Nalia Mie: Nani Muuaji wa Askari HUYU

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,037
Ndugu wa JF, nimepokea taarifa za kifo cha askari huyu "aliyejiua" baada ya kukosea kuelekeza msafara wa "RAHISI" wetu kule kwa ndugu zetu tarime. Uchungu nilionano ni mazingira ya utokeaji wa kifo chenyewe, eti alijipiga risasi baada ya kugundua amekosea kuulekeza msfara wa muheshimiwa mtukutu/fu. Hapa ndipo nilipoanza kujiuliza maswali magumu yafuatayo.

Moja, taarifa zinasema alijipiga akiwa kituoni akihojiwa bada ya kukamatwa, Swali, Inakuaje ajiue katika kituo hiki, silaha aliipata wapi wakati tayari alikuwa ni mtuhumiwa??

Pili, hadi anachukua silaha na kuikoki, walikuwa wapi walikokuwa wanamhoji? Labda walilala kidogo au walienda mslanai!!

Tatu, Alijipiga risasi tano, kwa mujibu wa taarifa zilizopo, ninavyoelewa mimi, risasi moja tu, ingetosha kumfanya atupe bunduki chini na kufa...lakini hapa tunaambiwa alijishindilia rsasi tano, aliouata wapi uhai na nguvu za kuendelea kujimimnia risasi hizi?

Nne, Iweje wahusika " waliokuwa wanamhoji" wasichunguzwe na kukamatwa wao baada ya tukio? Mbona tunasikia wapo nje tu....

Tano, Kwanini mazishi yanafanyika fasta fasta hata kabla ya uchunguzi kukamilika?

Sita, Je ni kweli tuamini kuwa kulikuwa na mkono wa "wanausalama" wakihisi kuwa askari huyu alikuwa na lake jambo?? HIVYO wakaamua kummaliza?

Mwisho, Ni nani hasa muuaji wa askari huyu? Nini uhalali wa kamati au tume inayoundwa kuchunguzwa kifo hicho?

Naskia Pia Mkuu wa Polisi wa Mkoa huo maalumu wa Kipolisi alikuwa Hukooo Dar wakati bosi wake alipotembelea Tarime....hapa napo pana kitendawili.

Maoni; kama kweli huyu askari alikua na ujasiri huo basi ni mfano wa kuigwa kwa wananchi wengine wenye tuhuma za udhalilishaji, wizi na udhulumati, tuwape RISASI nao wajimalize fasta.....Nakupenda Dada

Nakulilia afande wangu wa Ukweli......

Maandiko yanasema; Kila auwaye kwa Upanga nae atakufa kwa upanga.........
 
Wadu, hoja ndiyo hiyo, au mnaiigopa???
 
....haya maswali yapo sana mtaani kwa sasa! hivi ni wangapi sasa wana-rely taarifa za Polisi inapohusu jambo lao la ndani? wangapi wana trust na jeshi la Polisi hivi sasa tangu kamanda Mwema na 'mshikaji' Masha? mimi binafsi, I dont a word from them since three years ago maana imekuwa ni wing ya CCM.
 
Wana JF,

Hii habari inatukanganya sana wajameni hiiiii bha behi na tuubhaga gete gete, yaaani maelezo yamekuwa mengi mpaka naona ni mashikoro magheni.

Nadhani tume iliyo undwa nayo ianze kwa kiuwajibikaji ngazi kwa ngazi iwahoji wale wote walio tupia maneno kwa Dada yetu askari aliye jiua.

mi nalipenda kujua endapo askari ameteleza kidogo
(on Duty) katika hali ile anapaswa kuwajibishwa vipi kinidhamu?

Maaana wanalifumbia hili jambo as if kulikuwa na njama ya uhaini au?lets be open now naona watu wanashindwa sema hapa au ni watu walitaka kujionyesha wao ni maafisa usalama no. One wanaijua kazi kuwa huwa hawakosei? misafara ya Rais imekubwa na matukio mengi sana na ninapenda kuihijo Idara nzima ya Usalama wa Taifa na Ikulu kitengo kinachoshughurikia misafara ya Rais na hutujawai pewa majibu katika matukio yaliyotoke huko nyuma? Kunani hapa kwani Rais wetu akumbwe na matukio mabaya kila asafiripo tuuu je haya yote hutokea ndani ya nchi yetu au hata uko nje huwa nakubwa na matatizo kama haya?

