Namkumbuka: Juma "Babu" Duni Haji 1995

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
MWENYEKITI WA TAIFA ACT WAZALENDO JUMA ‘’BABU’’ DUNI HAJI: NINAVYOMKUMBUKA

Kuna kitu katika haiba nzima ya wanasiasa walio katika upinzani Zanzibar ambacho ni tabu kukieleza kwa maneno haya yetu ya kawaida.

Kuna picha kila nikiiangalia machozi yananilenga.

Ismail Jussa yuko kwenye ''wheelchair,'' ameshika beleshi anatia mchanga kwenye kaburi la Maalim Seif.

Yuko kwenye kiti cha magurudumu hawezi kusimama.

Amepigwa wakati wa uchaguzi.

Nimeangalia mapokezi makubwa aliyopewa leo Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa Juma Duni Haji.

Nimeangalia umma uliotoka kumpokea yeye na viongozi wenzake.

Hakika mapokezi haya yanasema mengi.

Historia ya Zanzibar ni historia iliyojaa mengi majonzi na majonzi haya hayakuchagua yamewafika wanachama wa kawaida na viongozi.

Haya si mambo ambayo mtu ungependa kuyarudia kuyaeleza tena na tena kwani kufanya hivyo ni kurejesha machungu.

Nimesikiliza hotuba ya Mwenyekiti Juma duni Haji.

Hotoba safi sana yenye utulivu na kuonyesha njia.

Wazanzibari wamemwitika.

Wazanzibari wameitika kama walivyoitika, ''Shusha Tanga Pandisha Tanga Safari Iendelee.''

Kuna kitu nakiona kwa Juma Duni.
''Humility'' yaani unyofu.

Nuona unyofu wa hali ya juu sana na si kama nilikuwa siujui.

Hakuna makeke kwenye haiba yake wala kwenye maneno yatokayo kinywani mwake.

Siku zote nimsikilizapo Juma Duni Haji ujumbe wake ni In Shaa Allah Zanzibar itatulia na haki itasimama.

Hata mimi hili naamini bila ya chembe ya shaka kuwa Zanzibar itarejea kuwa njema na atakae kuingia visiwani atabisha hodi na mlango atafunguliwa kama ilivyokuwa zama.

Mara ya kwanza kukutana na Juma Duni Haji ilikuwa mwaka wa 1995 na alikuja naamini akitokea Uwanja wa Ndege moja kwa moja hadi Starlight Hotel ambapo mimi na wenzangu (sotowataja majina) tulikuwa chumbani kwa marehemu Maalim Seif tunafanya mazungumzo ya vipi tutaijenga CUF Tanzania Bara.

Juma Duni alikuwa anatokea masomoni Uingereza.

Juma Duni alikuwa amevaa suti ya rangi ya majivu iliyomkaa vyema.

Hii ndiyo siku ya kwanza nilipomfahamu Juma Duni.

Sote tuliokuwa ndani ya chumba kile tulikuwa vijana pamoja na kiongozi wetu Maalim Seif, sote tulikuwa vijana tunapendeza ukitutizama.

Nakuwekea hapo chini picha niliyompiga ‘’Babu,’’ kama wapenzi wake wanavyopenda kumwita umuone Babu Duni alivyokuwa kijana.

Picha hii nimempiga Juma Duni Korogwe wakati wa kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka wa 1995.

Pembeni ya Juma Duni yuko Prof. Ibrahim Lipumba na kuliani kwake ni Mzee Hassan Onari aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Tanga mjini.

Picha hii inanikumbusha mbali sana.

Tulitoka Korogwe tukafanya mkutano mwingine siku hiyo hiyo Muheza kituo cha mabasi na jioni tukaingia Tanga mjini kwa ajili ya mkutano mkubwa siku ya pili.

Naam.

Mkutano wa Tanga wenyeji wetu walitueleza kuwa haukupatapo kutokea hata wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika Nyerere na Bi. Titi Mohamed walipohutubia mkutano wa kwanza wa TANU kiwanja cha Tangamano mwaka wa 1955.

