Nakusudia kuishtaki Serikali (TCRA) kuzima Simcard za wateja wa mitandao

Rais hajasema mkajisajili nida kasema tusajiri laini zetu, na vigezo viko wazi, msimlishe maneno, nayeye pale chato akisajiri line yake ya Airtel hakujiandikisha nida
Sasa nani awezaye kupindua sheria
 
Mbona kama vile unajinyaga mwenyeww pale juu umesema sheria inasema driving licence inafaa, hapa unasema kama tumetumia driving licence tukajipange NIDA.
Mkuu embu fafanua kidogo hapo kwa national Id ni ipi yaani?
Samahani nimeghafirika tu mafuta kauli driving licence inakubaliks kisheria
 
Msiwashitue wakuu maana nimewapania sana.
Tutawashtaki kwa kutusababishia hasara ya mamilioni ya fedha.
 
Hakuna laini itakayofungiwa. Mnatishwa kiboya na nyie mnatishika. Sijasajili na sina mpango na kitambulissho ninacho
 
eddy, Mjomba mimi mwezi wa 12 mwaka jana nilienda ofisi za tigo , kununuwa line ya tigo na kisha kutaka kujisajili. Niliambiwa kujisali ni lazima niwe na namba zangu za nida! Nikawaambiwa kuwa mm bado sijapata hizo namba wala hicho kitambulisho, ila niliwaambia kuwa nina driving license! Lkn waligoma katakata kunisajili kwa kutumia driving license.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mjomba mimi mwezi wa 12 mwaka jana nilienda ofisi za tigo , kununuwa line ya tigo na kisha kutaka kujisajili. Niliambiwa kujisali ni lazima niwe na namba zangu za nida! Nikawaambiwa kuwa mm bado sijapata hizo namba wala hicho kitambulisho, ila niliwaambia kuwa nina driving license! Lkn waligoma katakata kunisajili kwa kutumia driving license.

Sent using Jamii Forums mobile app
Makampuni ya simu yametengeneza kero ya makusudi ili kukwepa rungu la tcra wamewasajilia watu simu kwa kutumia kitambulisho Cha mpiga Kura kinyume na sheria hivyo wamewageuza nida human shields na scape goat
 
Kila la kheri mkuu katika kesi mhimu Kama Ile natamani kuja nchini ili niongeze kikosi Cha timu Kazi. Maana si kwa upuuzi huu unaotaka kufanywa tarehe 20.
 
Unaweza kujiuliza maswali 200,na usipate jibu hata moja juu ya taifa la Tanzania hasa watu wake.

Hivi hawa ni Binadamu kutoka sayari hii ya Dunia au ni viumbe kutoka Planet X?

Binadamu aliyekamilika ni lazima awe na kumbukumbu za kutosha juu ya kila Tukio analopitia.

Tanzania hii hakuna tena anayekumbuka juu ya vitambulisho vya kupigia kura na Driving Licence kuwa vyote vina mfumo wa Biometric (unaohifadhi alama za vidole).

95% ya Watanzania wana vitambulisho vya kupigia kura vyenye mfumo wa Biometric sawa tu na Vitambulisho vya Taifa, lakini leo hii eti hivyo Vitambulisho havitakiwi kusajilia line za simu hadi viwe Vitambulisho vya Taifa.

Eti lengo ni kudhibiti uhalifu, sasa binadamu mmoja ana fingerprints ngapi kama ID za kura ambazo pia zilipatikana kama Vitambulisho vya Taifa kwa njia hiyo hiyo ya alama za vidole leo tena havifai?

Wenye akili wameshasoma mchezo, kuna kitu kinatafutwa hapo, kwa sababu fingerprints tayari watu walishachukuliwa kwenye Vitambulisho vya kura na Driving Licence, sasa kuna haja gani ya kutesa watu kiasi hiki?

Details za kila raia na fingerprints zake zipo Tayari kupitia Vitambulisho vya kura. Taifa lenye mamilioni ya wajinga wamesahau kuwa information zao zilishachukuliwa na fingerprints pia.