Na nimara nyingi tumeona matukio ya uzembe yakitokea na wanao wajibishwa ni viongozi wa chini wenye vyeo vidogo sana na wasio na vyeo lakini wakubwa hawa/wao hawawajibishwi wala kuwajibika kwao kinidhamu hii inaashiria uonevu na hakuna uadilifu katika uongozi na kuna dosari kubwa sana, kila kukicha ni matukio juu ya matukio na kutopata solution yake na kuanikwa bayana ndio kwaendelea changia matukio kuongezeka kwani majibu hayarudi kwani tume iliyo undwa hurudi na majibu au muafaka na unafungiwa kabatini kwa hali hiyo tusitegemee mabadiliko yeyote katia administrations zetu zinazoongozwa na viongozi wa namna hiyo.

Me namwomba sana IGP Mwema kuliangali hili more professional and not politicaly, mtu huwezi ukakurupuka tu huko na kuji twika bullets wakati few hours ulikuwa online of Duty.
 
yaani alikamatwa akawa kituoni na bunduki mkononi? hivi wanapomkamata wanamwachia bunduki?..mbona sielewi? au walimtandika wao wenyewe wakasingizia tu...hatutaki mambo ya kina zombe tena sisi.
 
Hapo patamu, na mkuu wa mkoa wa Kipolis eti alikua Dar wakati haya yakitokea...naliliaaaaaaa jamaniiiiiiiiii tanzania tenaaaaaa hhiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
yaani msafara wa raisi tuliyemweka madarakani sisi wenyewe ndo usababishe kifo cha raia wetu hata kama alikosea....hapa tunahitaji maelezo. mimi sijui hii issue ikoje, ndo nasikia sasaivi,,..lakini nafikiri inahitaji maelezo ya kutosha.
 
MSIBA.jpg
Kifo cha kujiua kwa kujipiga risasi kilichofanywa na askari wa kike WP Suzana aliyekuwa amepangiwa kuzuia magari ili msafara wa Rais Jakaya Kikwete upite wilayani Tarime mkoani Mara kabla ya kwenda katika hafla kanisani, kimekuwa kama sinema.


Mwili wa marehemu Suzana duara pichani linaonyesha risasi zilipoingilia
Habari za kifo hicho zimethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya, Sebastian Zakaria ambaye alipozungumza na gazeti hili alisema askari huyo alijiua saa 7.05 mchana (juzi) ndani ya kituo cha polisi Tarime na wananchi wametafsiri kuwa ni kama sinema kutokana na walivyoona muingiliano wa vyombo viwili wa dola.

Habari kutoka chanzo chetu cha habari zinasema maofisa wa Usalama wa Taifa walipogundua msafara umepotoshwa walikuja juu kwa vitisho na wale wa polisi kunywea kabla ya kuchukuliwa hatua.


Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Askofu Raphael Mwita Akiri wakati wa ziara yake
"Ni kweli askari wetu amejiua baada ya kutoka kwenye eneo lake tulilokuwa tumempangia baada ya msafara wa rais kupita… sijui chanzo gani kilichomsibu," alisema Kamanda Zakaria.

Habari zaidi zinasema WP Susana baada ya kukosea kuelekeza msafara huo alifuatwa na maafisa wa Usalama wa Taifa ambao walimfokea kisha wakaamuru akamatwe kana kwamba wao ndiyo wakuu wake wa kazi.

"Baada ya muda mchache WP Susana alikamatwa na kupelekwa mahabusu kwaajili ya kuchukuliwa hatua kali zaidi," kilisema chanzo chetu cha habari ndani ya jeshi la polisi mjini Tarime.

Chanzo hicho kilibainisha kuwa kitendo hicho kilimkera marehemu hivyo akaamua kuchukua bunduki aina ya SMG na kujipiga risasi nne kifuani na kukata roho papo hapo na kuongeza kuwa askari huyo si mzoefu kwani alianza kazi hivi karibuni.


Rais Kikwete alipotembelea bwawa la Magumu katika ziara yake wilayani Serengeti, Mara
Watu walioshuhudia tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa askari huyo alikosea kuelekeza magari ya kwanza yaliyokuwa kwenye msafara ambayo yalitakiwa yaelekee Bomani ambako Rais Kikwete alikwenda ili asomewe taarifa ya wilaya na kusaini kitabu cha wageni.