Juma Duni alipanda jukwaani kwanza kisha Prof. Lipumba akaja kuhitimisha.

CUF ilikuwa imepokelewa kwa kishindo kikubwa Tanga.

Toka asubuhi, ‘’mood’’ ya mkutano yaani hamasa ya mkutano ilianza kuonekana mfano wa mechi ya fainali katika ya African Sports na Coastal Union enzi zao.

Tanga usafiri mkubwa ni baiskeli na kila baiskeli ukiiangalia ilikuwa ina bendera ya Lipumba na mwendeshaji akipiga kengele hata bila sababu kuashiria kuwa leo kuna jambo kubwa.

Mitaa yote ya Ngamiani, Tanga Mjini ilishamiri picha za Prof. Lipumba pamoja na T Shirt zenye picha yake.

Mkutano ule uliinyongesha sana CCM Tanga.

Kuna picha mbili za Juma Duni naziweka hapo chini tukiwa Ngamiani nyumbani kwa marehemu Mama Ummy bint Anzuani aliyetualika kwake na kutufanyia dhifa kubwa sana.

Katika picha moja nipo.
Naamini haitakuwa tabu kunitambua.

Nje ya nyumba ya Mama Ummy walijaa wanachama wa CUF waliotusindikiza kwa maandamano kutoka Tangamano hadi Ngamiani.

Naweka ukurasa kutoka shajara (diary) yangu msomaji wangu usome uone hali ilivyokuwa Tanga siku ile sasa miaka 27 imepita.

Kila fursa niliyopata nilijitahidi kumueleza Juma Duni historia ya siasa za Tanganyika.

Juma Duni Haji leo ni kiongozi mkubwa Zanzibar na uongozi wake In Shaa Allah utatengeneza hali ya baadae ya nchi yake.

Kwa miaka mingi tumekuwa pamoja ingawa mimi niko Tanganyika na nimeshuhudia kila msukosuko uliomfika akiwa ubavuni kwa Maalim.

Juma Duni kafungwa na Komando na Komando akasema akae ndani yeye si papai kuwa ataoza.

Kama niliposema hapo awali historia ya Zanzibar imegubikwa na simanzi nyingi na inakuwa tabu kuieleza historia hii bila hata kwa mbali kugusia misiba hii.

Juma Duni amesema katika hotuba yake hii ya leo kuwa ni tegemeo lake kuwa Zanzibar itafanya uchaguzi wa wa 2025 kwa amani.

Hapo kwenye uchaguzi wa 2025 ndipo ulipo mtihani mkubwa kwa Wazanzibari na yeye Juma Duni.

Nilikuwa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa 1995 siku ya pili uvumi ulipozagaa kuwa CUF imeshinda uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.

Waingereza wana msemo, ''The rest is history,'' yaani kilichobakia ni historia.

Namtakia kila la kheri rafiki yangu Juma ‘’Babu,’’ Duni Haji.

Hakika miaka mingi imepita.

Screenshot_20220202-164517_Facebook.jpg
 
Pembeni ya Juma Duni yuko Prof. Ibrahim Lipumba na kuliani kwake ni Mzee Hassan aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Tanga mjini.

Picha hii inanikumbusha mbali sana.

Tulitoka Korogwe tukafanya mkutano mwingine siku hiyo hiyo Muheza kituo cha mabasi na jioni tukaingia Tanga mjini kwa ajili ya mkutano mkubwa siku ya pili.

Naam.

Mkutano wa Tanga wenyeji wetu walitueleza kuwa haukupatapo kutokea hata wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika Nyerere na Bi. Titi Mohamed walipohutubia mkutano wa kwanza wa TANU kiwanja cha Tangamano. mwaka wa 1955.

Juma Duni alipanda jukwaani kwanza kisha Prof. Lipumba akaja kuhitimisha.

CUF ilikuwa imepokelewa kwa kishindo kikubwa Tanga.

Toka asubuhi, ‘’mood’’ ya mkutano yaani hamasa ya mkutano ilianza kuonekana mfano wa mechi ya fainali katika ya African Sports na Coastal Union enzi zao.

