Nakuwa mzito kuomba mchango wa harusi

Vicenza

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
973
1,467
Habari za saa watanzania wenzangu,

Namshukuru Mungu Kwa kuzidi kuniongoza katika safari ya maisha ,Mimi ni kijana ninaye chukia sana kitu kinaitwa mchango wa harusi ,ni Bora niombe mchango wa matibabu lkn sio harusi,nilibahatika kupata kazi mwezi wa tano mwaka huu ,ila pia Kwa neema za Mungu pia nilibahatika kukutana na mwanamke niliye kuwa naishi naye tangu chuo na hatimaye akapata ujauzito pindi tu tulivyomaliza chuo,alitamani sana tufunge harusi,sikuwa na kipingamizi chochote,kwasababu pia nilikuwa nampenda .changamoto wazazi wake na baba mkubwa wake wanataka harusi ambayo kiuhalisia Mimi Sina uwezo huo wa kualika watu wengi ila nilikuwa nauwezo wa kualika wazazi wangu na wazazi wa mke wangu na mashaidi wachache sana bila kuomba mchango wowote ,inshort watu 10 tu ,ila sasa wazazi wangu hawataki harusi ya namba iyo wanataka kujulisha ndugu hasa mzee wangu anapenda sana sifa ,za kutaka Kila mtu uko kijijini ajue ,

Ninachoka sana nikiwaza hili ,ila Kwa bahati nzuri mzee ana marafiki ambao aliwachangia sana harusi ila awamu hii anataka ela zake zirudi ,nimejitoa na kukaa pembeni kisubiri tu iyo siku ifike ya harusi Kwa maana sielewi,nilipenda sana harusi iwe simple IL Sasa wazee wamekuwa wagumu kutaka kunielewa ,wao wanataka harusi ya umati mkubwa ndugu uko kijijini wajue.

Ukweli ni kwamba nashindwa kuelewa huu utaratibu wa kuomba mchango wa harusi Kwa ndugu jamaa na marafiki ,nimekuwa na waza sana ni Kwa nini jamii imeweka huu utaratibu tangu zamani,nachoka Kwa hichi kipindi kuelekea kufunga harusi,siwezi kuomba naona ni utaratibu wa ajabu sana ,kusumbua watu eti kisa ninaoa.

Hapa wazazi wangu wanasema ni add watu Kwa group la wasap kuwajulisha naoa aisee nikiwaza sipati majibu nachoka akili,na wazazi na ndugu wa huyu mke wangu wanapenda harusi kupita maelezo,
Siku si nyingi wazazi wanawatambulisha home wakwe na ndugu wa huyu mke wangu ,hapa wazazi wanapanga debe za mbege walizo ambiwa na hao wazee wa huyo mke wangu na wao pia wanachoka ila ki ukweli pia wazazi wangu wanapenda sifa za kutaka kuonekana wanafanya harusi Kwa ajili ya mtoto wao.

Naomba Ushauri wenu wadau.
 
kwani ww ulikuwa unataka nini.? ukachangishe.!?

Ok fanya hivi ‘’Huna moyo wa kuchangia wala wa kuchangisha’’ waeleze wazazi sherehe wakufanyie wao kwa gharama zao.
Ninamoyo wa kuchangia ila Sina moyo wa kuomba ..mchango
 
kuoa/kuolewa anafanya mwengine mchango nimchangie mimi utasema kuna kitu nafaidi nikishachanga kumbe kama si kwenda ukumbini na kula hakuna cha maana sana sana bado ntaingia gharama za kujitaftia outfit bado niende salun huku nimetoa mchango
 
Naitaji Mimi kama Mimi ndiyo nitumie gharama zangu kufanya harusi ,michango sitaki,
Nilikuwa na mawazo kama yako kumbe kuchangisha watu siyo kwamba Huna hela ya harusi bali ni kutambua uwepo wao. Andaa kadi weka hata kiwango kidogo cha kuchangiwa. Binadamu usipochangisha na kuwaalika waje kula inaonekana kama dharau hiyo harusi yako watahudhiria watoto tu.
 
Back
Top Bottom