Nakwambia Umenikwaza na nimekwazika..

Feb 20, 2012
93
11
Habari ya jumapili ndugu zangu. Ni matumaini yangu kuwa kila mwanaJF kwa imani yake anaheshimu misingi ya maadili ya kiimani.
Leo mmenikwaza, nawaambia mmenikwaza mchungaji wenu. Kwani sio wewe? Basi mwambie rafiki/jirani yako amenikwaza na nimekwazika!
1. Umevaa mavazi yasiyo na "adabu" na kujipeleka kwenye nyumba ya Ibada(kanisani). Kwani umeambia hapo kuna maonesho ya mitindo ya mavazi?
2. Umechelewa ibada inayoanza saa tatu, kanisa lipo mtaa wa pili kutoka kwenu. Mbona kazini unaamka saa 10 alfajiri na unawahi? Tena bila adabu unajikwatua na viatu vyako "vinapiga makelele", unaenda kukaa viti vya mbele.
3. Unakaa back bench kanisani unaanza kuchat. Kwa nini usingebaki kwenu ili utanue kwa raha zako..
4. Unakaa jirani na shoga/rafiki yako mnaanza kunong'onezana! Mnaongea nini? Nakwambia umenikwaza wewe na huyo shoga/rafiki yako.
5.....
6.....
7.....
Tafadhali chukua hatua, badilika..
.....
Ndimi mchungaji wenu. Rev Fr KABOKA mchizi.
 
Kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa umetoa mia mbili wakati Jf inakuona wa maana na una hela nyingi mfukoni
 
Duh! Nilichelewa kweli leo. Naingia hivi, nakuta neno limeshasomwa mchungaji ndio anatoa mahubiri ila nilibana bench la nyuma. Pole sana baba mchungaji. Tutajirekebisha.
 
Kama umekasirika basi na wewe umeshatenda dhambi. Hii ni kwa mujibu wa Biblia.
 
Umeingia kanisani na suti yaani suruali na koti fupi vyote vyeupe ndani umevaa ch upi nyeupe unaonekana hata ilipopita lol.
 
Back
Top Bottom