- Thread starter
- #21
ama kweli mmetuokota watanzania!!!
mbona miradi yote iko mkoa wa pwani anakotoka mumewe? sio ukanda huu??
au sio ufadhili unaofuata mkondo wa madaraka ya mumewe?
bila urais wa mumewe, WAMA itabaki kitu gani?
urais wa mkapa ulipoisha, EOTF ilibaki kitu gani?
wamekulipa kiasi gani kuja kuwavua magamba hapa JF?
Sijalipwa chochote na wala sio wa type hiyo kama nyinyi ambao mnalipwa na CDM ili hata pale mambo mazuri yanafanyika hamuoni , MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA. Nimejitokeza kusema ninayo yajua sio kwa Kuvua mtu gamba, hakuna mwenye magamba ndani ya WAMA, kwa uongo ukirudiwa mara kwa mara huwa ukweli .
Taasisi yoyote inapotaka kufanya uwekezaji lazima inafanya tathimini ya maeneo ya kufanya uwekezaji huo, na ndio maana kuna upembuzi yakinifu unafanyika na kwa kuzingatia vigezo vinavyotolewa na Wafadhili wa miradi hii. WAMA inaongozwa kwa taratibu hizo. kwa mazingira na vigezo hivyo Rufiji ikachaguliwa na sio kwa kuwa Mkoa anakotoka Mhe Rais kama hivyo ndivyo kwanini miradi isiwekezwe BAGAMOYO
Mlitaka miradi hiyo ipelekwe maeneo ambayo huduma hizo zipo ? Shule imejengwa Pwani sawa, lakini mbona wanaosoma pale ni watoto toka Mikoa yote Ishirini na Sita ya Tanzania na kwa makabila yote ? Kama anaefadhili ujenzi wa hiyo shule ameridhika inatosha ! Akija F/Lady mwengine atawekeza maeneo mengine baada ya miaka kadhaa Nchi yetu yote itakuwa imefikiwa Mdau .
Hoja hapa ilikuwa kutoa DATA za namna gani Mama Salma anachangia shughuli za jamii kupitia Taasisi ya WAMA na sio Taasisi ya Maulaji na HAKUNA UFISADI WOWOTE