Mikembo Samike
Member
- Oct 4, 2018
- 13
- 12
Wakuu habari zenu,
Inawezekana hili ni jambo ambalo linaonekana kama ni gumu sana, lakini nisiwe mnafiki, maisha yangu yote sijawahi kuuonja upendo wa mama.
Nyumbani tuko wa tano, mimi ni wa nne, na kaka zangu wote wameshaoa. Nyumbani niko mimi na mdogo wangu wa kike.
Mama yetu ni mlevi wa kupindukia, analewa siku nzima, mara nyingine analala kwenye vilabu vya pombe watu wanamuokota wanamrudisha nyumbani, au wakati mwingine analala nje mpaka asubuhi.
Hapa mtaani wameshamjua kwa tabia zake mbovu na matendo mengi sana ya aibu anayoyafanya, mpaka kufikia wakati anakuwa na mahusiano ya kimapenzi na watoto wadogo wa kuwazaa kabisa. Ameshafumaniwa kwenye majumba ya watu akifanya mapenzi na walevi wanaomuokota vilabuni akiwa amelewa na kwenda kumfanyia mambo mabaya.
Baba yetu alishafariki tangu mwaka 2013 kwa maradhi ya kisukari, jambo lililofanya mama yetu kupata mwanya wa kufanya mambo ya ajabu, ya ajabu, ya ajabu na ya kutisha!
Kipindi baba yetu yuko hai, alikuwa anagombana vibaya sana na mama kwasababu ya ulevi wa mama na mambo yake ya kushindwa kulea familia mpaka ikafika kipindi baba akahama nyumbani akaenda kupata mwanamke mwingine!
Baada ya kifo cha baba yetu, tulipata mirathi ambayo inaingia kwenye akaunti ya mama yetu kwa awamu kila mwezi.
Fedha hizi za mirathi ndizo anazotumia kufanya ulevi na umalaya wa kutisha na walevi wenzake.
Kila mara anarudi nyumbani amepigwa, amechaniwa nguo na kudhalilishwa na hao waume zake wasiojulikana.
Kiufupi mama yetu amegeuka dampo la kila mlevi kumfanyia uchafu.
Tumeshamkanya na kumuweka vikao vya familia zaidi ya mara mia moja lakini hasikii lolote.
Mimi ni mwanachuo, na nilipopata likizo nikasema ngoja niende nyumbani nikawasalimu kidogo. Lakini matokeo yake nimekutana na mambo ya kutisha na kuniumiza sana moyo wangu.
Imefika wakati mpaka napatwa na ghadhabu na kuanza kurudishiana nae maneno makali. Matokeo yake ananitukana sana na kunilaani.
Namchukia sana mama yangu!