Namchukia sana mama yangu mzazi

Namchukia sana mama yangu mzazi

Unazungumzia vitu sijavizungumzia, Chuo imetoka wapi? kiherehere kimeingiaje hapa? jenga Hoja kama mtu mwenye Akili!
Wewe toa hoja elekezea kwa mwanzisha mada juu huko, hapa katikati unajichomekea kujibu watu wewe nani??? acha kukurupuka, comments yangu ya mwanzo sijaweka matusi mle sasa ww inakuhusu nini???
Ukitaka majibizano anzisha thread yako tujibizane huko ama jibizana pm acha utoto wa kutoka nao chuo!!!...saizi sijibu tena
 
Pole sana mdogo wangu,kiukweli inasisikitisha sana mzazi kuwa na tabia izo za kudhalilisha,jaribu kufuata ushaur mzur walio toa wenzangu hapa.. Mungu akuhurumie ilo jambo lipite na pia akupe uvumilivu
 
Pole mkuu, leo nageuka msomaji comments nimejikuta nimeumia sana, wadau jitahidini comments za kumtia moyo na kutatua tatizo si za kukebehi na kukejeli.
 
huenda na Tigo wamekula aiseeh!
lakini nikutie moyo tu! ichukie tabia yake lakini usimchukie yeye!
wakati mwingine ubongo ukivurugwa binadam hufanya mambo ya ajabu!! Tafta mbinu nyingine ya kuitokomeza hiyo tabia;
huenda ana pepo kivuruge huyo!
Na huyo akiacha pombe atakufa! maana pombe ishakuwa addiction na misuli ya damu, mfanyieni sobbing na maombi
Hivi kuna umuhimu wa kuonyesha wewe ni mjinga na mpumbavu kiasi hiki?
 
That is devil's spirit,anatakiwa kuombewa ukipata nafasi siku mama yupo sawa mpeleke kanisani akaombewe itamsaidia mno
 
Nimehuzunika sana pole sana Mkuu nendeni na mama sehemu za maombi yatapita tuu usimchukie mama Dunia ina mambo mengi anaweza kufanya vitu hivyo sio kwa ufahamu wake ila maombi naamini yatasaidia...
 
Pole sana.
Usimchukie mama yako bali mchukie shetani anayemtumia kufanya huo uchafu. Tafuta msaada wa kiroho ili afunguliwe.
 
Counselling inahitajika hapo
Mama ni mama tu msaidie sana na chukua mda wako wote kwake
Maisha ni mafupi acha yote na mshughulikie kikamilifu kwani anahitaji msaada wa hali ya juu

Pole sana
Kumbuka ya kuwa unaumia kila siku na umeathirika kisaikolojia sana.

Mpeleke kwa hospital aweze kusaidiwa kwani hasira hazimsaidii kabisa
Du numeumia sana
 
Mkuu IQ zetu zipo - 10 mwenye akili ndio ana 0 wakati wenzetu wengi ni + 70 kuendelea sasa utaendelea kujibishana na - IQ unapoteza muda...
Ni kweli kabisa. Kama walivysema wahenga wetu ''akili ni nywele, kila mtu ana zake''. Nashangaa mtu anajaribu kuandika uchafu kama huu kwenye matatizo kama haya. Hata kama amelewa gongo na anatumia ID isiyomtambulisha lakini jamaa ni hopeless kabisa.
 
Wakuu habari zenu,

Inawezekana hili ni jambo ambalo linaonekana kama ni gumu sana, lakini nisiwe mnafiki, maisha yangu yote sijawahi kuuonja upendo wa mama.

Nyumbani tuko wa tano, mimi ni wa nne, na kaka zangu wote wameshaoa. Nyumbani niko mimi na mdogo wangu wa kike.

Mama yetu ni mlevi wa kupindukia, analewa siku nzima, mara nyingine analala kwenye vilabu vya pombe watu wanamuokota wanamrudisha nyumbani, au wakati mwingine analala nje mpaka asubuhi.

Hapa mtaani wameshamjua kwa tabia zake mbovu na matendo mengi sana ya aibu anayoyafanya, mpaka kufikia wakati anakuwa na mahusiano ya kimapenzi na watoto wadogo wa kuwazaa kabisa. Ameshafumaniwa kwenye majumba ya watu akifanya mapenzi na walevi wanaomuokota vilabuni akiwa amelewa na kwenda kumfanyia mambo mabaya.

