Wanakwambia mtt wa kwanza haiwezi kupita hivi hivi 😄Wazee wangu wamechangia sana ila naona wanataka na wao ela Yao irudi ,Kwa kijana wa wa kwanza .ila Mimi napata wakati mgumu kuweza kuamua kuhusu harusi yangu hawataki nisikiliza kabisa.
WEwe kama mimi, sipendi kuchangisha ila za wengine nawachangiaHabari za saa watanzania wenzangu,
Namshukuru Mungu Kwa kuzidi kuniongoza katika safari ya maisha ,Mimi ni kijana ninaye chukia sana kitu kinaitwa mchango wa harusi ,ni Bora niombe mchango wa matibabu lkn sio harusi,nilibahatika kupata kazi mwezi wa tano mwaka huu ,ila pia Kwa neema za Mungu pia nilibahatika kukutana na mwanamke niliye kuwa naishi naye tangu chuo na hatimaye akapata ujauzito pindi tu tulivyomaliza chuo,alitamani sana tufunge harusi,sikuwa na kipingamizi chochote,kwasababu pia nilikuwa nampenda .changamoto wazazi wake na baba mkubwa wake wanataka harusi ambayo kiuhalisia Mimi Sina uwezo huo wa kualika watu wengi ila nilikuwa nauwezo wa kualika wazazi wangu na wazazi wa mke wangu na mashaidi wachache sana bila kuomba mchango wowote ,inshort watu 10 tu ,ila sasa wazazi wangu hawataki harusi ya namba iyo wanataka kujulisha ndugu hasa mzee wangu anapenda sana sifa ,za kutaka Kila mtu uko kijijini ajue ,
Ninachoka sana nikiwaza hili ,ila Kwa bahati nzuri mzee ana marafiki ambao aliwachangia sana harusi ila awamu hii anataka ela zake zirudi ,nimejitoa na kukaa pembeni kisubiri tu iyo siku ifike ya harusi Kwa maana sielewi,nilipenda sana harusi iwe simple IL Sasa wazee wamekuwa wagumu kutaka kunielewa ,wao wanataka harusi ya umati mkubwa ndugu uko kijijini wajue[emoji51].
Ukweli ni kwamba nashindwa kuelewa huu utaratibu wa kuomba mchango wa harusi Kwa ndugu jamaa na marafiki ,nimekuwa na waza sana ni Kwa nini jamii imeweka huu utaratibu tangu zamani,nachoka Kwa hichi kipindi kuelekea kufunga harusi,siwezi kuomba naona ni utaratibu wa ajabu sana ,kusumbua watu eti kisa ninaoa.
Hapa wazazi wangu wanasema ni add watu Kwa group la wasap kuwajulisha naoa [emoji51] aisee nikiwaza sipati majibu nachoka akili,na wazazi na ndugu wa huyu mke wangu wanapenda harusi kupita maelezo,
Siku si nyingi wazazi wanawatambulisha home wakwe na ndugu wa huyu mke wangu ,hapa wazazi wanapanga debe za mbege walizo ambiwa na hao wazee wa huyo mke wangu na wao pia wanachoka ila ki ukweli pia wazazi wangu wanapenda sifa za kutaka kuonekana wanafanya harusi Kwa ajili ya mtoto wao.
Naomba Ushauri wenu wadau.
🤣🤣🤣Michango ni kujiaibisha ,michango ni utapeli ,michango Haina maana .
"Asante sana Mungu akubariki"kuchangisha watu ni ujinga flani lazima uanze kujinyenyekeza KWA watu na kujenereti tabia ambazo huna.
Apo upate pande zote mbili zinaufahamu mzuri kuhusu uislamu,ndoa itafungwa kwa wepesi sana….vinginevyo ni vurugu mechiUislam raha sana, ulishaweka wazi, anaeoa, anaeolewa, wakili wake, mashahidi wawili, muozeshaji. Mchezo kwisha. Wakimaliza unawapiga na vijisambusa. Kila mtu anasepa kwao. Ukitaka makuu ni wewe na ujinga wako tu.
