Oa mwingine!!!
Aoe ana hela? Kinachomshinda kwa huyu atakiweza kwa mwingine?
Oa mwingine!!!
Kichwa cha habari chahusika,
Nimemaliza chuo mwaka juzi, sijapata kazi mpk time hizi, familia yangu ni ya kimasikini, kutoka ni kwa juhudi zako binafsi, swala la mahali au ndoa wazazi hawalitambui ni juhudi zako pekee.
Nilikuwa na uhusiano na binti mmoja takribani miaka mitano sasa, mwanzoni mwa mwaka huu nilianza kuishi nae kwangu kama mke na mume, mama yake alivyogundua yuko kwangu alianza kumsumbua arudi nyumbani haraka, kwa siku simu zilipigwa takribani 50 kumtaka arudi nyumbani sababu akidai ni aibu kubwa kwake na ukoo wao binti kuishi kwa mwanaume kabla ya mahali, na anadai yeye alichumbiwa, akatolewa mahali na harusi ikafungwa ndo akaenda kwa mwanaume sasa yeye mwanae iweje asifuate taratibu hizo,? ilifika mahali ikabidi nimruhusu aende kwao kufika huko aligombezwa sana na kuahidiwa kulaaniwa endapo atatoroka kuja tena kwangu, na mama mkwe ashapanga hadi mahali anadai ni milioni 3, sijui kisa binti yake ni mzuri na mweupe (kwa wasukuma mnaelewa hilo)
Sasa wajameni nimetokea kumchukia mama mkwe kiama, anatumia ufukara wangu km fimbo yakunichapia kwani nilishamueleza nikipata hela niko serious kufuata taratibu zote hizo lakin anamwambia mwanae mimi ni taperi.
USHAURI BANDUGUZ:A S 103::spider::clock:
Haujaelewa au unatafakari?Milion 3 taslim? pesa halali kwa malipo ya kitanzania? mahari!! :mvutaji::mvutaji::mvutaji:
Usimchukie sababu nyie vijana wa kileo ni ngumu kuaminika maana ukishammega vya kutosha binti wawatu unaanza kumuona ana mapungufu,ukipata na kazi ukutane na wale wa kazini ndo kabisaaa unamtosa.
Acha kummega mtoto wa watu tafuta pesa kwanza uje utoae mahali,hata kama ni mtoto wako utakubali akae na jamaa linamtumia tu halieleweki....."ikimbieni zinaa"
Hiyo suti yako inanichanganya ujue....Haujaelewa au unatafakari?
huna adabu! zaa wakwako kisha muoe hivyo kihunihuni! kazi yenyewe huna! unawaza ngono tu! hao watoto utawalisha kondom!?[/QUO
Tena huyu sio hana adabu tu ila hata akili ya kufikilia hana shwain huyu
Uko sahihi...
1. Kuowana ni mkataba (implied kama hauko katika maandishi) wa makubaliano kati ya watu wawili mwanamme na mwanamke
2. Influence yoyote ya wazazi ni kinyume na haki ya uhuru wa mtu kuoa au kuolewa
3. Mahali sio criteria ya ndoa (zipo kesi ambazo tayari zimeshakuwa ruled kwa jambo hili)
4. Kuendelea kuishi na mkeo mpendwa huyo kwa sasa UAMZI UPO MIKONONI MWAKE YEYE MKEO
5. Usiache kutoa mahali kwa maana ni valued culture katika Tanzania yetu
6. Tengeneza mazingira ya mama mkwe wako kukuamini na kukupenda
7. Kama unamchukia, sina uhakika kama utaendelea kumpenda huyo dada kama yeye anampenda mama yake..
Unahitaji ushauri mkuu
Imagine angekua mtoto wako anagegedwa na njemba .... ungefurahi?
Hahahahaha yeye alitaka wazazi wa binti wamuonee huruma kisa hana kazi . Tena hii ya kutokua na kazi ni sababu tosha kuwa hana uwezo wa kutunza mke. Huyo binti hajielewi ndio maana akaamua kukaa na jamaa bila kufuata utaratibu.Mkuu mtoa mada fuata taratibu mke utapewa tu kama walivyokwambia lipa mahali usitafute ugomvi na wakwe .Yaani we ulitaka ukae na mtoto wa watu bila ndoa afu iweje? Yaani wewe ulitaka wazai wake wafurahie tu kusikia mtoto wao anaishi na mwanaume bila ndoa? Mbona bado sijaona sababu ya kukufanya umchukie mama mkwe...
Labda uniambie mahari ni kubwa lakini hata kama ni kubwa mara zote mahari hua unaweza usimalize yote ukalipa kiasi afu mkafuata taratibu za kiimani mkahalalisha.
Tena usilete mambo yako ya ajabu, kama unahitaji mke tafuta watu wenye busara wakusaidie ukamilishe taratibu zote sio kuleta zako hapa.
Tena mwombe Mungu msamaha fasta kwa kumchukia huyo mama.
Afadhari hatuonani hivi ungemuona mtoa mada si ungempiga kelbu wewe lol. Hahahaha sipati picha ambavyo ungemkata mitama na vikofi vya hapa na pale . Ukizingatia huyo ni binti yako halafu lijamaa linaleta hizi hadithi humu khaaaaaa. Jamaa anataka kuhurumiwa yeye fukara, inashangaza kijana msomi na mzima wa afya analia lia kipuuzi eti ufukara kwani ufukara kilema.Kijana huna adabu na maadili halafu unakuja kulia lia hapa...
Utaendelea kumchukia mama wa watu na binti utamkosa kinyangarika wewe...