Neno la Mungu katika Kitabu cha Mithali linasema "Mwanangu mtafute sana Elimu na wala Usimwache aende zake”.

Poleni Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika kwenye mada yako;
''Wenye akili wameshasoma mchezo, kuna kitu kinatafutwa hapo, kwa sababu fingerprints Tayari watu walishachukuliwa kwenye Vitambulisho vya kura na Driving Licence,sasa kuna haja gani ya kutesa watu kiasi hiki?''.

Ni kitu gani kinachotafutwa? Naomba unielimishe!

Nimekuomba unielimishe kwa sababu kwa sasa hapa Jamiiforums kumejitokeza baadhi ya wanachama ambao wanadhani hisia zao ndio ukweli lakini kibaya zaidi wanataka kuwalazimisha na watu wengine kwa hoja za nguvu waamini hisia zao!
 
Wewe nawe msahaulifu mkubwa zaidi.
Umesahau wakati wa vitambulisho vya mpiga kura au leseni ya udereva hakukuwa na uhakiki/usahili wa idara ya uhamiaji kujiridhisha uraia wa muombaji.
Umesahau ktk vitambulisho vya kura hakukuwa na uwasilishaji cheti cha kuzaliwa.

Umesahau passport za zamani ilikuwa sio lazima upeleke cheti cha kuzaliwa, kuna waliopeleka affidavit tu ambazo ni rahisi kughushi(forge), unaenda na mtu yeyote mahakamani au kwa mwanasheria unasema alikuwepo nilipozaliwa kisha unalipia stamp duty haifiki mwekundu wa msimbazi mmoja au balimi 5.

Umesahau wakati wa vitambulisho vya wapiga kura haikuwa lazima kutambuliwa nambari ya nyumba au kitalu kwa wakazi wa mijini ambako wageni ni wengi.

#Ujuaji mwingi mbele giza.
#Waacheni wenye wajibu na taaluma zao wafanye kazi zao kitaalamu, sio kila kitu siasa.
 
Kama yalitaka mkojo Wa lissu haya mamtuchato siyaamini kuyaachia Alana za vidole vyangu.ningekuwa najua ile sheria ya takwimu inawapa mamlaka kampuni za simu kutoa taarifa za marangapi nimefanya uhalifu Wa mtandao na Mimi ningeomba nisajili kampuni ya simu
 
Wewe nawe msahaulifu mkubwa zaidi.
Umesahau wakati wa vitambulisho vya mpiga kura au leseni ya udereva hakukuwa na uhakiki/usahili wa idara ya uhamiaji kujiridhisha uraia wa muombaji.
Umesahau ktk vitambulisho vya kura hakukuwa na uwasilishaji cheti cha kuzaliwa.

Umeasahau passport za zamani ilikuwa sio lazima upeleke cheti cha kuzaliwa, kuna waliopeleka affidavit tu ambazo ni rahisi kughushi(forge), unaenda na mtu yeyote mahakamani au kwa mwanasheria unasema alikuwepo nilipozaliwa kisha unalipia stamp duty haifiki mwekundu wa msimbazi mmoja au balimi 5.
Umesahau wakati wa vitambulisho vya wapiga kura haikuwa lazima kutambuliwa nambari ya nyumba au kitalu kwa wakazi wa mijini ambako wageni ni wengi.

#Ujuaji mwingi mbele giza.
#Waacheni wenye wajibu na taaluma zao wafanye kazi zao kitaalamu, sio kila kitu siasa.
Naunga mkono hoja
P
 
ILA WABONGO WABISHI😂😂😂😂😂

MUDA ULIONGEZWA, RAIS YEYE MWENYEWE ALITUMIA KIDOLE KUSAJILI ILI KUWAHAMASISHA WATU LAKINI HAIKUSAIDIA KUTU🤦🤦🤦🤦🤣

WALA KELELE ZA MUDA HAUTOSHI HAZIKUTOLEWA, MUDA UMEFIKA WA UTEKELEZAJI KELELE ZINAPIGWA KILA KONA🤦🤦🤦🤦😄


Shikamooni wakubwa😂🤸🤸🤸
 
Back
Top Bottom