Namfagilia mhe mama Salma Kikwete

Namfagilia mhe mama Salma Kikwete

Rais Salma, Rahma na Kikwete na walamba viatu wao

Kwa wanaojua urais barani Afrika ulivyo mtaji mkubwa kwa familia na waramba viatu wa kwenye kuwa nao, watakubaliana nasi kitu kimoja. Chunguza picha hiyo hapo juu ambapo Rais wa WAMA, Salma Kikwete yuko ziarani nchini Marekani.
Je Salma amekuwa rais lini zaidi ya baada ya mumewe kuwa rais? Kabla hapo rais wa kutumia NGO hakuwa mwingine bali Anna Mkapa ambaye alitimka baada ya mumewe kuutema ulaji.

Je rais Salma ameandamana na nani? Kwenye picha anaonekana Zakhia Meghji aliyekuwa waziri wa fedha wa mumewe kabla ya kuondolewa kwa kashfa mbali mbali za wizi wa mabilioni ya fedha za umma.

Anayefuata nani? Mwanaidi Maajar ambaye ni balozi wa mumewe nchini Marekani anayetuhumiwa kusaini nyaraka za baadhi ufisadi wa kutisha na mwisho wa yote kuzawadiwa ubalozi. Je aliteuliwa kuwa balozi kutokana na merit au kuwa karibu na bwana au bi mkubwa kama anavyooneka? Je ni wangapi wamo kwenye ofisi za umma kupitia mgongoni mwa ufisadi huu wa kunuka unaoendelea kuvumiliwa? Tuliwahi kuandika makala ya Hidden Presidents of Africa.

Wanaoikumbuka wanaweza kujua ni marais wangapi Afrika inao nyuma ya pazia. Wa mwisho mkumbuke Simone Gbagbo na alivyoisha kabla ya Suzana Mubarak na Leila Trebelsi wa Tunisia. Wakumbuke marais hawa waliopata urais kutokana na kulala kitanda kimoja na rais wako wakati ukiangalia picha ya rais huyo wa WAMA.

Bado rais Rahma al Kharoos Kasiga wa RBP Group ambayo imeota baada ya Kikwete kuingia madarakani.
 
hongera mama salma usife moyo na maneno ya baadhi ya watu

Jitahidi mama maana sasa naanza kupata picha kuwa kwanini siku hizi umaarufu wako unashuka kiwango. Jitahidi maana wanawake wengi walihusika sana kuwaokoa waume zao ambao wamepotoka! Kaza mwendo maana mama mweye hekima huijenga nyumba yake mwenyewe! Taadhari na Swali pia kwa wana Jf ni kwamba watu hao waliotajwa walipat nafasi hizo kwa upendeleo au ni kwa kuangalia qualification zao? Tusijejikuta tunashabikia kitu ambacho hakitakiwi kupongezwa!
 
Ripoti hazina shida zitawekwa hapa jamvini, ila pia sio mbaya ukiwa mtanzania ukatembelea WAMA ambapo pia utapewa copy ya hizo ripoti . Lakini ripoti peke yake hazisaidii kama Mtanzania mwenye mapenzi ya dhati basi tembelea kwenye miradi mikubwa ya WAMA kama ifuatavyo

1. Kijijini Nyamisati njia panda ya Bungu wilayani Rufiji -kuna shule ya vipaji maalum ya wasichani ni uwekezaji wa 1.9 Billion, utakuta Mkandarasi na mshauri kazi inaendelea. Utakuta wanafunzi 172 yatima na wanaotoka familia duni watakupa ushuhuda

2.Kijiji cha Hoyoyo Mkuranga ujenzi wa Kituo cha Afya unaogharimu milioni 145, ujenzi unaendelea na utamkuta Mkandarasi yupo site anakamilisha kazi.

3.Nyamisati ujenzi wa shule ya kata ya salale ambapo kulikuwa hakuna sekondari na kata hii imezungukwa na visiwa ujenzi huu umegharimu Milioni Hamsini,kwa sasa zaidi ya wanafunzi 400 wapo hapo wanasoma.

Safari hii unaweza kuifanya kwa siku moja kwenda na kurudi ili ujiridhishe na thamani ya fedha yaani Value for Money !

