Namna ya kupunguza msongamano wa Maroli yanayokuja ndani ya mji kushusha mzigo kwenye ICD

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,957
12,550
Changamoto ya foleni ya Malori yanayoingia katikati ya mji wa Dar kwenye Bandari kavu (ICDs-Inland Container Depots) na yards za kushushia mizigo inabidi itatuliwe kwa wamiliki wa Bandari kavu na Yard kuwa na mfumo wa Tehama.

Huu mfumo itabidi kila Bandari kavu wanapopata order ya magari ya kushusha list ya magari, Dereva akifika Chalinze au Misugusugu inabidi atoe taarifa kwa kujisajili kimtandao kwenye yard husika.

ICD baada ya kuliingiza gari kwenye mfumo, ambao utakuwa na taarifa ya gari kufika,idadi ya magari yaliyo nje yanasubiri kuingia mjini kushusha. Yard/ICD itakuwa na uwezo wa kuingiza idadi ya magari ambayo wanaweza kuyahudumia kwa parking na kushusha bila kuweka msongamano.

Faida za mfumo itasaidia kujua takwimu za magari yanayoingia kushusha kwa siku, magari yanayosubiri kushusha mzigo yaliyo ndani ya mji na nje.Kuondoa foleni nje ya ICD na kupunguza usumbufu kwa madereva kutafuta sehemu za maegesho kabla ya kushusha mzigo na kuepusha kukamatwa kwa kuegesha eneo lisilo sahihi.
 
Changamoto ya foleni ya Malori yanayoingia katikati ya mji wa Dar kwenye Bandari kavu (ICDs-Inland Container Depots) na yards za kushushia mizigo inabidi itatuliwe kwa wamiliki wa Bandari kavu na Yard kuwa na mfumo wa Tehama...
Kwala containers' terminal inaanza lini? Ndio ilikuwa suluhisho.
 
Back
Top Bottom