Nakuwa mzito kuomba mchango wa harusi

Nakuwa mzito kuomba mchango wa harusi

Uislam raha sana, ulishaweka wazi, anaeoa, anaeolewa, wakili waake, mashahidi wawili, muozzeshaji. Mchezo kwisha. Wakimaliza unawapiga na vijisambusa. Kila mtu anasepa kwao. Ukitaka makuu ni wewe na ujinga wako tu.
Safi sana ,Sasa huku kwetu mambo ni mengi adi unaweza ukakopa Ili Tu harusi iwe nzuri
 
Habari za saa watanzania wenzangu,

Namshukuru Mungu Kwa kuzidi kuniongoza katika safari ya maisha ,Mimi ni kijana ninaye chukia sana kitu kinaitwa mchango wa harusi ,ni Bora niombe mchango wa matibabu lkn sio harusi,nilibahatika kupata kazi mwezi wa tano mwaka huu ,ila pia Kwa neema za Mungu pia nilibahatika kukutana na mwanamke niliye kuwa naishi naye tangu chuo na hatimaye akapata ujauzito pindi tu tulivyomaliza chuo,alitamani sana tufunge harusi,sikuwa na kipingamizi chochote,kwasababu pia nilikuwa nampenda .changamoto wazazi wake na baba mkubwa wake wanataka harusi ambayo kiuhalisia Mimi Sina uwezo huo wa kualika watu wengi ila nilikuwa nauwezo wa kualika wazazi wangu na wazazi wa mke wangu na mashaidi wachache sana bila kuomba mchango wowote ,inshort watu 10 tu ,ila sasa wazazi wangu hawataki harusi ya namba iyo wanataka kujulisha ndugu hasa mzee wangu anapenda sana sifa ,za kutaka Kila mtu uko kijijini ajue ,

Ninachoka sana nikiwaza hili ,ila Kwa bahati nzuri mzee ana marafiki ambao aliwachangia sana harusi ila awamu hii anataka ela zake zirudi ,nimejitoa na kukaa pembeni kisubiri tu iyo siku ifike ya harusi Kwa maana sielewi,nilipenda sana harusi iwe simple IL Sasa wazee wamekuwa wagumu kutaka kunielewa ,wao wanataka harusi ya umati mkubwa ndugu uko kijijini wajue[emoji51].

Ukweli ni kwamba nashindwa kuelewa huu utaratibu wa kuomba mchango wa harusi Kwa ndugu jamaa na marafiki ,nimekuwa na waza sana ni Kwa nini jamii imeweka huu utaratibu tangu zamani,nachoka Kwa hichi kipindi kuelekea kufunga harusi,siwezi kuomba naona ni utaratibu wa ajabu sana ,kusumbua watu eti kisa ninaoa.

Hapa wazazi wangu wanasema ni add watu Kwa group la wasap kuwajulisha naoa [emoji51] aisee nikiwaza sipati majibu nachoka akili,na wazazi na ndugu wa huyu mke wangu wanapenda harusi kupita maelezo,
Siku si nyingi wazazi wanawatambulisha home wakwe na ndugu wa huyu mke wangu ,hapa wazazi wanapanga debe za mbege walizo ambiwa na hao wazee wa huyo mke wangu na wao pia wanachoka ila ki ukweli pia wazazi wangu wanapenda sifa za kutaka kuonekana wanafanya harusi Kwa ajili ya mtoto wao.

Naomba Ushauri wenu wadau.
Rafiki kipindi nataka kuoa nilikua na akili na mawazo kama yako ila nilijifunza kitu. Ww unaweza tamani ndoa ya watu kumi au wasizidi 50 lakini ukumbuke mkeo unaemuoa naye anamatamanio yake. Mm nilipiga hesabu mwishoe nikajikuta naandaa sherehe ya watu 80-120. Cha msingi jipange alika watu angalau 80 ili sherehe inoge na itakua bomba zaidi kama hutawachangisha michango skuhizi sherehe za michango ndio zinaongoza kwa kuwa mbovu kamati inamichezo michafu sana.

