Namfagilia mhe mama Salma Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namfagilia mhe mama Salma Kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkufu, Apr 24, 2011.

 1. M

  Mkufu Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wana jf salaam,

  leo najitokeza rasmi kumfagilia kwa sana f/lady wa tanzania mhe mama salma kikwete kwa utendaji wake wa kazi tangu ameingia madarakani mumewe mhe rais jakaya mrisho kikwete .

  Wana jf nimekuwa nikosoma mara hapa jamvini. Kadhaa mada mbalimbali juu ya huyu mama nyingi zikionyesha kumshambulia pengine kwa kutojua kazi alizozifanya mpaka sasa. Pia baadhi ya magazeti hasa mwanahalisi na raia mwema zimekuwa zikiandika makala yenye mtizamo hasi juu ya f/lady na taasisi ya wama . Mwandishi mmoja nkwazi anaeishi kanada ktk makala zake nyingi juu ya f/l na wama ameonyesha waziwazi chuki binafsi juu ya wama na f/l

  wana jf taasisi ya wama inafanya kazi kubwa ya kusaidia makundi maalum ya kijamii husasani wanawake na watoto wa kike walio katika mazingira hatarishi yaani yatima na familia duni kwa kuwapatia elimu itakayoweza kuwakuomboa .

  Taasisi ya wama inayo bodi ya wakurugezi, timu ya menejimenti iliyopatikana kwa njia ya usaili wenye ushindani . Na katika timu ile mama salma hana ndugu hata mmoja aliemweka . Kuna wakati alituhumiwa kwa ukabila na udini katika taasisi yake ufuatao ni ukweli wa timu ya menejimenti ya wama ;

  1. Daudi nasib- katibu mtendaji mpare muilslam
  2. Neema mhada-afisa afya msukuma - mkiristo
  3 gloria minja - afisa tathimini -mchaga-mkiristo
  4 philomena marijani -afisa uraghibishi-mpare-mkiristo
  5 john mataka -afisa elimu ya mtoto wa kike-mmakonde-mkiristo
  6 tabu likoko- afisa uwezeshaji wanawake-mzigua -muislam
  7 christina ngonyani(cpa)- mhasibu -mngoni -mkristo
  8 subira mgalu(cpa) -mhasibu -mzaramo-muislam
  9. Anande munuo -secretary f/l-mchaga-mkristo
  10. Veronica -ngulupa -mhudumu-mnyasa-mkiristo

  haya hoja ya ukabila na ukiristo ina mshiko ? Watanzania tumuogope molla wetu

  hoja nyingine kwamba wama inapata fedha toka ikulu hii sio kweli tangu wama ianzishwe haijawahi kuchangiwa pesa yoyote toka ikulu wala mfuko mkuu wa hazina . Vyanzo vya mapato ni kutoka kwa wasamalia wema wenye kuguswa na shughuli zinazofanywa na f/l kupitia taasisi yake ya wama . Fedha zote zinazochangwa zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa .

  Kila mwaka taarifa hesabu za taasisi zinaandaliwa kwa viwango vya kimataifa na kuwasilishwa kwa mkaguzi wa nje kampuni ya kimataifa pkf iliyopo jengo la amani house floor ya tisa na zinapewa hati . Miaka mitatu mfululizo wama imepata hati safi .

  Mafanikio ya wama inayoongozwa na mhe mama salma kikwete ni mengi sana na yameelezwa katika ripoti ya mwaka ya taasisi hasa 2006/2007 , 2007/2008 , 2008/2009.

  Lakini jambo kubwa ni kwa mama salma kikwete kujenga shule ya kisasa ya mfano wa kuigwa wilayani rufiji mkoa wa pwani kwa mchango wa mfadhili hayao nakayama wa japan na wadau wa ndani ya nchi .shule hii mpaka sasa imegharimu zaidi ya billion 1.9 za kitanzania na inasomesha bure watoto yatima na wanaotoka kwenye familia duni toka mikoa yote ya tanzania bara na visiwani. Shule hii ina wanafunzi mpaka kidatio cha pili wapatao 272 na kati ya hao hakuna hata ndugu mmoja wa mama salma au mjumbe yoyote wa bodi au ndugu wa mfanyakazi wa wama

  watoto hawa wanachaghuliwa na wizara ya tamisemi bila ya kujali dini,kabila , itikadi za wazazi wao,rangi n.k . Tunaomba wadau waendelee kumuunga mkono mhe mama salma kikwete kwa moyo wake huu wa kizalendo .kupitia shule hiyo taifa la tanzania litapata wataalamu wa kutosha katika maeneo mbalimbali . Shime wananchi/wadau/wahisani tuache kusikiliza maneneo ya mitaani , mhe mama salma ni mfano wa kluigwa .