Umesemaje tena! Mbona hiyo taarifa yako inataka kunifanya nione udhaifu wake tena kutokana na sehemu ulizozitaja. Nilitegemea utaje sehemu ambazo hazitanipa mashaka! Ila anajua anachofanya yeye. Mambo ya kujilimbikizia mali umeyajuaje wewe? Nani kakuuliza? Ungesubiri lakini uulizwe kwenza, maana maana ajibuye kabla ya kuulizwa na ajiteteaye kabla ya kutuhumiwa huwa tuna wasiwasi naye! Utasemaje hujaiba kabla hujatuhumiwa?
 
duh .. kumbe Salma ni mhe.? Nielimisheni .. kwa k(v)igezo gani?

Bwana eee z hukusikia Musoma alisomewa ripoti ya mkoa na mkuu wa mkoa? Huoni msafara wake? Nchi iko Loliondo hii inapatiwa kikombe
 
uwakumbushe. Tunapoongelea WAMA hatumaanishi hawa wafanyakazi wadogo wanaochapa kazi ili kupata mkate wao. Tunamaanisha mapapa wake za wakubwa au wakubwa wenyewe hapa chini:

Mama. Salma Kikwete Chairaperson mke wa rais Jakaya Kikwete
Mama. Sophia Simba Chairperson of the Board waziri katika utawala wa Kikwete
Mama. Zakia Zamdan Meghji Board Member waziri wa zamani wa fedha aliyeondolewa kwa ufisadi
Amb. Mwanaidi Majaar Sinare Board Member balozi wa serikali ya Kikwete nchini Marekani anayedaiwa kusaini mikataba mingi ya kifisadi na asikanushe
Mama. Regina Lowassa Board Member mke wa waziri mkuu wa zamani aliyetimuliwa kwa ufisadi
Mama. Blandina Nyoni Board Member
Mama Hulda S. Kibacha Board Member
Kama kweli nia ya WAMA ni njema na si kutafuta kuchuma kwa kutumia matatizo ya akina mama, kwanini kwenye bodi ambayo ndiyo roho ya WAMA hakuna wanawake wa mashambani ambao ndiyo walengwa na waathirika? Bila kutoa jibu linaloingia akilini kuhusiana na NGO hii ya mke wa rais na mashoga zake bado umma utaendelea kuamini ni ya kiulaji kama ilivyokuwa EOTF ya Anna Mkapa.Mbona siku hizi imedoda? Simple. Mkapa si rais tena. Naandaa makala iitwayo WAMA ni wizara ya mambo yote. Je wizara husika zitafanya kazi gani? WAMA bado itaendelea kuwa kitendawili cha utawala wa kujuana na kuibiana hadi itakapotokomea baada ya Kikwete kuondoka madarakani hapa 2015. Tusiruhusu rais ajaye kuwa na NGO ya mkewe. Ni ufisadi wa kimfumo huu.:kev::kev::kev::kev::kev::kev::kev:

Haya sasa! Ukujua hili wenzio wanajua lile, endelea kutujuza،
 
DUA la kuku Halimpati Mwewe , WAMA itaendelea hata Rais Kikwete atakapoondoka madarakani. Ni Taasisi inayoendeshwa kisomi ina mpango mkakati wake Strategic Plan ya miaka mitano mitano ( 2010-2015) ,inatumia MTEF kupanga mipango yake , inafanya SWOT analysis kila wakati . Hata EOTF inaendesha shughuli zake kama kawaida nenda kaitembelee Chang'ombe ipo imejaa tele.

Kuhusu wajumbe wa Bodi hapo juu, nashauri rudi darasani hususan fanya mapitio ya somo la Governance/ Organisation Development ukichukua MBA option yoyote utapitia hilo somo halafu jiridhishe na topic /sub topic inayohusu Roles za Board of Directors halafu utapata jibu la kwanini wameteuliwa watu wa kaliba tofauti wao sio watendaji Ufisadi huo wataufanyaje . Mmeshaona hoja yenu ya Mhe Mama Salma kwenye Taasisi yake ameweka ndugu zake ,n mkabila na mdini haina mshiko !

