Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 42
A little while ago one of the cream of analytical politics of Tanzania had this to say with regard to the so called Kibanda;
Baada ya mashinikizo, vitisho, vitimbi na kejeli za kila aina kutoka kwa "Mhariri mtendaji" wa gazeti la TanzaniaDaima Absalom Kibanda hatimae Zitto Kabwe ame succumb to the pressure na kuondoa jina lake kwenye kinyang'anyiro cha ugombea wa uenyekiti wa Chadema.
Tukirudi nyuma kidogo na kuangalia mlolongo wa matukio kuelekea Zitto kujitoa, jina la Bwana Kibanda linachomoza mithili ya mnara wa kuongozea meli bandarini.
Huko aki defy obvious principles za conflict of interest Kibanda akishirikiana na "Baba mkwe" mzee Mtei wameweza kum bully Zitto na hata kufikia kujaribu "kumhonga" cheo (kama alivyonukuliwa Zitto mwenyewe).
Kibanda amei aibisha fani ya uandishi, yeye mwenyewe, Mbowe na Chadema kwa ujumla kwenye sakata hili ambapo demokrasia imechinjwa wazi wazi mchana kweupe.
Unless Kibanda anafikiri atafanya kazi TanzaniaDaima maisha yake yote labda ndio amefanya hayo aliyo yafanya lakini kama kutakuwa na maisha nje ya TanzaniaDaima basi what we have seen is just the beggining of the end of Absalom Kibanda.
Time will tell....
Masatu hii thread yako kavu sana haina hoja wala mashiko. Kuwa mahsusi kwenye tafakuri ya Kibanda. Jibu hoja kwa hoja aliyoandika siyo maneno ya kijumla jumla tu. Kwani Zitto hawezi kukosea? Mbona kuna wakati alishabikia ununuzi wa mitambo ya Dowans na JF ilimrekebisha. Nilisoma vizuri habari ya Kibanda na kulikuwa na hoja. Vilevile Maswali Magumu alitoa habari inayomshauri Zitto kwa manufaa ya chama.
Sasa wewe unaona hali ya sasa baada ya mvutano wa uchaguzi wa mwenyekiti ya Chadema kuwa ya kuvutia? Habari ya Kibanda na ya Maswali Magumu (Ansbert Ngurumo) jumapili iliyopita ilikuwa ni ushauri mzuri sana ili Chadema iendelee kuwa imara hasa kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kukiko kumchukia Kibanda na kuchafua tu jina lake bila sababu ya msingi, Masatu toa tafakuri ya kujibu hoja kwa hoja. Kwanza toa habari ya Kibanda hapa kuhusu Zitto halafu ujibu hoja kwa hoja. Sote tunajua umuhimu wa Zitto katika vita ya ufisadi tangu Buzwagi, lakini hii haina maana kuwa kukiwa na tatizo asishauriwe. Hiyo Sahihi yako kuhusu Kibanda ninaitafsiri kuwa ni chuki kwake, kwa vile sijaona hoja uliyotoa zaidi ya malalamiko ya juu juu na jumla jumla. Tafadhari tumia JF vizuri.