  Nawasilisha wada
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mungu amzidishie nguvu kwa haya anayoyafanya, kwani kila mtenda wema si lazima alipwe jema, watu humu JF hata kama ni ya wema kama afanyayo huyu mama , wao huona ni mabaya tu
   
 3. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mwache achape kazi!
  Lakini huu utaratibu wa tz kutegemea NGO badala ya kuwa na taasisi na serikali responsible utaisha lini?
  Nimemsikia Prime Minister anaomba ardhi Arusha naye anataka kuanzisha taasisi ya kansa na masuala ya albino. Kwa mwendo huu zile taasisi za serikali zitatoa huduma iliyotukuka kweli!
  Ninawaza kwa sauti iliyokuu! Ukitilia maanani shule za sirikali sasa zimetelekezwa na zile za St ....... zinachana mbuga kwa kuwahudumia watoto wa familia bora ili hali watoto wa bora famili wakichota ujinga wa kumwaga kutoka St government primary and sec school.
  Anyway, huenda ndo falsafa mpya ya afrika na hasa hasa tz.
   
 4. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  hongera mama salma usife moyo na maneno ya baadhi ya watu
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Vibaraka mna kazi kweli...hivi si mna gazeti lenu la uhuru au wavuti ya wama ndo muende mkaandike haya mautumbo yenu huko...mbona mnahangaika sana
   
 6. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mkufu usemayo ni sahihi lakini lengo walilonalo wasemaji a.k.a wapayukaji...a.k.a over intelligence wa hapa jf sio kukosoa serikali ili irekebishe pale penye mapungufu bali ni kukosoa kila kitakachofanyika kwenye serikali hii iliyopo madarakani na ukitaka kuwa member mpendwa basi shiriki kikamilifu katika ukosoaji hata kwa jema tafuta kasoro otherwise jiandae kujiongezea idadi ya maadui!
   
 7. wa UDOM

  wa UDOM Member

  #7
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ******!
   
 8. wa UDOM

  wa UDOM Member

  #8
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ******
   
 9. M

  Mkufu Member

  #9
  Apr 24, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nilijua baadhi ya Vibaraka mtakosa la kujibu. Kwa kuwa mnatumia jf hii nami nimeamua kutoa Data kupitia jamvi hilihili, TUTABANANA HAPA HAPA ! Na kwa taarifa yenu Mama Salma yupo makini hana tuhuma za kujilimbikizia mali ! resources zote za WAMA hahusiki nazo kabisa , kuna menejimenti iliyoenda shule na ikabobea ndio inaratibu shughuli zote .

  Huo ni wivu tu unaokusumbua . Muda wake wa kukaa madarakani utakwisha lakini ataacha LEGACY na atakumbukwa na mamia ya watoto wa kike yatima na mazingira duni watakaokuwa wamefanikiwa kupitia mkono wake

  Hakuna ukibaraka, penye ukweli lazima tuseme kwa bahati nzuri ni watu wachache wanaomchukia mama salma ukiwemo wewe , mama salma mungu anampenda zaidi idumu Taasisi ya WAMA

  Wadau tunaikubali.Wenye wivu wajinyonge! Wamoja Havai Mbili !
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mkufu, tunaomba utuwekee hizo ripoti zake ya mwaka
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  la kujiuliza:

  1. kabla mumewe hajawa rais wa JMT alikuwa na mchango gani na alionyesha umahiri gani wa utendaji?

  2. kwanini huo "umahiri wake wa utendaji" ulisubiri mumewe apate urais wa JMT?

  akili za mbayuwayu.... changanya na zako!!
   
 12. M

  Mkufu Member

  #12
  Apr 24, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ripoti hazina shida zitawekwa hapa jamvini, ila pia sio mbaya ukiwa mtanzania ukatembelea WAMA ambapo pia utapewa copy ya hizo ripoti . Lakini ripoti peke yake hazisaidii kama Mtanzania mwenye mapenzi ya dhati basi tembelea kwenye miradi mikubwa ya WAMA kama ifuatavyo

  1. Kijijini Nyamisati njia panda ya Bungu wilayani Rufiji -kuna shule ya vipaji maalum ya wasichani ni uwekezaji wa 1.9 Billion, utakuta Mkandarasi na mshauri kazi inaendelea. Utakuta wanafunzi 172 yatima na wanaotoka familia duni watakupa ushuhuda

  2.Kijiji cha Hoyoyo Mkuranga ujenzi wa Kituo cha Afya unaogharimu milioni 145, ujenzi unaendelea na utamkuta Mkandarasi yupo site anakamilisha kazi.

  3.Nyamisati ujenzi wa shule ya kata ya salale ambapo kulikuwa hakuna sekondari na kata hii imezungukwa na visiwa ujenzi huu umegharimu Milioni Hamsini,kwa sasa zaidi ya wanafunzi 400 wapo hapo wanasoma.

