Mimi pia nliwahi pitia hilo ila rahisi sana ,tena dogo,fanya hivi :
1. Kama wewe si mcha mungu(Pagan)
Nenda sumbawanga au kigoma vijijini katafute mganga ,mwambie hilo tatizo kuna dawa atakupa ya kunywa mvizie amelewa mnyweshe kinguvu ,baada ya hapo hata akipita mbele ya bia iliyofunguliwa atatapika
Madhara yake
Kisayansi dawa hii huwa kali inaweza unguza ini akafa hivyo dozi izingatiwe sana isizidi,pili mama yetu atapitia mateso ikiwemo ndoto mbaya kutetemeka kutokana na madhara ya kuacha pombe ghafla (withdrawal effects) ,hapo inabidi mumuone daktari kuna vidonge vina punguza mateso hayo takriban mwezi
2.Kama ni mkristo
Tafuta nyumba za maombi ,mfano Arusha pale safina redio ,vizia akirudi amelewa ile nguo atayoitoa iibe,kisha uwe unaenda nayo kwenye maombi siku kumi ,hakikisha umefunga siku hizo ,tendo hili litagusa huruma ya mungu na baada ya siku kumi toa sadaka walau ya laki madhabahuni kama sadaka ya shukrani ,kisha fungua nakupa muda kidogo tu amepona na atakuwa mwema atawafuta machozi yenu yote .
Madhara yake
Kisayansi ni yaleyale mumhusishe daktari kupunguza mateso ya kujitoa kwenye pombe,pia iwapo ikatokea akaasi akarudi ,biblia inasema huwa anakuwa mbaya kuliko mwanzo ,maana mapepo hurudi kwa idadi ya mara saba
3.Kama muislamu
Nenda kwa masheikh wasoma dua Zanzibar tembelea kama watano ,hii alipigwa mzee yusuph mpaka leo na muziki wa dunia akauacha,hii pia huwa inamrtesa mwezi wa kwanza mjitahidi kuwa nae karibu kumtoa out ,kumwonesha upendo
NB: NIKO TAYARI KUKUPA USHAURI WOWOTE KUMTOA MAMA YETU HUKO TENA BURE .