Habari zinadai baada ya kufanya kosa hilo askari huyo alikamatwa na polisi wenzake kisha akapelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Tarime na kwamba huko wakubwa wake wa kazi walionekana wakiongea na watu wa Usalama wa Taifa na walimtisha na kumpiga mkwara kutokana na kosa alilofanya.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Dk . Charles Samson alithibitisha kupokea mwili wa askari huyo na kufafanua kuwa alijipiga risasi maeneo ya kifuani ambazo zilitokea mgongoni upande wa kushoto ambako ni eneo la moyo.

Alisema taarifa kuhusu tukio hilo alizipata akiwa kwenye msafara wa Rais na kwamba alipokwenda kumfanyia uchunguzi marehemu alibaini kuwa alikata roho muda mfupi baada ya kujipiga risasi.

Rais Kikwete alikuwa amekwenda Tarime kuhudhuria kusimikwa kwa Askofu, Dk. Raphael Mwita Akiri ambaye amekuwa Askofu wa Anglikana Jimbo Jipya la Rorya Tarime. "Kitaalamu kilichosababisha kifo ni risasi maana nimefanya uchunguzi na kubaini… sijui nini kimepelekea kujiua maana huo ni uamuzi mzito sana aliouchukua," alisema Dk. Samson.

Hili ni tukio la pili ndani ya siku nne kwani mwishoni mwa wiki Mkufunzi wa Chuo cha Tanzania Police Academy jijini Dar es Salaam, Konstebo Nole Paul Njega alijipiga risasi na kufumua kichwa chake bila kutoa sababu licha ya kuandika katika daftari la makabidhiano kuwa asisumbuliwe mtu yeyote.
Sinema ya askari aliyejiua msafara wa JK - Global Publishers
 
Kabinti kazuri na bado kabichi kabisa. Wamekauwa. Hata kama ni SMG, bado haiwezekani matundu yote matatu yakaingia kwa precion nzuri kiasi hicho. Angelianza ku-move na matundu yangelikuwa mengi.

Nina wasiwasi kuwa wamekauwa kwa kitu kingine na kukapiga risasi kuonyesha kuwa kamejiuwa.

RIP Suzzy. Damu hako kuna siku watailipa.
 
Kwa uelewa wangu, askari anayeongoza msafara huwa hana silaha. Sasa huyu dada alipata wapi silaha? Nafikiri kamanda wa polisi akianzia hapo kutoa maelezo tunaweza kupata picha. Kuna kila dalili ya jambo lililo jificha kwenye kifo hiki. RIP Suzan.
 
Sumaye alisema anaekuua kwa kalamu wakati huu wa kampeni, atakua kwa bunduki akipata madaraka, Vijana wa Kikwete wamemuua, wameeua kwa bunduki zilizonunulia kwa kodi za binti yule.......
pole familia ya yule mrembo, yule Polisi, yule dada.
 
Kwanza tumpe marehemu heshima anayostahili kwa kumuita jina lake kamili. Mbona IGP isjasikia akiitwa IGP Said? Hii ni kama vile wazungu walivyokuwa wakituita "boy" bila kujali umri wetu. Kutumia jina lake la kwanza ni uendelezaji wa dhana hiyo hiyo kuwa aliyechini yako hastahili kutambuliwa kama mtu kamilifu! Kama Susan ni ubini wake basi natanguliza samahani.

Amandla......
 
Kwanza tumpe marehemu heshima anayostahili kwa kumuita jina lake kamili. Mbona IGP isjasikia akiitwa IGP Said? Hii ni kama vile wazungu walivyokuwa wakituita "boy" bila kujali umri wetu. Kutumia jina lake la kwanza ni uendelezaji wa dhana hiyo hiyo kuwa aliyechini yako hastahili kutambuliwa kama mtu kamilifu! Kama Susan ni ubini wake basi natanguliza samahani.

Amandla......

Mkuu Fundi, kumuita mtu jina la kwanza ni kumdharau? Hii ya karne!!
 
Mkuu Fundi, kumuita mtu jina la kwanza ni kumdharau? Hii ya karne!!