Tanga usafiri mkubwa ni baiskeli na kila baiskeli ukiiangalia ilikuwa ina bendera ya Lipumba na mwendeshaji akipiga kengele hata bila sababu uashiria kuwa leo kuna jambo kubwa.

Mitaa yote ya Ngamiani, Tanga Mjini ilishamiri picha za Prof. Lipumba pamoja na T Shirt zenye picha yake.

Mkutano ule uliinyongesha sana CCM Tanga.

Kuna picha mbili za Juma Duni naziweka hapo chini tukiwa Ngamiani nyumbani kwa marehemu Mama Ummy bint Anzuani aliyetualika kwake na kutufanyia dhifa kubwa sana.

Katika picha moja nipo. Naamini haitakuwa tabu kunitambua.

Nje ya nyumba ya Mama Ummy walijaa wanachama wa CUF walitusindikiza kwa maandamano kutoka Tangamano hadi Ngamiani.

Naweka ukurasa kutoka shajara (diary) yangu msomaji wangu usome uone hai ilivyokuwa Tanga siku ile sasa miaka 27 imepita.

Kila fursa niliyopata nilijitahidi kumueleza Juma Duni historia ya siasa za Tanganyika.

Juma Duni Haji leo ni kiongozi mkubwa Zanzibar na uongozi wake In Shaa Allah utatengeneza hali ya baadae ya nchi yake.

Kwa miaka mingi tumekuwa pamoja ingawa mimi niko Tanganyika na nimeshuhudia kila msukosuko uliomfika akiwa ubavuni kwa Maalim.

Juma Duni kafungwa na Komando na Komando akasema akae ndani yeye si papai kuwa ataoza.

Kama niliposema hapo awali historia ya Zanzibar imegubikwa na simanzi nyingi na inakuwa tabu kuieleza historia hii bila hata kwa mbali kugusia misiba hii.

Juma Duni amesema katika hotuba yake hii ya leo kuwa ni tegemeo lake kuwa Zanibar itafanya uchaguzi wa wa 2025 kwa amani.

Hapo kwenye uchaguzi wa 2025 ndipo ulipo mtihani mkubwa kwa Wazanzibari na yeye Juma Duni.

Nilikuwa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa 1995 siku ya pili uvumi ulipozagaa kuwa CUF imeshinda uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.

Waingereza wana msemo, ''The rest is history,'' yaani kilichobakia ni historia.

Namtakia kila la kheri rafiki yangu Juma ‘’Babu,’’ Duni Haji.

Hakika miaka mingi imepita.

View attachment 2105446
Yuko wapi Lipumba siku hizi?
 
..kuuwawa kwa Aboubakar Khamis Bakari kumenisikitisha mno.

..Na ni maoni yangu kwamba chama cha ACT hakijauenzi vya kutosha mchango wa Aboubakar Khamis Bakari.
 
Uchaguzi wa mwaka 1995 ulikua moto kweli kweli, laiti kama Lipumba (CUF ) wangekubali kuungana na Mrema wa NCCR Mageuzi hakika Mkapa asingekua raisi ingawa kuna siku niliwahi msikia Lipumba akikiri kwenye moja ya interview zake kwa TV kwamba Mrema alishinda ule uchaguzi, it was very hot
 
..Nimemsikia Babu Duni akidai Chadema / Ukawa walishinda Uraisi mwaka 2015 ila wakatangazwa wengine.
 
Nanukuu"Juma Duni Haji leo hii ni kiongozi mkubwa Zanzibar"kwanini umesema hivi wakati Babu Duni ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa yaani Tanzania yote?
 
Shukrani sana Mohamed Said kwa kumbukumbu nzuri ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995!
 
MWENYEKITI WA TAIFA ACT WAZALENDO JUMA ‘’BABU’’ DUNI HAJI: NINAVYOMKUMBUKA

Kuna kitu katika haiba nzima ya wanasiasa walio katika upinzani Zanzibar ambacho ni tabu kukieleza kwa maneno haya yetu ya kawaida.

Kuna picha kila nikiiangalia machozi yananilenga.

Ismail Jussa yuko kwenye ''wheelchair,'' ameshika beleshi anatia mchanga kwenye kaburi la Maalim Seif.