Na kwataarifa yenu Wajumbe hao wa Board wanafanya kwa kujitolea tu hawana hata Ada yoyote wanayolipwa hata sitting allowance hawalipwi kamwe . Waacheni wafanye kazi yao .HAKUNA UFISADI WAMA NA KAMWE HAUTATOKEA

Naanza sasa kujua kuwa unalipwa na umetumwa! Unavyozidi kuendelea kujibizana unaanza kujifunua mwenyewe!
 
Wabongo bana, yaani umahiri wa huyu mama na mumewe wa kuomba omba and yet someone want us to cheer the trend?
 
Mkufu sina hakika km shanga ni nduguyo ama ni jamaa tu kwa kua wote mnavaliwa!...
Nikupongeze kwa post yako nzuri sana!...nadhani bi mkubwa akiona ataku PM na sitashangaa keshokutwa ukapewa kakitengo...
lakini hebu tumia akili kidogo kutafakari...bila hata kusema neno!
-Kwamba ni nani huyu mama?
-Ni nguvu gani ipo nyuma ya hayo yote anayokukosha nayo?
-Kwanini hudhani hiyo nguvu ndiyo spark yake na isingekuepo huenda angekua km mama fulani wa Makokola Tabora?

Nimefurahishwa sana na kibwagizo chako cha mheshimiwa mama fulani...kesho andaa ya mheshimiwa mtoto wa baba na keshokutwa usisite kutuletea ya mheshimiwa mshauri wa baba kwenye mambo ya utawala kwa kua Tanzania yetu imepiga hatua kubwa sana na soon tutaanza kuwakopesha wenzetu wa ulaya ili kuinua hali zao za maisha!
Salaam!
 
Mkufu jaribu kuwa great thinker na sio cheap thinker. WAMA inafanya vizuri that is good and thank you 4 the gud newz. Swali linakuja je ni nani yupo responsible for th success behind WAMA? Hapa ndio umeshindwa kutudhihirishia, inawezekana ni management team ya WAMA na wala sio hao board of directors coz wengi wao hapo wamewekwa tu kama ceremonial leaders na hata hawana mchango mkubwa hapo WAMA kama hao management wanaoplan na kujua what do every day. Kwahiyo suala la wewe kuchukua mafanikio ya WAMA na kuyahusisha moja kwa moja na mama salma kikwete ndio linalotupa shaka na nia yako. Au umetumwa...?
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Mpigie simu mpe hongera, sio lazima kujaza kurasa hapa!
 
Mdau naamaanisha muda wa kukaa madarakani mumewe Mhe Rais utakapoisha na yeye U F/Lady nao unaisha

Mkufu, muda ya kukaa madarakani Rais kamwe haumpi mkewe madaraka. Madaraka yanatokana na sheria na au Katiba, sijaona mahali popote kwenye katiba ambamo mke wa Rais anapewa madaraka yoyote. Ukweli ni kwamba kisheria na kikatiba mke wa Rais hana madaraka yoyote.
 
Happy Easter nawe Mdau hakuna swali ambalo sikulijibu. Upeo wangu mi mkubwa sana kuliko unavyofikiri !

kwa kiakirishi (indicator) gani umeconclude kua upeo wako ni mkubwa?!?!
mtu mwenye upeo mkubwa anajulikana kwa kutathminiwa na watu, nasi kujitathmini mwenyewe..
sasa kama watu wamekutathmini na kukuona una upeo mdogo..hivyo ndivyo ulivyo
 
mie yule mama natamani nionane naye,hivi anapendelea mitaa ipi vile,naona siku hizi ana mwenzake mpya
 
Hivi Salma Kikwete uheshimiwa ameutoa wapi, yeye ni nani kwa watz, alichaguliwa na nani kupata uheshimiwa? We umetumwa nini? Mijadala inayomuhusu huyu mama bora ikasitishwa maana inawagadhabisha wengi na kusababisha familia nzima ya ****** kuchukiwa. Kama hauna la kuongea kaa kimya.
 
uwakumbushe. Tunapoongelea WAMA hatumaanishi hawa wafanyakazi wadogo wanaochapa kazi ili kupata mkate wao. Tunamaanisha mapapa wake za wakubwa au wakubwa wenyewe hapa chini:

Mama. Salma Kikwete Chairaperson mke wa rais Jakaya Kikwete
Mama. Sophia Simba Chairperson of the Board waziri katika utawala wa Kikwete
Mama. Zakia Zamdan Meghji Board Member waziri wa zamani wa fedha aliyeondolewa kwa ufisadi
Amb. Mwanaidi Majaar Sinare Board Member balozi wa serikali ya Kikwete nchini Marekani anayedaiwa kusaini mikataba mingi ya kifisadi na asikanushe
Mama. Regina Lowassa Board Member mke wa waziri mkuu wa zamani aliyetimuliwa kwa ufisadi
Mama. Blandina Nyoni Board Member
Mama Hulda S. Kibacha Board Member
Kama kweli nia ya WAMA ni njema na si kutafuta kuchuma kwa kutumia matatizo ya akina mama, kwanini kwenye bodi ambayo ndiyo roho ya WAMA hakuna wanawake wa mashambani ambao ndiyo walengwa na waathirika? Bila kutoa jibu linaloingia akilini kuhusiana na NGO hii ya mke wa rais na mashoga zake bado umma utaendelea kuamini ni ya kiulaji kama ilivyokuwa EOTF ya Anna Mkapa.Mbona siku hizi imedoda? Simple. Mkapa si rais tena. Naandaa makala iitwayo WAMA ni wizara ya mambo yote. Je wizara husika zitafanya kazi gani? WAMA bado itaendelea kuwa kitendawili cha utawala wa kujuana na kuibiana hadi itakapotokomea baada ya Kikwete kuondoka madarakani hapa 2015. Tusiruhusu rais ajaye kuwa na NGO ya mkewe. Ni ufisadi wa kimfumo huu.:kev::kev::kev::kev::kev::kev::kev:

....Dah! Mkuu, Tafadhali chukua TANO! Ina maana huyu mpiga debe alipokuwa akitaja wale 'Kaj*mba nani' wenzetu kwenye post yake ya nyuma, haya majina ya hawa magogo alikuwa ameyasahau???
 
Hivi Salma Kikwete uheshimiwa ameutoa wapi, yeye ni nani kwa watz, alichaguliwa na nani kupata uheshimiwa? We umetumwa nini? Mijadala inayomuhusu huyu mama bora ikasitishwa maana inawagadhabisha wengi na kusababisha familia nzima ya ****** kuchukiwa. Kama hauna la kuongea kaa kimya.

Mhe Mama Salma Kikwete ni Mama wa Taifa hili (FIRST LADY ), alichaguliwa na Mhe Rais Jakaya Kikwete aliechaguliwa na Watanzania kuwa Rais wao .Wala sijatumwa na mtu yoyote, Mijadala haitasitishwa kwani mnaochukia mna wivu wa kijinga ! Familia haichuki , sema unaichukia kwa kuwa Mhe mama Salma Kikwete kwa jitihada zake Taasisi anayoiongoza imejenga shule inayosomesha watoto yatima na mazingira magumu tanzania nzima . Unachukia kwa vile mhe mama Salma anasomesha watoto wengine kila mkoa kumi walio yatima waliopo mikoa yote na wengine mwaka huu wanajiunga na kidato cha Tano. Bila ya WAMA na jitahada za Mama Salma watoto hao wangekosa fursa. Unachukia kwa vile Mhe Mama Salma amesaidia kupata mfadhili wa kuisaidia MEWATA mchakato wa ujenzi wa Hospital ya kina mama itakayoshughulikia saratani za Akina Mama hutaki kina mama wapate huduma . CHUKI YAKO KAMWE MWENYEZI MUNGU HATAIPOKEA MAMA SALMA ATAENDELEA VIZURI PAMOJA NA WAMA KWANI HAO WALIOFAIDIKA NA WANAOENDELEA KUFAIDIKA NA JITIHADA ZAKE HASA WATOTO YATIMA WANAKESHA KUMUOMBEA POLE SANA , KUNYWA CHUPA UTANGULIE! ILI YASIKUKERE MAFANIKIO YA MHE MAMA SALMA F/LADY WA UKWELI !
 
Jitahidi kuwaelesha hawa jamaa mkuu, you have been paid for that!!
 
Back
Top Bottom