Mzazi wako unaweza kumuita jina lake la kwanza? Aliyekuzidi madaraka unaweza kumuita jina lake la kwanza? Tunazungumzia context tuliyopo. Mbona tunazungumzia IGP Mwema na si IGP Said? Au Rais Kikwete na si Rais Jakaya? Katika hii habari, Mkuu wa Polisi ameitwa kwa jina lake lote, Sebastian Zakaria. Mganga Mkuu nae ameitwa jina lake lote, Dk. Charles Samson. Mbona huyu WP ananyimwa heshima hiyo? Hii ni institutionalised dharau! Na ni mitizamo kama hii ndiyo inayochangia kuwaona watu kama marehemu kuwa expendable! Hakuna atakaejali lolote likiwapata. Ndiyo maana hata hadithi waliyotoa kuhusu kifo chake inaonekana ya ovyo ovyo tu. Angekuwa mtu anayehishimiwa basi angalau hata hadithi ingepangwa inayoeleweka. Si kama hii.

Amandla......
 
Kabinti kazuri na bado kabichi kabisa. Wamekauwa. Hata kama ni SMG, bado haiwezekani matundu yote matatu yakaingia kwa precion nzuri kiasi hicho. Angelianza ku-move na matundu yangelikuwa mengi.

Nina wasiwasi kuwa wamekauwa kwa kitu kingine na kukapiga risasi kuonyesha kuwa kamejiuwa.

RIP Suzzy. Damu hako kuna siku watailipa.
Ulipaswa kujuwa kwamba SMG ni automatic carbine, kwa dakika moja inaweza kutema risasi zaidi ya 30 mkuu, uwezekano wa huyo askari kujiuwa ni mkubwa kutokana na msongo wa mawazo. Unaweza kujipiga risasi tano na tundu likwa moja tu. SMG inayo zungumziwa hapo ni ile inayojulikana kimataifa kama AK 47.
 
JESHI LA POLISI LATOA UFAFANUZI WA KIFO CHA PC SUZANA


Na Aron Msigwa – MAELEZO.

Jeshi la Polisi nchini limesema kifo cha askari Polisi WP.7338 PC Suzana kilichotokea katika kituo cha Polisi Tarime tarehe 4/7/2010 kilitokana na tukio la askari huyo kujipiga risasi kifuani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi Nchini ASP Advera Senso amesema askari huyo WP .7338 PC Suzana siku ya tukio hilo aliingia kazini asubuhi na baadaye kutakiwa kuelekea kwenye lindo kwa muda kuzuia magari yasiingilie msafara wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikuwa na ziara wilayani Tarime siku hiyo.
Amesema siku hiyo msafara wa rais ulipofika alipokuwa PC Suzana uligawanyika gari la RPC Mara liliacha njia ya msafara na kuingia barabara ya Bomani kwenda ofisi ya DC likifuatiwa na magari mengine matatu likiwemo la Rais.
ASP Senso amefafanua kuwa eneo ulipogawanyikia msafara kuna kilima na kona kali iliyosababisha RPC Mara kupotezana na magari yaliyokuwa mbele yake na hivyo kushindwa uelekeo wa msafara.

"Mara baada ya kuona amepotea RPC wa Mara alisimama alipokuwa PC Suzana na kutaka kujua kwa DC ni wapi, akawaonyesha njia ya mkato ambayo haikuwa rasmi iliyopangiwa msafara" amesema.

Amefafanua kuwa ilionekana PC Suzana alielewa kuwa RPC Mara alitaka kwenda Ofisi ya DC wakati yeye alitaka kuelewa njia ulipopita msafara. Baadaye RPC Tarime Rorya alimwagiza mkuu wa kituo Tarime apeleke askari mwingine eneo hilo na PC Suzana arudi kituoni umbali wa takribani mita 100 toka alipokuwa amepangiwa kazi.

Amesema PC Suzana alipofika chumba cha mashitaka aliendelea na kazi, baadaye kwa kushirikiana na askari mwenzake PC Dora waliaadaa makabidhiano ya zamu na wakati wakiendelea kuandaa ghafla PC Suzana alichukua silaha moja kati ya mbili zilizokuwa kwenye sanduku na kuingia kwenye ofisi ya mkuu wa kituo na kufunga mlango.

