Kesho Jumatano katika Tanzania Daima nimeandika sehemu ya pili ya makala hiyo. Kwanza nimemuomba radhi Sitta na Watanzania kwa lugha kali niliyotumia dhidi yake na dhidi ya Watanzania wenzangu. Naamini katika kukosoana. Nimekiri mapungufu katika maandishi yangu. Hata hivyo nimesisitiza msimamo wangu kuhusu Sitta uko pale pale. Nimejaribu kutumia lugha ya staha kueleza kile ninachoamini kuhusu sakata la Dowans na vitanzi tulivyojifunga
Pole sana Kibanda! Umesahau kitu kimoja... Kusoma ni jambo moja na kuelewa ni jambo jengine! Baadhi ya wasomi wetu wa kileo, upeo wao ni mdogo sana, kwa sababu wao wanataka kuamini kile walichokwishaamini hivyo basi anaweza kusoma paragraph moja tu, akahitimisha habari nzima na kutoa hukumu zake. Hapo ndipo wanapozusha na hawaambiliki!!Kwa hiyo umesoma issue ya kwanza na ya pili ya UMOJA halafu unaandika uongo hapa kwamba kwenye jarida hilo kuna utetezi kwa mafisadi. Ama kweli tunajenga taifa la hatari la watu wasomi wazushi. Hebu waandikie wasomaji humu ukitoa ushahidi wa hilo ulilosema.
Leo sitochangia hadi nihisome makala hiyo ya pili, Cha msingi KIBANDA simamia msimamo wako na wadau mnao amini kuwa KIBANDA kanunuliwa na mafisadi tunaomba ushahidi. KIBANDA ni member humu JF hivyo mkitoa ushahidi tutasubiri utetezi wake na kisha tutachambua mchele ni hupi na chuya ni zipi.
Thubutu... afanyeje??? Kule ndiko anakojua kwamba angalau angali na chochote na anaheshimika labda hamumjui mzee yule! Ulizeni wanaojaribu kugombea nae ubunge kule jimboni kwake mtapata habari zake. Mnadhani jimboni kwake wanamtaka! Ila wale wapinzani halisi huwa anawawahi kimtindo wa kutumia dola biashara inaisha anabaki na mngombea dhaifu. Akitoka huko na kuja mjengoni anaonekana shujaa! Lakini kwa akili zetu wacha na tumuone shujaa kwa muda, wakati utafika kila ukweli utajulikana... kama mjuavyo media zikikubeba utaonekana na siku zikikuacha ndio mporomoko na mengineyo yanajulikanaSitta si safi na kama safi angeruhusu mjadala wa Richmond uendelee mpaka kuparta muafaka bungeni na kwa hesabu tu marupurupu ya Spika yanazidi ya Uwaziri alionao ndo maana anakurupuka.
Sikatai anasema jambo jema lakini wasiwasi wetu wananchi ni kwamba hizi ni hasira za kuukosa uspika.
Kama safi ahame chama maana kinanuka
Mkuu, Kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni yake na hatoi maoni kwa sababu ya kumfurahisha mtu bali kutoa ukweli uliomo ndani ya nafsi yake. Mzigo wa moyo hautuliwi kwa kuwafurahisha watu, Koti la mfalme likiwa na mawaa aambiwe... ili asiaibike. Lakini tukitaka kufurahishana (si ni heri tununuliane chai na vitafinwa) sio katika mambo na mustakabali wa Nchi. Hii ni Nchi yetu sote lazime tuwe na muono tofauti ili tupate kilicho bora. Tukiwa na mawazo ya aina moja basi itakuwa Nchi ya wendawazimu na tusio na fikra bali kufatana kama mchwa hata kama tunatumbukia mtoni!!Nakushukuru kwa uvumilivu wako na kwa uzito wa maelezo yako. Nilikaribia kuiweka hapa lakini nimeogopa kuwakera wengi kwa uurefu wake
Kama nilivyochangia kule kwenye thread ya hoja kwenda kwa Balile wa Mtanzania, mathinkers wengi humu tunaelekea kuwa mediocres-hatusomi.Mwandishi anafanya kitu ambacho watanzania wengi na hata wachambuzi makini wameshindwa kukifanya. Kibanda amekuwa akindika kila wiki kwa takribani mwezi sasa katika Tanzania Daima la Jumatano kumkashifu Sitta na akionekana kuchekelea zigo la mabilioni wanayotakiwa kulipwa Dowans. Kibanda amekuwa akichekelea lakini kwa ujanja ambao si wake, amekuwa akisukuma zigo hilo eti ni lawama kwa Sitta na Bunge lake lililozikataa Richmond na Dowans.
Balile amekuwa akiandika upuuzi huo na hakuna wa kumjibu, mathinker wanapotumia jukwaa hili kujibu kwa hoja sadifu, mathinker wanaotakiwa kusoma wanaishi aya ya kwanza na kuanza kulaumu, kama si ujinga wa kweli, basi nadhani kuna watu wanahujumu hili jukwaa kwa kuanzisha mada za kupuuza michango yenye nguvu matokeo yake jukwaa hili litakosa maana.
Hebu tuwe na culture ya kusoma. Tuache uvivu. Yaani pages 2 watu mnalalamika. By the way hayo yalishajadiliwa hapa JF
Kabanda, Balile, Kibonde deserve a place in CCM's propaganda newspaper Uhuru and not progressive and highly respected papers like Tanzania Daima.Everyday, now & then, we said here JF, most journalists including this one, are stupid, waganga njaa, illeterate, arrogant & ignorant too,
it doesn't matter how long he has been writting articles, he thinks using his foolish, idiot mind can convince or persuade all of us kwa issue
ya UWIZI MKUBWA wa wazi kama wa DOWANS, as i said ni ujinga wake unamsumbua, he is dirty to discuss him, Prostitution of journalism, hana lolote
hana uzalendo ( Patriotism)
watu wanachoka kusoma summarize
Yaani hueleweki. Hoja zako zinajipinga zenyewe.
bandikeni alichoandika Kibanda la sivyo acheni ngojera humu
Kibanda kuna kitu kinaitwa jf public opinion kwenye issues mbali mbali. Ukitofautiana na public opinion hizi tegemea matukano.Naamini Jamiiforums ni Home of Great Thinkers sasa hawa ndugu zangu akina informer na wengine ni kwa nini wanashusha tuhuma nyingi wasizo na uhakika nazo. Mimi ndiye Absalom Kibanda. Nimekuwa Mhariri wa Tanzania Daima huu ni mwaka wa nne na ninaelekea wa tano. Msimamo wangu kuhusu mambo kadha wa kadha haujabadilika.