Yuko kwenye kiti cha magurudumu hawezi kusimama.

Amepigwa wakati wa uchaguzi.

Nimeangalia mapokezi makubwa aliyopewa leo Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa Juma Duni Haji.

Nimeangalia umma uliotoka kumpokea yeye na viongozi wenzake.

Hakika mapokezi haya yanasema mengi.

Historia ya Zanzibar ni historia iliyojaa mengi majonzi na majonzi haya hayakuchagua yamewafika wanachama wa kawaida na viongozi.

Haya si mambo ambayo mtu ungependa kuyarudia kuyaeleza tena na tena kwani kufanya hivyo ni kurejesha machungu.

Nimesikiliza hotuba ya Mwenyekiti Juma duni Haji.

Hotoba safi sana yenye utulivu na kuonyesha njia.

Wazanzibari wamemwitika.

Wazanzibari wameitika kama walivyoitika, ''Shusha Tanga Pandisha Tanga Safari Iendelee.''

Kuna kitu nakiona kwa Juma Duni.
''Humility'' yaani unyofu.

Nuona unyofu wa hali ya juu sana na si kama nilikuwa siujui.

Hakuna makeke kwenye haiba yake wala kwenye maneno yatokayo kinywani mwake.

Siku zote nimsikilizapo Juma Duni Haji ujumbe wake ni In Shaa Allah Zanzibar itatulia na haki itasimama.

Hata mimi hili naamini bila ya chembe ya shaka kuwa Zanzibar itarejea kuwa njema na atakae kuingia visiwani atabisha hodi na mlango atafunguliwa kama ilivyokuwa zama.

Mara ya kwanza kukutana na Juma Duni Haji ilikuwa mwaka wa 1995 na alikuja naamini akitokea Uwanja wa Ndege moja kwa moja hadi Starlight Hotel ambapo mimi na wenzangu (sotowataja majina) tulikuwa chumbani kwa marehemu Maalim Seif tunafanya mazungumzo ya vipi tutaijenga CUF Tanzania Bara.

Juma Duni alikuwa anatokea masomoni Uingereza.

Juma Duni alikuwa amevaa suti ya rangi ya majivu iliyomkaa vyema.

Hii ndiyo siku ya kwanza nilipomfahamu Juma Duni.

Sote tuliokuwa ndani ya chumba kile tulikuwa vijana pamoja na kiongozi wetu Maalim Seif, sote tulikuwa vijana tunapendeza ukitutizama.

Nakuwekea hapo chini picha niliyompiga ‘’Babu,’’ kama wapenzi wake wanavyopenda kumwita umuone Babu Duni alivyokuwa kijana.

Picha hii nimempiga Juma Duni Korogwe wakati wa kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka wa 1995.

Pembeni ya Juma Duni yuko Prof. Ibrahim Lipumba na kuliani kwake ni Mzee Hassan Onari aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Tanga mjini.

Picha hii inanikumbusha mbali sana.

Tulitoka Korogwe tukafanya mkutano mwingine siku hiyo hiyo Muheza kituo cha mabasi na jioni tukaingia Tanga mjini kwa ajili ya mkutano mkubwa siku ya pili.

Naam.

Mkutano wa Tanga wenyeji wetu walitueleza kuwa haukupatapo kutokea hata wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika Nyerere na Bi. Titi Mohamed walipohutubia mkutano wa kwanza wa TANU kiwanja cha Tangamano mwaka wa 1955.

Juma Duni alipanda jukwaani kwanza kisha Prof. Lipumba akaja kuhitimisha.

CUF ilikuwa imepokelewa kwa kishindo kikubwa Tanga.

Toka asubuhi, ‘’mood’’ ya mkutano yaani hamasa ya mkutano ilianza kuonekana mfano wa mechi ya fainali katika ya African Sports na Coastal Union enzi zao.

Tanga usafiri mkubwa ni baiskeli na kila baiskeli ukiiangalia ilikuwa ina bendera ya Lipumba na mwendeshaji akipiga kengele hata bila sababu kuashiria kuwa leo kuna jambo kubwa.