Nakumbuka nilishachangia 100k double hio nikaenda na wife kwenye sherehe imagine kinywaji tena soda na grandmalta unafanya kuziomba wakati umechangia yaani toka siku ile nikasema sichangii sherehe na kama wife kachangia ataenda mwenyewe aibu na fedheha siwezi na yote hio ni kamati ndio inasababisha kwakua ni walafi. Cha msingi kusanya hata upate 6m unafanya kasherehe kako kadogo watu wanaenjoy
 
Yaani ntahakikisha nafanya siri nikiwa nna cash zangu ndio ntatangaza ndoa sitaki mchango wa yeyote
Kaka iyo ni plan nzuri sana ila Sasa utakutana na wazee wa Mila na deaturi Wana Fanya mambo kuwa magumu hasa uku uchagani..utajikuta unaingia gharama kubwa zaidi adi utachanganyikiwa ..
 
Juzi kati rafiki yangu kaoa.
Ni kijana mdogo tu.
Ilikua harusi ya kifahari to be honest (mwakilishi wangu ndo aliniambia).
Kijana yule hakupitisha mchango, alichofanya aliandika meseji moja nzuri sana yenye maneno machache lakini powerful. Ndani ya hyo text, alisema kua amefika wakati wa kuoa na kama itakupendeza muunge mkono.
Hakuna mambo ya group na majina mengi wala kiwango.
Mimi nilichanga 50k, (ndo kiwango changu kwa marafiki wa karibu ambao sio wamenitafta bkoz wanaoa).
Nkatumiwa kadi ya kielektroniki ya double.
All in all, usiombe michango kama watu wengine na mambo ya kuandikana majina kuoneshana nani katoa nini.
Harusi ni yako, so wale close friends watumie ujumbe, usiwasumbue. At least once per month tuma same ujumbe, mtu atakachotoa shukuru ishi nacho.
Panga plan yako then hao wanaotaka kumuona gara bii kwa ajili ya masifa ndo wakahangaike na michango ya kijinga.
Ndoa ni wewe na mke wako, wasikupe mapresha ya kiboya.
 
Wazee wa Mila na desturi wanafanya mambo kuwa magumu Kwa vijana wanapo taka kuoa ,mara leta debe ishirini za mbege mara kitenge Cha shangazi ,mara blanketi la babu[emoji3][emoji3]utazani Babu alikuwa analalia majani..
 
Wale uspate shida, wewe washirìkishe wazazi unachotaka na bajeti uliyonayo.Mwambie mzee atafute watu na kufanya fundraising.Aalike marafiki zake akae nao apike chakula halafu awashirikishe kwenye kutafuta kamati ndogo ya harusi yako.Kamati hiyo ndio ichague mtu kwa niaba yako atakayefanikisha harusi yako.Huitaji kujiumiza wakati wazazi wapo kukusapoti.
 
Juzi kati rafiki yangu kaoa.
Ni kijana mdogo tu.
Ilikua harusi ya kifahari to be honest (mwakilishi wangu ndo aliniambia).
Kijana yule hakupitisha mchango, alichofanya aliandika meseji moja nzuri sana yenye maneno machache lakini powerful. Ndani ya hyo text, alisema kua amefika wakati wa kuoa na kama itakupendeza muunge mkono.
Hakuna mambo ya group na majina mengi wala kiwango.
Mimi nilichanga 50k, (ndo kiwango changu kwa marafiki wa karibu ambao sio wamenitafta bkoz wanaoa).
Nkatumiwa kadi ya kielektroniki ya double.
All in all, usiombe michango kama watu wengine na mambo ya kuandikana majina kuoneshana nani katoa nini.
Harusi ni yako, so wale close friends watumie ujumbe, usiwasumbue. At least once per month tuma same ujumbe, mtu atakachotoa shukuru ishi nacho.
Panga plan yako then hao wanaotaka kumuona gara bii kwa ajili ya masifa ndo wakahangaike na michango ya kijinga.
Ndoa ni wewe na mke wako, wasikupe mapresha ya kiboya.
Hongera Kwake huyo kijana,Vijana tunapenda kuoa mapema ila Sasa wazee wa Mila na desturi wanaweka vikwazo vingi sana,
Saiv system ya ku add watu wasap ni ya ajabu sana watu hawapendi ni usumbufu kama huna ukaribu na watu vizuri..
 
Nyumbani kwa wazee ilikuwa unakuta mikadi mpaka ishirini ipo ina hitaji michango nikawa najisemea ndio us#%#£ gani huu nilikuwa nachukia kinoma [emoji3]
Wazee wangu wamechangia sana ila naona wanataka na wao ela Yao irudi ,Kwa kijana wa wa kwanza .ila Mimi napata wakati mgumu kuweza kuamua kuhusu harusi yangu hawataki nisikiliza kabisa.
 
Back
Top Bottom