Upo kama Mimi ,aisee sipende umati hasa sherehe ila unakuta uyu mwanamke ndiyo mambo yake ,adi nachoka ..mara aposti Niko nae mara anataka nifanye bethi day aite watu [emoji51][emoji51] arhggg ,inakera sanaWanakwambia mtt wa kwanza haiwezi kupita hivi hivi [emoji1]
Ila mimi wananijua sipendi masherehe masherehe kwanza naona hakuna jipya
Mimi napenda starehe na watu wachache ninao wajuaUpo kama Mimi ,aisee sipende umati hasa sherehe ila unakuta uyu mwanamke ndiyo mambo yake ,adi nachoka ..mara aposti Niko nae mara anataka nifanye bethi day aite watu [emoji51][emoji51] arhggg ,inakera sana
Wezee wamejipanga kuja kulewa na kuondoka na chupa eti mtu hataki sherehe [emoji3][emoji3] hapo ni ugomvi bomu la heroshima ..Apo upate pande zote mbili zinaufahamu mzuri kuhusu uislamu,ndoa itafungwa kwa wepesi sana….vinginevyo ni vurugu mechi
Good IdeaJuzi kati rafiki yangu kaoa.
Ni kijana mdogo tu.
Ilikua harusi ya kifahari to be honest (mwakilishi wangu ndo aliniambia).
Kijana yule hakupitisha mchango, alichofanya aliandika meseji moja nzuri sana yenye maneno machache lakini powerful. Ndani ya hyo text, alisema kua amefika wakati wa kuoa na kama itakupendeza muunge mkono.
Hakuna mambo ya group na majina mengi wala kiwango.
Mimi nilichanga 50k, (ndo kiwango changu kwa marafiki wa karibu ambao sio wamenitafta bkoz wanaoa).
Nkatumiwa kadi ya kielektroniki ya double.
All in all, usiombe michango kama watu wengine na mambo ya kuandikana majina kuoneshana nani katoa nini.
Harusi ni yako, so wale close friends watumie ujumbe, usiwasumbue. At least once per month tuma same ujumbe, mtu atakachotoa shukuru ishi nacho.
Panga plan yako then hao wanaotaka kumuona gara bii kwa ajili ya masifa ndo wakahangaike na michango ya kijinga.
Ndoa ni wewe na mke wako, wasikupe mapresha ya kiboya.
Nimeshakutana na hao watu 😆Sasa mkuu unakuta una force kupeleka kadi Kwa mtu Hata hujawahi kuwa na stori naye..ata kama mnakaa ofic Moja..
[emoji23][emoji23] nimecheka sanaa..na unakuta anafuatilia adi ahakikishe umechangia [emoji23][emoji23]Nimeshakutana na hao watu [emoji38]
Mtu anampa kadi rafiki yake anakuona umekaa pembeni na wewe anakutandika kadi [emoji1] nabaki najiuliza huyu mtu kichwa chake kinafanya kazi sawasawa kweli [emoji1]
Uislamu naupenda San kwenye hili eneo la ndoa na msiba hkn kupotezaa Muda on the spot unaolewaaUislam raha sana, ulishaweka wazi, anaeoa, anaeolewa, wakili wake, mashahidi wawili, muozeshaji. Mchezo kwisha. Wakimaliza unawapiga na vijisambusa. Kila mtu anasepa kwao. Ukitaka makuu ni wewe na ujinga wako tu.
Huyu atakushauri ushauri usio tekelezeka be care fullRobert Heriel Mtibeli njoo uku kaka..Ushauri wako tafadhali..
[emoji3] Sasa hapo unawaza nini..,hapo utakunywa na kula adi ukimbie iyo harusi mwenyewe..,shida ni kuomba ndiyo inakuwa ngumu aiseeeM. Nina mdg angu anaoa ila nimeshindwa kuwaeleza marafiki zangu nimetulia tu ifike siku tule wali
So far Kam familia tu tumepata milion 8 ,Bado michnago ya wajomba na marafiki nearly itatika 20 kwa mtazmo wangu SAS mm najiuukiza nwezaje kiwambia marafiki
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Akishageuza kichogo tu mimi huku 🚮[emoji23][emoji23] nimecheka sanaa..na unakuta anafuatilia adi ahakikishe umechangia [emoji23][emoji23]