Namchukia mama mkwe, yaani hatari

Namchukia mama mkwe, yaani hatari

Mastamind

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
1,319
Reaction score
847
Kichwa cha habari chahusika,
Nimemaliza chuo mwaka juzi, sijapata kazi mpk time hizi, familia yangu ni ya kimasikini, kutoka ni kwa juhudi zako binafsi, swala la mahali au ndoa wazazi hawalitambui ni juhudi zako pekee.

Nilikuwa na uhusiano na binti mmoja takribani miaka mitano sasa, mwanzoni mwa mwaka huu nilianza kuishi nae kwangu kama mke na mume, mama yake alivyogundua yuko kwangu alianza kumsumbua arudi nyumbani haraka, kwa siku simu zilipigwa takribani 50 kumtaka arudi nyumbani sababu akidai ni aibu kubwa kwake na ukoo wao binti kuishi kwa mwanaume kabla ya mahali, na anadai yeye alichumbiwa, akatolewa mahali na harusi ikafungwa ndo akaenda kwa mwanaume sasa yeye mwanae iweje asifuate taratibu hizo,? ilifika mahali ikabidi nimruhusu aende kwao kufika huko aligombezwa sana na kuahidiwa kulaaniwa endapo atatoroka kuja tena kwangu, na mama mkwe ashapanga hadi mahali anadai ni milioni 3, sijui kisa binti yake ni mzuri na mweupe (kwa wasukuma mnaelewa hilo)

Sasa wajameni nimetokea kumchukia mama mkwe kiama, anatumia ufukara wangu km fimbo yakunichapia kwani nilishamueleza nikipata hela niko serious kufuata taratibu zote hizo lakin anamwambia mwanae mimi ni taperi.
USHAURI BANDUGUZ:A S 103::spider::clock:
 
hata ukimchukia mama mkwe ni bure tafuta pesa tatizo ni pesa tu chakarika ukaoe jumla kijana maana mama mkwe wako yuko sahihi
 
Usimchukie sababu nyie vijana wa kileo ni ngumu kuaminika maana ukishammega vya kutosha binti wawatu unaanza kumuona ana mapungufu,ukipata na kazi ukutane na wale wa kazini ndo kabisaaa unamtosa.
Acha kummega mtoto wa watu tafuta pesa kwanza uje utoae mahali,hata kama ni mtoto wako utakubali akae na jamaa linamtumia tu halieleweki....."ikimbieni zinaa"
 
Unamchukia kwa kumwambia mtoto wake arudi kwao au mahari kubwa?

Huyo mama ana busara na mtoto wake ni mjinga hawezi kuhamia kwa mwanaume bila kufuata utaratibu. Si lazima umuoe lakini kupata baraka za wazazi ni vizuri. Mama ana haki mtoto alikuwa anamdhalilisha kwa kuja kuishi kwako bila makubaliano ya wazazi wako na wazazi wa mwanamke. Kwa kifupi alikuwa anajirahisi kwako huyo mwanamke
 
Mama hana kosa, kosa ni lako. Wala usimchukie mama....tena una kosa kumwita mama mkwe, bado hajawa mama mkwe, iwe kimila au kidini...
Jipange tu kijana, kama sio rizki hailiki..
 
pole sana mkuu.lakini mama mkwe hana shida sana hapa anajaribu kulinda heshima ya mwane na ya familia jichange change upate pesa mkuu,maisha ni magumu lakini inawezekana zidi kupambana kutafuta ajira.ninakijua unajua unachokipitia pole sana braza ,nikishauri usimchukie mama mkwe ,hamna anaweza kufanya tofauti na hivyo,all ze best!
 
Kwanini umgegede mwenzio bila ridhaa ya wazazi?hv ikitokea kwa mtoto wako utafanyaje?
 
Yaani we ulitaka ukae na mtoto wa watu bila ndoa afu iweje? Yaani wewe ulitaka wazai wake wafurahie tu kusikia mtoto wao anaishi na mwanaume bila ndoa? Mbona bado sijaona sababu ya kukufanya umchukie mama mkwe...

Labda uniambie mahari ni kubwa lakini hata kama ni kubwa mara zote mahari hua unaweza usimalize yote ukalipa kiasi afu mkafuata taratibu za kiimani mkahalalisha.

Tena usilete mambo yako ya ajabu, kama unahitaji mke tafuta watu wenye busara wakusaidie ukamilishe taratibu zote sio kuleta zako hapa.

Tena mwombe Mungu msamaha fasta kwa kumchukia huyo mama.
 
Hivi angekuwa dadaako ndio kafanyiwa hvyo ungefurahi?? Huoni hata aibu kumchukia mama wa watu? Ww ulitaka uishi naye bure tu bila kumtolea chochote? Ningekuwa mm ndio kaka yake ningekuvuruga kweli aisee. Yaan mwanaume mzima unataka vya bure
 
Milion 3 taslim?
pesa halali kwa malipo ya kitanzania?
mahari!!
:mvutaji::mvutaji::mvutaji:
 
Kwanza huna adabu na umshukuru Mungu hujaishia Mahakamani kwa kesi ya kukaa na mtoto wa watu bila taratibu.


Kwani vijana wa siku hizi taratibu hamzijui? unapatawi guts za kukaa na binti wa watu je akiugua au kukufia utanzaje kujieleza?

Unatakiwa ukamwombe radhi mama wa watu kwa unynyekevu na kuahidi kufuata mila zote pindi ukiwa tayari.
 
Wewe si kijana mzuri,ungekuwa kijana mzuri ungeenda kujitambulisha na kufuata taratibu nyingine kabla ya kuishi na huyo binti,milioni 3 sio ishu mahali haimalizwi wewe,jichange hata laki 5 alafu tafuta wazee muende kwa wazazi wa binti.
 
Uko sahihi...

1. Kuowana ni mkataba (implied kama hauko katika maandishi) wa makubaliano kati ya watu wawili mwanamme na mwanamke
2. Influence yoyote ya wazazi ni kinyume na haki ya uhuru wa mtu kuoa au kuolewa
3. Mahali sio criteria ya ndoa (zipo kesi ambazo tayari zimeshakuwa ruled kwa jambo hili)
4. Kuendelea kuishi na mkeo mpendwa huyo kwa sasa UAMZI UPO MIKONONI MWAKE YEYE MKEO
5. Usiache kutoa mahali kwa maana ni valued culture katika Tanzania yetu
6. Tengeneza mazingira ya mama mkwe wako kukuamini na kukupenda
7. Kama unamchukia, sina uhakika kama utaendelea kumpenda huyo dada kama yeye anampenda mama yake..

Unahitaji ushauri mkuu
 
Back
Top Bottom