Kila mtu ana uhuru wa kufikiri anavyotaka. Niweke kumbukumbu sawasawa. Sina sababu hata moja ya kununuliwa na mtu yeyote. Rostam Aziz amekuwa mkurugenzi wangu Mwananchi na nikaacha kazi kinyume cha matakwa yake. Ninaamini katika mabadiliko. Nimeanza kumpinga Sitta kila anapofanya mambo ambayo sikubaliani nayo tangu akiwa spika na hata kabla Lowassa hajajiuzulu.

Nikiwa mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima ninatoa uhuru kwa viongozi wote pasipo kujali misimamo yao kutoa maoni yao. Nimeruhusu mijadala ya kina kupitia Tanzania Daima kutoka pande zote mbili. Kwangu mimi Rostam, Sitta, Lowassa, Chenge, Mwakyembe na wengine wote ni vyanzo muhimu vya habari na kwa Tanzania Daima wana nafasi sawa kihabari. Msimamo wangu huo uko bayana na kimsingi hili ndilo gazeti linalokimbiliwa na kila mtu, hatufungamani na upande wowote zaidi ya kupigania mabadiliko. Ninapata furaha nisikiapo nikituhumiwa kuwa wakala wa Chadema, mara wakala wa CUF, mara wakala wa mafisadi, mara wakala wa Kikwete kwa sababu ya msimamo huru wa mawazo.

Nilikataa tangu mapema kujiingiza katika vita ya ufisadi inayopiganwa na akina Sitta na akina Mwakyembe kwa sababu nimejiridhidhs kwamba ni vita ya kitapeli na yenye malengo ya kisiasa zaidi kuliko kihalisia. Naamini na hili nimekuwa nikiliandika katika safu yangu ya Tuendako kuwa ufisadi uliopo nchini unakigusa Chama Cha Mapinduzi moja kwa moja. Kwa hiyo hakuna anayeweza kumnyoshea mwenzake kidole. Viongozi wote wa juu wa chama hicho tawala wakianzia na mwenyekiti wao wa taifa hawana ubavu wa kukwepa tuhuma halisi za chama chao kuhusika katika ufisadi.

Hiyo ndiyo dhambi yangu iliyonikosanisha na wengi katika taaluma. Nimekataa kuingia katika mkumbo wa kujifanya mwanaharakati na jemedari wa ufisadi kwa kuwa naamini ni unafiki. Ni jambo la kheri kwamba wamiliki wa Tanzania Daima wanathamini mchango wangu, wanaufahamu na kuuamini msimamo wangu, wanaujua uzushi wa kila siku wa akina informer ambao wao wanalipwa mamilioni ya fedha kuwachafua akina Lowassa kwa sababu ambazo mimi ninazijua na ushahidi upo.

Acha nihukumiwe kwa haki huku nikiwa na uhakika kuwa ipo siku historia itanitetea
Everyday, now & then, we said here JF, most journalists including this one, are stupid, waganga njaa, illeterate, arrogant & ignorant too,
it doesn't matter how long he has been writting articles, he thinks using his foolish, idiot mind can convince or persuade all of us kwa issue
ya UWIZI MKUBWA wa wazi kama wa DOWANS, as i said ni ujinga wake unamsumbua, he is dirty to discuss him, Prostitution of journalism, hana lolote
hana uzalendo ( Patriotism)
KIBANDA KWA HILI TUKO PAMOJA ! sema tu, nimekuelewa na ninatayarisha nakala ya kutetea na kuuelewesha umma unamaanisha nini! just simple logic is needed!