Namchukia sana mama yangu mzazi

Namchukia sana mama yangu mzazi

True that, lakini wafanye namna ya kumuokoa wabuni mbinu mbadala mkuu tabia ni chafu kama mama kuzifanya najua zinapelekea hata huyo binti mdogo kupata mfadhaiko kwa tabia za mama ake lakini kusema hivo haitoshi wamsaidie
Hilo limeshasababisha Mgogoro ndani ya Nyumba, na watoto hawatakuwa sawa kisaikolojia.. Haya Mambo yananifanya Nikumbuke Mbali!
 
Mazingira yanaweza kuwa chanzo kikubwa sana cha tabia zake, ongaea na nduguzo muangalie namana ya kumuhamisha yaan kubasili mazingira, mpangieni ata self contained, au nyumba ndogo tu kwenye mazingira tofauti na aliyopo sasa, naamin itasaidia sana.
 
Pole sana mkuu, ni ngumu sana hii ila usimchukie Mama yako, mpende, muonyeshe upendo wewe na ndugu zako, kama hamna ukaribu nae kuweni karibu nae ndo mtapata kujua kwa nini anafanya hayo. Msisahau kumuombea pia, maana maandiko yanasema "Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya".
Luka 6:28.
 
huenda na Tigo wamekula aiseeh!
lakini nikutie moyo tu! ichukie tabia yake lakini usimchukie yeye!
wakati mwingine ubongo ukivurugwa binadam hufanya mambo ya ajabu!! Tafta mbinu nyingine ya kuitokomeza hiyo tabia;
huenda ana pepo kivuruge huyo!
Na huyo akiacha pombe atakufa! maana pombe ishakuwa addiction na misuli ya damu, mfanyieni sobbing na maombi
Tumia staha mpe heshima yake hata km hajieshimu
 
Nikupe pole kwa hayo yaliyokufika pia Santana maji yameshamwagika, wakianza kuanggalia jinsi wanavyoparanganyika kwa tabia ya mama watazidi kumpoteza wamsaidie tu heri huyu wanamuona mkuu wanamshika wamnambeba wanamsafisha kuna mwengine anatamani hata kumgysa na kumshika lakini haiwezekani walishawazika
Hilo limeshasababisha Mgogoro ndani ya Nyumba, na watoto hawatakuwa sawa kisaikolojia.. Haya Mambo yananifanya Nikumbuke Mbali!
 
Pole sana kiongozi.

Biblia inasema kama ndugu akipotea, basi mrudishe kwa upendo. Mama yako anahitaji sana upendo wenu na kumrekebisha kwa upendo.

Lakini pia huu upendo unaweza ukaufanya kwa matendo, akija amelewa mwandalieni chakula, mpikieni supu, mpeni maji ya kunywa.

Unywaji wa namna hiyo mwisho wake ni ugonjwa wa figo. Zuieni haya kwa kumpa maji kila wakati kwa upendo mkubwa.
 
Kama ulivyosema, mama kayaanza hayo siku nyingi, tangu akiwa na baba yako, hivyo inaelekea ni sugu katika huo uteja wake na si ajabu alikutana na baba yako katika mazingira hayo hayo na baba yako akaamua kuwa naye na kushindwa kumdhibiti.
Sijui kama mtaweza kumbadilisha, ninachoshauri ni kumtengenezea mazingira ya kukosa kinywaji kwa muda, ili akili yake iwe timamu na awekwe chini na watu wa familia, ukoo na wa dini, pamoja nanyi, angalau muafikiane naye kama ni kunywa, basi apate kinywaji chake hapo nyumbani. Maana hiyo ya kutoka nje ya nyumba, inapelekea maisha yake kuwa hatarini kwa kila hali. Na pia akiafiki, apatiwe matibabu/ nasaha za kumwezesha kuacha au kuwa na staha katika uteja wake.
 
Ukiwa na Kichwa Chepesi huwezi kuelewa, Karibu JF
Acha utoto mtu anataka apate mawazo mengi achanganue, nyie mnaotoka chuo miaka hii mnajifanya mnajua mambo tunawachora tu na kiherehere cha mbele
 
kuna mwengine anatamani hata kumgysa na kumshika lakini haiwezekani walishawazika
Kabisa Mkuu hata mimi sasa namshukuru Mwenyezi Mungu, mimi nilikuwa nawachukia wote wawili na nilitamani hata wafe.. siku nikisikia natembelewa na baba au mama shule inakuwa siku ya huzuni sana kwangu.. ila Namshukuru Mungu at the Moment i love my Momma the Most!
 
Mkuu huyu anazungumzia mambo yanayomsibu, anahitaji courage, na ushauri wa vipi ataweza kumsaidia Mama, ili awe kama mama wengine wanojali familia zao,
VIPI NDO MAMA YAKO KISHA MTU AANDIKE KAMA WEWE, UTAJISKIAJE, NA

Na Mama anauma sana kuliko hata mke au Mume, kwani Mke/Mume waweza pata mwingine na ukamsahau wa mwanzo moja kwa moja, MAMA HUWEZI PATA MWINGINE hata ajitokeze mlezi akawa na Mapenzi kuliko Mama Mzazi, lakin still hawezi kuiziba nafasi yake completely
Umeongea point kama mimi niliwaza
 
Acha utoto mtu anataka apate mawazo mengi achanganue, nyie mnaotoka chuo miaka hii mnajifanya mnajua mambo tunawachora tu na kiherehere cha mbele
Unazungumzia vitu sijavizungumzia, Chuo imetoka wapi? kiherehere kimeingiaje hapa? jenga Hoja kama mtu mwenye Akili!
 