Mitaa yote ya Ngamiani, Tanga Mjini ilishamiri picha za Prof. Lipumba pamoja na T Shirt zenye picha yake.

Mkutano ule uliinyongesha sana CCM Tanga.

Kuna picha mbili za Juma Duni naziweka hapo chini tukiwa Ngamiani nyumbani kwa marehemu Mama Ummy bint Anzuani aliyetualika kwake na kutufanyia dhifa kubwa sana.

Katika picha moja nipo.
Naamini haitakuwa tabu kunitambua.

Nje ya nyumba ya Mama Ummy walijaa wanachama wa CUF waliotusindikiza kwa maandamano kutoka Tangamano hadi Ngamiani.

Naweka ukurasa kutoka shajara (diary) yangu msomaji wangu usome uone hali ilivyokuwa Tanga siku ile sasa miaka 27 imepita.

Kila fursa niliyopata nilijitahidi kumueleza Juma Duni historia ya siasa za Tanganyika.

Juma Duni Haji leo ni kiongozi mkubwa Zanzibar na uongozi wake In Shaa Allah utatengeneza hali ya baadae ya nchi yake.

Kwa miaka mingi tumekuwa pamoja ingawa mimi niko Tanganyika na nimeshuhudia kila msukosuko uliomfika akiwa ubavuni kwa Maalim.

Juma Duni kafungwa na Komando na Komando akasema akae ndani yeye si papai kuwa ataoza.

Kama niliposema hapo awali historia ya Zanzibar imegubikwa na simanzi nyingi na inakuwa tabu kuieleza historia hii bila hata kwa mbali kugusia misiba hii.

Juma Duni amesema katika hotuba yake hii ya leo kuwa ni tegemeo lake kuwa Zanzibar itafanya uchaguzi wa wa 2025 kwa amani.

Hapo kwenye uchaguzi wa 2025 ndipo ulipo mtihani mkubwa kwa Wazanzibari na yeye Juma Duni.

Nilikuwa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa 1995 siku ya pili uvumi ulipozagaa kuwa CUF imeshinda uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.

Waingereza wana msemo, ''The rest is history,'' yaani kilichobakia ni historia.

Namtakia kila la kheri rafiki yangu Juma ‘’Babu,’’ Duni Haji.

Hakika miaka mingi imepita.

View attachment 2105446
Shukran mkuu.
Mungu ninayemuabudu akuongezee maisha marefu ikimpendeza ili niweke kujifunzia mengi toka kwako.
Inshallah
 
Alitoa takwimu za matokeo?...au ni madai tu?

..hakutoa takwimu lakini Babu Duni anadai taarifa hizo walipewa na mtu ambaye wanamuamini / anaaminika.

..lakini utakumbuka hata Lowassa alidai wamemuibia kura zake.

..Hakuna chombo ambacho ni independent kimejitokeza ku-disprove madai hayo.

..Binafsi nilipuuza madai ya Lowassa, lakini sasa nijikuna kichwa baada ya kumsikia Babu Duni akizungumzia kitu hichohicho.
 
..hakutoa takwimu lakini Babu Duni anadai taarifa hizo walipewa na mtu ambaye wanamuamini.
...Ni wanasiasa wachache sana wa huku Africa hukubali wameshindwa kihalali hasa uchaguzi unapokuwa na mchuano mkali.
 
..I agree with you.

..lakini umewahi kujiuliza ni chaguzi ngapi hapa Afrika zinafanyika bila dhuluma, manyanyaso, na wizi?

..kwa mfano, uchaguzi wetu wa 2020. CCM walikuwa na kila sababu na uwezo wa kushinda, sasa kilichowapelekea kufanya waliyofanya ni nini?

..hivi uchaguzi gani wa Kidemokrasia huwa mgombea mmoja anakuwa na mabango nchi nzima, na kutangazwa na vyombo vyote vya habari, huku wagombea wengine wakiwa gizani?

..Wakati mwingine huwa nashangaa iliwezekana vipi uchaguzi wa namna ile ukafanyika Tanzania.
 
Back
Top Bottom