  Safari hii unaweza kuifanya kwa siku moja kwenda na kurudi ili ujiridhishe na thamani ya fedha yaani Value for Money !
   
 13. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135

  ama kweli mmetuokota watanzania!!!

  mbona miradi yote iko mkoa wa pwani anakotoka mumewe? sio ukanda huu??

  au sio ufadhili unaofuata mkondo wa madaraka ya mumewe?

  bila urais wa mumewe, WAMA itabaki kitu gani?

  urais wa mkapa ulipoisha, EOTF ilibaki kitu gani?

  wamekulipa kiasi gani kuja kuwavua magamba hapa JF?
   
 14. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  duh .. kumbe Salma ni mhe.? Nielimisheni .. kwa k(v)igezo gani?
   
 15. M

  Mkufu Member

  #15
  Apr 24, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Kabla mumewe hajawa Rais alitumia kipaji chake kwa kufundisha kwa miaka 17, na ndio maana mumewe alipoingia madarakani aliendelea kutumia kipaji hicho kuwekeza katika Elimu ya Mtoto wa Kike kwa kuwaomba Wasamaria wema kuchangia uwekezaji huo. Wadau hao hawaladhimishwa, lakini Wamesalute kwa ushupavu wa F/Lady na uthubutu wake.Wajapan wametembelea miradi hiyo na wameahidi kuzidi kuichangia WAMA, WAMA inapaa katika Anga za Kitaifa .Hata kwenye mikutano ya kimataifa Mama Salma yupo JUU, Taasisi za Mataifa mbalimbali yana appreciate kazi za WAMA kimsingi Ipo juu najua baadhi ya Wana JF mnakerekwa sana na hili tuvumiliane ila Penye Ukweli Uwongo Hujitenga !
   
 16. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mama Salma poa sana, mi nampenda sana, ni mchapa kazi.
  Serikali iunde taasisi za kusimamia mambo yote ili zi chape kazi harakaharaka kwani mawazi ni wawakilishi tu kwenye cabinet.
   
 17. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  1. kungekuwa na dhambi gani kama angeendelea kufundisha hata baada ya mumewe kuwa rais?

  2. je kazi pekee inayomfaa FL wa nchi kama yetu ni "kuongoza" NGO tu? tena yenye ofisi zake ikulu (au karibu na ikulu)?
   
 18. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  uwakumbushe. Tunapoongelea WAMA hatumaanishi hawa wafanyakazi wadogo wanaochapa kazi ili kupata mkate wao. Tunamaanisha mapapa wake za wakubwa au wakubwa wenyewe hapa chini:

  Mama. Salma Kikwete Chairaperson mke wa rais Jakaya Kikwete
  Mama. Sophia Simba Chairperson of the Board waziri katika utawala wa Kikwete
  Mama. Zakia Zamdan Meghji Board Member waziri wa zamani wa fedha aliyeondolewa kwa ufisadi
  Amb. Mwanaidi Majaar Sinare Board Member balozi wa serikali ya Kikwete nchini Marekani anayedaiwa kusaini mikataba mingi ya kifisadi na asikanushe
  Mama. Regina Lowassa Board Member mke wa waziri mkuu wa zamani aliyetimuliwa kwa ufisadi
  Mama. Blandina Nyoni Board Member
  Mama Hulda S. Kibacha Board Member
  Kama kweli nia ya WAMA ni njema na si kutafuta kuchuma kwa kutumia matatizo ya akina mama, kwanini kwenye bodi ambayo ndiyo roho ya WAMA hakuna wanawake wa mashambani ambao ndiyo walengwa na waathirika? Bila kutoa jibu linaloingia akilini kuhusiana na NGO hii ya mke wa rais na mashoga zake bado umma utaendelea kuamini ni ya kiulaji kama ilivyokuwa EOTF ya Anna Mkapa.Mbona siku hizi imedoda? Simple. Mkapa si rais tena. Naandaa makala iitwayo WAMA ni wizara ya mambo yote. Je wizara husika zitafanya kazi gani? WAMA bado itaendelea kuwa kitendawili cha utawala wa kujuana na kuibiana hadi itakapotokomea baada ya Kikwete kuondoka madarakani hapa 2015. Tusiruhusu rais ajaye kuwa na NGO ya mkewe. Ni ufisadi wa kimfumo huu.:kev::kev::kev::kev::kev::kev::kev:
   
 19. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280
  asante mkuu... watu wanafikiri Jf ni global publishers ambapo unaweza kuandika upuuzi kwenye magazeti ya risasi na ijumaa
   
 20. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280

  huu upuuzi ungepeleka kwenye magazeti ya uhuru, mzalendo au global publishers wangekuelewa sio humu
   
Loading...