Namna pekee ambayo wanawake wanaweza kutukomoa wanaume tukaumia au kuharibu future yetu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,652
52,485
Kwema Wakuu!

Juzi kuna dada mmoja alinicheki na kuniomba ushauri kuwa afanyeje ili amkomeshe kijana mmoja ambaye kwa madai yake anasema amemkatili.

Sisi wanaume wengi wetu hatukomolewi wala kuumizwa na Matusi yenu.
Sisi wanaume wengi wetu hatuumizwi wala kukomolewa na maringo au kejeli au kujishaua kwenu. Mashauzi ya Mwanamke hayamuumizi mwanaume kamili.

Sisi wanaume kuna mambo ukitufanyia tunasema eehee! Hapa nimepatikana. Au hapa nimejichanganya au nimeingia cha kike.

1. Kutubambikia watoto.
Hii ndio komesha. Yaani hakuna kipigo heavy kama hiki. Unalea mtoto miaka nenda rudi ukijua ni wako alafu katika umri wa ubuda, utu uzima unajua unamadume au majike yako kadhaa kumbe umepigwa. Hapa sio poa.

2. Kubeba Mimba wakati tulikuwa kwenye tamaa zetu
Hakuna kitu wanaume tunachukia na kuona tumewezwa kama Mwanamke ambaye tumemtamani tuu abebe mimba. Aiseeh!
Hakuna taarifa mbaya kama kusikia Mwanamke ambaye ulimtamani tuu kwa tamaa zako kabeba mimba.😀😀

Fikiria Mwanamke unayemuingiza ghetto kwako kimagendo kama madawa ya kulevya alafu akuambie amebeba mimba. Ni taarifa mbaya sana.

Ingawaje wanaume hatusemagi lakini huo ndio ukweli wenyewe.
Hiyo ipo pia kwa wanawake, inaweza kuwa hajakupenda na hakuwa na mpango wa kukubebea mimba ila tamaa zake tuu iwe za kimwili au kipesa anajikuta Kitu imetiki.

3. Kula Pesa ya Mwanaume alafu usimpe Mchezo.
Kwa sisi wengine tupo radhi utunyime huo mchezo lakini kamwe hatuwezi kukupa pesa kabla ya mchezo.

Pesa inauma Aiseeh!
Tuma nauli, sijui yakutolea, alafu usitokee. Dadeki inauma kweli.

4. Usaliti.
Usaliti unauma ingawaje sio kwa Watu wote. Kwa sababu wapo Watu wanaotarajia kusalitiwa. Usaliti unaouma ni ule ambao mtu hatarajii wala hata kuamini ipo siku atamfumania mwenza wake.

Baada ya dondoo hizo naamini nimetoa ufahamu wa Watu kujua namna ya kukabiliana na Ishu kama hizo endapo zikitokea.

Kwa kijana unayetafuta maisha, linda sana jasho lako(pesa yako), kwa wakiondoa ni vizuri kuwa makini na watoto utakaoambiwa ni wako kwa sababu pigo hilo hutoa ushindi katika dakika za mwisho kabisa za nyongeza, hapo ukisikia unazikwa kesho yake.

Dunia sio salama kivile. Ishi kwa tahadhari.

Wasalamu
 
Mi naona hapo ni kupata mtoto na kumtelekeza….hapa mwanaume atajifanya hajali wala nini lakini ukweli ni kuwa hii huwa inawatesa mpaka mwisho wao wa pumzi….damu yako ni damu yako tu.vaeni condom wakuu wanawake wengi hatujui kutumia kalenda🥴
 
Mi naona hapo ni kupata mtoto na kumtelekeza….hapa mwanaume atajifanya hajali wala nini lakini ukweli ni kuwa hii huwa inawatesa mpaka mwisho wao wa pumzi….damu yako ni damu yako tu.vaeni condom wakuu wanawake wengi hatujui kutumia kalenda🥴

Ushauri mzuri ni kuwa Watu waache zinaa.

Ni kweli wanawake wengi hawajui kusoma kalenda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom