Namkataa Paul Makonda, sijamtuma Bungeni

Namkataa Paul Makonda, sijamtuma Bungeni

Hayo matamshi ya Makonda is a blessing in disguise, kwani amesaidia kuitangaza JF kwenye BMK.

Huenda Mhe Sitta & Co. baada ya kauli hiyo ya Makonda watapitia hapa JF, ili wajue maoni ya watanzania kuhsu katiba mpya
 
eti anapiga kura kwa niaba ya vijana Wa jamiiforum halafu anawashutumu kupotosha juu ya uundwaji Wa time ya mashauriano.
 
nimemsikia akisema jamii folam na si hii ya kwetu jamii Forum
 
Safi sana Mh Paul Makonda umetuwakilisha vyema vijana wa JamiiForum!!

CCM ni kama Maji, usipoyanywa, utayaoga. CCM kila sehemu tupo.
 
Leo hii nimefurahi sana, Wana JF tumewakilishwa vyema kabisa...Na uzuri wengi humu ndani kura yetu ni NDIYO!!!
Kwa Katiba inayopendekezwa....Hakika tumpongeze huyu kijana.
 
Makonda kajituma mwenyewe halafu anasingizia mimi nimemtuma,CCM bila kusema uongo hawawezi
 
Kumbe chadema/bavicha mnafuatilia kwa makini BMK,,,Vip hamuandamani tena????
 
kwenye JF kama kweli yeye ni mwanachama aangalie kura inasemaje mpaka sasa katiba ya warioba inaongoza kwa asilimia 94 kura ya ndio ni asilimia 6 tu,
 
Jamani watu wanatafuta fursa, anaona watu wanaaeeka ndani ya ccm, hivyo lazima apambane wamuone kama walivyofanya kwa Nape.
 
Hayo matamshi ya Makonda is a blessing in disguise, kwani amesaidia kuitangaza JF kwenye BMK.

Huenda Mhe Sitta & Co. baada ya kauli hiyo ya Makonda watapitia hapa JF, ili wajue maoni ya watanzania kuhsu katiba mpya

Wanapita kila saa.
 
Nimemsikia anavyopiga kelele....Hivi huyo Makonda ni kijana wa jinsi ipi?
 
Ccm watambue wanachofanya ndio kujiandalia kifo, KANU did the same na waliumbuka kura ya maoni ndio ikawa safari yao, kuondoa tunu za taifa ni kwa malengo ya nani? Ili waendelee kuiba, leo madaraka ya rais analala akiamka anateua hata mkwewe kua mkuu wa mkoa huo ujinga mwisho. Mikataba yote iwe wazi, ijadiliwe bungeni na iweke maslah ya taifa na si ten percent
 
jana katibu hamasa wa vijana taifa alituwakilisha vyema sana kwa kusema amepiga kura kwaniaba ya vijana wote wa Tanzania
 
Back
Top Bottom