Mkuu kama kuna uwezekana wa kumuhamishia ugenini itapendeza sana japo kwa muda.
Ile kabla hajaanza kuzoea mazingira atakua hanywi hivyo itakua ndio muda sahihi wa kumpa nasaha. Tofauti na sasa mnaongea nae akiwa kalewa hapo hakuna mnachofanya.
 
Wakuu habari zenu,

Inawezekana hili ni jambo ambalo linaonekana kama ni gumu sana, lakini nisiwe mnafiki, maisha yangu yote sijawahi kuuonja upendo wa mama.

Nyumbani tuko wa tano, mimi ni wa nne, na kaka zangu wote wameshaoa. Nyumbani niko mimi na mdogo wangu wa kike.

Mama yetu ni mlevi wa kupindukia, analewa siku nzima, mara nyingine analala kwenye vilabu vya pombe watu wanamuokota wanamrudisha nyumbani, au wakati mwingine analala nje mpaka asubuhi.

Hapa mtaani wameshamjua kwa tabia zake mbovu na matendo mengi sana ya aibu anayoyafanya, mpaka kufikia wakati anakuwa na mahusiano ya kimapenzi na watoto wadogo wa kuwazaa kabisa. Ameshafumaniwa kwenye majumba ya watu akifanya mapenzi na walevi wanaomuokota vilabuni akiwa amelewa na kwenda kumfanyia mambo mabaya.

Baba yetu alishafariki tangu mwaka 2013 kwa maradhi ya kisukari, jambo lililofanya mama yetu kupata mwanya wa kufanya mambo ya ajabu, ya ajabu, ya ajabu na ya kutisha!

Kipindi baba yetu yuko hai, alikuwa anagombana vibaya sana na mama kwasababu ya ulevi wa mama na mambo yake ya kushindwa kulea familia mpaka ikafika kipindi baba akahama nyumbani akaenda kupata mwanamke mwingine!

Baada ya kifo cha baba yetu, tulipata mirathi ambayo inaingia kwenye akaunti ya mama yetu kwa awamu kila mwezi.

Fedha hizi za mirathi ndizo anazotumia kufanya ulevi na umalaya wa kutisha na walevi wenzake.

Kila mara anarudi nyumbani amepigwa, amechaniwa nguo na kudhalilishwa na hao waume zake wasiojulikana.

Kiufupi mama yetu amegeuka dampo la kila mlevi kumfanyia uchafu.

Tumeshamkanya na kumuweka vikao vya familia zaidi ya mara mia moja lakini hasikii lolote.

Mimi ni mwanachuo, na nilipopata likizo nikasema ngoja niende nyumbani nikawasalimu kidogo. Lakini matokeo yake nimekutana na mambo ya kutisha na kuniumiza sana moyo wangu.

Imefika wakati mpaka napatwa na ghadhabu na kuanza kurudishiana nae maneno makali. Matokeo yake ananitukana sana na kunilaani.

Namchukia sana mama yangu!
Pole Sana kaka huyo ndio mama yako usithubutu kumvujia heshima wala kumrushia maneno mabaya kama mmesha mkanya muacheni Mungu ndio anajua akikulaan Lana lazima ikufike
 
Mnao comment utani please
Najaribu kujiweka Mimi naona naweza onekana mjinga Ila inauma sana
Ila kwa kuwa ni mama basi tu angekuwa Dada hata makofi angeluka Ila ni mama yake
 
Jamani, we ulifika mbali
Kabisa Mkuu hata mimi sasa namshukuru Mwenyezi Mungu, mimi nilikuwa nawachukia wote wawili na nilitamani hata wafe.. siku nikisikia natembelewa na baba au mama shule inakuwa siku ya huzuni sana kwangu.. ila Namshukuru Mungu at the Moment i love my Momma the Most!
 
If she doesn't have you, the fruit of her womb then who does she have to back her up in this dirty filthy world?

Unajiita msomi wakati mentally you are still a slave. A slave to what people think of your Mommy. And here you are judging her and calling her a whore. Pathetic.

That is your Mother. Despite everything she is your Mother! Fight with every breath you have to get your Mother back and shame the devil.

To begin with, fight alcoholism. You know how? Take her to Rehab in a different town. Pay the fees there. Have her Booked. Visit her and make sure all her needs are taken care of.

Alcohol is the mother of all evils. Alcohol made you lose your Mom. You need to appreciate your Mom despite everything. She could have chosen to abort your little asses while she was pregnant but she fought all the pregnancy woes and gave birth to you little monsters who are there mnabana pua na kumuita mlevi na malaya. SMDH.

Prove the world wrong. Put to shame those evil people taking advantage of her drunken stupor. Fight for your Mama young Man.
 
Back
Top Bottom