Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 3,564
- 3,472
Leo mtu akitokea na kuwauliza waumini wengi wa makanisa ya kiroho swali la Je! ni kweli tutakwenda mbinguni?.Bila shaka wengi watajibu ndiyo na sababu watakayoitoa kubwa ni kwamba wamempokea na kumkiri Yesu kama Bwana na Mwokozi. Lakini pamoja na jibu hilo bado siyo sababu kuu ingawa ni sehemu tu. Ipo namna ambayo Mungu ameifanya kwa watu kupata wokovu na kudumu katika wokovu.
Changamoto kubwa leo watu wengi wanakiri vitu wasivyovielewa Kwa mfano mtu akija akikuambia ipo jehanamu ya moto, jehanamu ni halisi, ukifa utaingia motoni unaweza kujenga hofu ila ukweli hatuingii mbinguni kwa sababu sababu ya kukwepa au kuogopa moto.
Wahubiri wengi leo wamesahau kabisa kufundisha juu ya misingi aliyoiweka Mungu inayowaunganisha wanadamu na wokovu. Wayahudi walipata nafasi ya kwanza ya wokovu kwa sababu ya misingi yao ya ufuasi na Mungu alijidhihirisha kwao kupitia utamaduni huo wa ufuasi. Mungu alijidhihirisha kwao kama Mungu wa Baba zao, waliishi katika misingi hiyo ya ufuasi kiasi kwamba walipoikiuka walipata mapigo.
Angalia jambo la hatari itakuwaje siku ya mwisho mtu anaambiwa na Mungu toka sikujui?.Unamueleza Mungu kuwa ukifanya unabii n.k Kwa kina lake halafu anasema hakujui!..Hii ina maanisha mtu anaweza kuwa muongofu wa imani na anajitoa sana katika masuala mbalimbali mahali anaposalia lakini yeye asitambuliwe na Mungu ila yule aliyewasaidia masikini Kwa kumpatia chakula, maji na mavazi, aliyewaona wafungwa Mungu akamwona ni mwenye heri kwa sababu alimsaidia alipokosa chakula, alimvisha alipokosa mavazi n.k.
Hii inaonesha yale unayowafanyia wengine ndiyo utamaduni uliojifungamanisha nao na ndiyo utakaokuwezesha kumuona Mungu ila siyo kukiri usiyoyafahamu. Hatutakiwi kukiri jambo tusiloliamini au tusilolifamu wala kuwa na uhakika nalo "you should not make confession to what you are not convicted by". Ibrahimu alihesabiwa haki sababu ya kuwa na imani thabiti "conviction".Uhakika wako ndiyo unaokupelekea wokovu.
Jiulize taratibu tu ni kwa nini leo nyumba za ibada zimejaa watu wanaosema wameokoka lakini wanatenda dhambi? Biblia inasema aliyeokolewa hatendi dhambi tena lakini ikitokea mtu anasema ameokoka na anaendelea kutenda dhambi kuna tatizo mahali. Inawezekana mtu huyo kuna hatua za mdsingi alizikosabna huenda aliyemuongoza mtu huyo alimwelekeza kufanya matamko tu ya kukiri na siyo katika uhakika wa mabadiliko ya mtindo wa maisha. Tunapoongoka sharti tupokee na mtindo wa maisha.
Hatupati wokovu Kwa kutamka tu 'tumeokoka' ila ni kwa kuwa na uhakika na imani dhabiti moyoni. Wokovu ni pale vitu vinavyoanza kubadilika ndani ya moyo wako na kuanza kufahamu maisha bila Yesu ni bure. Mtu huanza kutamani kuwa na Mungu, kumuona kuliko kitu chochote kile. Ila ukiona una mashaka mfano unajiuliza hivi Yesu akirudi mara ya pili nitanyakuliwa au la!.. ukiona una swali la aina hiyo elewa hautaiona pepo na haujaokoka au wewe siyo Mkristo bado.