Baba yetu alishafariki tangu mwaka 2013 kwa maradhi ya kisukari, jambo lililofanya mama yetu kupata mwanya wa kufanya mambo ya ajabu, ya ajabu, ya ajabu na ya kutisha!

Kipindi baba yetu yuko hai, alikuwa anagombana vibaya sana na mama kwasababu ya ulevi wa mama na mambo yake ya kushindwa kulea familia mpaka ikafika kipindi baba akahama nyumbani akaenda kupata mwanamke mwingine!

Baada ya kifo cha baba yetu, tulipata mirathi ambayo inaingia kwenye akaunti ya mama yetu kwa awamu kila mwezi.

Fedha hizi za mirathi ndizo anazotumia kufanya ulevi na umalaya wa kutisha na walevi wenzake.

Kila mara anarudi nyumbani amepigwa, amechaniwa nguo na kudhalilishwa na hao waume zake wasiojulikana.

Kiufupi mama yetu amegeuka dampo la kila mlevi kumfanyia uchafu.

Tumeshamkanya na kumuweka vikao vya familia zaidi ya mara mia moja lakini hasikii lolote.

Mimi ni mwanachuo, na nilipopata likizo nikasema ngoja niende nyumbani nikawasalimu kidogo. Lakini matokeo yake nimekutana na mambo ya kutisha na kuniumiza sana moyo wangu.

Imefika wakati mpaka napatwa na ghadhabu na kuanza kurudishiana nae maneno makali. Matokeo yake ananitukana sana na kunilaani.

Namchukia sana mama yangu!
Fanya maarifa wambambikizie kesi afungwe hata miezi sita jela! Akirudi anaweza kubadilika!
 
Pole sana ndugu . Mtihani wako ni mzito. Cha kukushauri mwombe sana Mungu maana sijaona njia nyingine yoyote unayoweza pata msaada zaidi ya Kwa Muumba wako. Jaribu kuwashirikisha watumishi wa kiroho jambo hilo. Ukiona mtihani ni mkubwa kwako jua kwamba aliekumba anaamini kuwa unaweza kuovercome
Cha kuongezea kuna hizi rehab centers unaweza kwenda kuulizià utaratibu ukoje kisha lipia apate uangalizi wa kitaalam zaidi. Hakikisha Hio rehab iko mbali na hapo alipopazoea
........MPENDE MAMA YAKO YEYE NDIYE ALIYEKUZAA HUNA MWINGINE
 
Mdau ...kwanza hongera kwa ujasiri ulionao kushare hili jambo, kuna watu wengine wanshindwa kushare mambo mpk wanajikuta wanapata msongo wa mawazo pengine na yeye anaishia kuwa mlevi bila kujua. Ni matumaini yangu umeshare hii experience yako ili upate msaada. Mi nikisoma content yako i can feel unampenda mama yako sana, naomba nikupe moyo endelea kumpenda hiki ndicho anachohitaji most show love zaidi kwake hata kama una muda akiwa anaenda kilabuni nenda nae kaa nae karibu mwambie unafanya hivyo kwa sababu unampenda, mi naona kuna pain mama yako anaficha hataki mjue pain aliyonayo so anajificha kwenye ulevi kitu ambacho si kizuri hiyo ni moja ya hatua ya kwanza kumsaidia mama yako.
Hatua ya pili naona watu wengi wamekushauri nenda kwenye maombi hii inaonyesha kuwa kitu mama yako anachopitia kiko more spiritual ambacho kinahitaji certain power ku overcome, kwa Mungu kila kitu kinawezekana kinachohitajika kwanza ni IMANI.
Je kwenye hili unaamini kuwa Mungu anaweza kubadilisha hali ya mama yako. Kama uko tayari kumsaidia mama yako na uko tayari kusimama kwa ajili ya mama yako niambie nikutumie prayers na muongozo wa maombi ya kumsaidia mama yako.
 
huenda na Tigo wamekula aiseeh!
lakini nikutie moyo tu! ichukie tabia yake lakini usimchukie yeye!
wakati mwingine ubongo ukivurugwa binadam hufanya mambo ya ajabu!! Tafta mbinu nyingine ya kuitokomeza hiyo tabia;
huenda ana pepo kivuruge huyo!
Na huyo akiacha pombe atakufa! maana pombe ishakuwa addiction na misuli ya damu, mfanyieni sobbing na maombi
Please naomba ufute sentensi yako ya kwanza. Mleta mada kaja kutafuta faraja na ushauri. Usimzidishie maumivu.
Tafadhali sana, naomba ufute
 
Back
Top Bottom