Amefafanua kuwa askari wengine waliokuwa kwenye chumba cha mashtaka walipoona hivyo walikwenda kwenye mlango alipoingilia PC Suzana na kujaribu kuuvunja ndipo akapiga risasi mlangoni na risasi hiyo kutoboa mlango kitendo kilichowafanya kurudi nyuma na baada ya muda walivunja mlango na kumkuta PC Suzana akiwa amejipiga risasi kifuani.

ASP Advera amesema Jeshi la Polisi limechukua hatua za kiutawala na kuboresha mwongozo wa namna ya kusimamia misafara kwenye mikoa ya kipolisi yenye makamanda zaidi ya mmoja chini ya mkuu wa mkoa mmoja, mafunzo kazini na vyuoni kuhusu namna ya kukabilianma na msongo (stress Management).
Hata hivyo amebainisha kuwa kifo cha WP Suzana ni suala linalohitaji uamuzi wa kisheria na jalada la tukio hilo limekamilishwa na kupelekwa ofisi ya wakili wa serikali kanda ya Ziwa kwa maamuzi ya kisheria.

Source: Michuzi blog

My take:

Yaleyale ya Zombe na wenzake, kufundishana cha kuongea. Hii taarifa inaonesha ni jinsi gani jeshi letu lilivyo butu na kutokuwa na uwezo wa kutumia logic katika kutengeneza report za kudanganyia umma.

Report hii imezidi kuzua maswali mengi zaidi kuliko kama wangekaa kimya tu kwani watanzania ni wepesi wa kusahau na suala hili walikuwa wameisha lisahau.


Haiingii akilini, mtu kuitwa kituoni na kuendelea na kazi nyingine bila kufanyiwa unyanyasaji, harrasment na utawala na baadae aishie kujitwanga risasi zaidi ya moja kwa kutumia SMG kifuani. Maswali waliyotakiwa kuyajibu ni:-

1. Baada ya kuitwa kituoni ofisi ya mashitaka nini kilifuata kati yake na uongozi wa polisi mkoani?

2. alipokimbilia ofisi ya mkuu wa kituo na kujifungia walisikia risasi ngapi?,

3. "Unaposema askari wengine walipotaka kuvunja mlango alipiga risasi mlangoni na kutoboa wakarudi nyuma na baadae kuvunja na kukuta amejipiga risasi kifuani"

Swali hapa ni je kipi kilianza kati ya kujipiga risasi kifuani au kupiga mlangoni, maana taarifa haioneshi baada ya kupiga risasi mlangoni walisikia risasi ingine ndani na huenda ndiyo iliyomuua, maana yake ni kwamba PC Suzana alikuwa na uwezo wa kupiga risasi mlangoni baada ya kujipiga kifuani risasi nne. HAPA KUNA MASWALI ZAIDI YA 150 YANATAKA UFAFANUZI.

3. Hawakusema wakati PC Suzan anaingia ofisi ya mkuu wa kituo wakati wa kukabidhiana yeye mkuu wa kituo alikuwa wapi?, na kama hakuwepo iweje ofisi yake iwe wazi?, na kama alikuwepo ndani alijificha wapi?

4. Mwisho wamemalizia na suala la "Stress Management", stress hiyo ilitokana na nini hasa?,

KWA TAARIFA HII YA KISANII ISIYOKUWA NA TAALUMA YA KIINTELIJENSIA NA COMMON SENSE, INAONESHA WAZI KUWA JESHI LA POLISI HALIKUSEMA UKWELI KWENYE HILI SUALA NA WALICHOJARIBU NI KU "COVER" WHAT REAL HAPPENED - KWA ULE USEMI WA MTU AMEISHAKUFA HATA UKWELI UKIJULIKANA HAITASAIDIA KITU, KWELI PC SUZAN AMEKUFA KIBUDU KWENYE HILI SUALA. SIJASHAWISHIKA NA KUAMINI KUWA ALIJIUA, KIFO CHAKE KIKO MIKONONI MWA MTU NA MTU HUYO ANALINDWA. ILA MUNGU NDIYO MTOA HAKI:
NDIYO MAANA WAMEMPATIA LOW PROFILE KUJA KUTOA UPUPU HAPA KWA KUHOFIA KINA MWEMA WATAJEOPARDIZE CREDIBILITY YAO KWA KUTOA MASOMO YA KICHEKECHEA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA

 
Back
Top Bottom