza mbona umemganda sana huyu dada, kuna mfanyakazi mwenzangu wa kike akamjibu ni wifi yetu huyo, akajibu muwe mnasema jamani akaondoka.

Kesho yake ofisini ikawa story kuhusu mimi na huyo wifi yao waliyenipatia.

Siku nyingine ikatokea safari nje ya mjini ya siku mbili tukatoka mimi, yeye na dereva jioni sasa wakati wa kutafuta hoteli ya kulala, bahati mbaya hotel tulipoenda tukakuta nafasi moja tu yeye akaichukua mimi na dereva tukaenda kutafuta mahali pengine tukaagana turudi pale tukishapata ili tukale chakula pamoja tukakubaliana hivyo.

Muda mchache akanipigia simu akakuta simu inatumika naongea na mtu, baada ya kukata akanipigia tena na akaniuliza ulikuwa unamuaga wifi nini? Na siyo mara moja kuniuliza hivyo nikamjibu mimi nipo single akacheka akaniuliza mmepata room nikamwambia yah! Akasema mje basi.

Nisiwachoshe ni mambo mengi sana, naomba mnisaidie ni jinsi gani ya kumfikishia ujumbe kuwa nampenda maana naogopa maana naweza kumweleza hilo jambo likazua mambo mengine mabaya maana natafuta maisha, niliwahi kumwalika chakula cha jioni akaniambia amechoka siku hiyo ana kazi ya ufuaji hivyo haitowezekana kwa siku hiyo

Uwa nachat nae na kumpigia simu nikitaka kuongelea hayo mambo uwa ananirudisha kwenye maswala ya kazi hata kama hamko kazini

Kuna siku nikamtext wasup kuwa kuna zawadi nimekununulia akataka kuijua zawadi nikamwambia no utaijua siku nikikupatia akasema poa!

Na uwa ananiambia anajua kupika sana, nikamuomba apike siku moja anialike akasema atapika siku ya kuzaliwa kwake na atatualika staff nzima nikamuuliza itakuwa lini? Hakuniambia akasema ni suprise, sasa nikawaza niifanye siku hiyo ya kumweleza hisia zangu kwa kumpelekea zawadi itakayokuwa inasema hisia zangu kwake je ni ipi wadau nisaidieni nampenda sana.
 
Sijui uhalisia wa hii post lakini kama kuna kosa kubwa utafanya katika maisha yako ni hilo unaloliombea ushauri
-anaweza kuona dalili na akatia timu lakini kubali kifuatacho ITV
-anaweza kuwa mweledi na mwenye msimamo akakufukuza kazi
-anaweza kuwa ni fisi maji ukaishia kuumia
Epuka mahusiano na mtu anayekulipa mshahara
 
Ahsante kwa ushuri mkuu.
 
Binafsi kama ulivyoeleza ndivyo sioni kuwa hizo ni dalili za yeye kukupenda...nafikir wewe hisia zako zimezidi sana juu yake kias kwamba unaona kuwa anakuhitaji....
Kuna siku alimfanyia suprise mfanyakazi mwenzetu katika siku yake ya kuzaliwa akaandaa kapart kadogo tu kwake, akanipigia simu nifike kwake, nikaenda pia wafanyakazi wenzangu nao walijulishwa na kufika, wakati wakupiga picha nikapiga nae nilikuwa na glass ya wine nikwambia au nikunyweshe wakati tunapigwa picha akasema wewe tu akawa amenishika kiunoni hisia zilinipanda ghafla mkuu nikataka kumweleza
 
Kuna nyakati kwenye maisha yetu...tunatakiwa kutambua namna ya kudeal na hisia zetu......hasa katika mazingira ambayo si muafaka kwa hilo unalotaka kulifanya......,
Na njia muafaka ya kudeal na hali hiyo na kuangalia ni kuangalia hasara na madhira ya wewe kutenda hilo ambalo hisia zako zinakutuma kulifanya........

Hisia za matamanio ni za kawaida kwa kila mwanamume aliye kamirika.....lakini si lazima kukidhi kila haja za matamanio hayo.......na huo ni ukomavu wa kiume......

Unatakiwa baadhi ya mambo uyapuuzie kwa manufaa ya mambo mengine muhimu zaidi kwenye maisha yako.......

BE A GENTLEMAN......
 
Ahsante mkuu kwa ushauri wako mzuri, nitaufanyia kazi.
 
Kuna siku alimfanyia suprise mfanyakazi mwenzetu katika siku yake ya kuzaliwa akaandaa kapart kadogo tu kwake, akanipigia simu nifike kwake, nikaenda pia wafanyakazi wenzangu nao walijulishwa na kufika, wakati wakupiga picha nikapiga nae nilikuwa na glass ya wine nikwambia au nikunyweshe wakati tunapigwa picha akasema wewe tu akawa amenishika kiunoni hisia zilinipanda ghafla mkuu nikataka kumweleza
Ana mtu?
 
Back
Top Bottom