Nakupenda lakini umechelewa

Nakupenda lakini umechelewa

Kama alikuwa anampenda kweli angevumilia coz bidada si alikuwa anaendelea washawishi wazazi wake na at the same time anawasiliana na jamaa
Mwaka na miezi 3 ni muda mchache huo bidada?
 
dada alikuwa mtumzimakuamua aolewe na nani na awe dini gani....tatizo watu kushupalia wakiamini wao ndio wanajuaimani zaidi.....mambo ya dini tuyaache tu ila kama wlipendana angeolewa tu walimbanmia bure...hao waliombania wao wana ndoa zao...sasa baadae eti amekubaki...kile walichogoma mwanzo ndio wamekiachia....sasa ndio nini....KWELI HAPO ITS TOO LATE
 
yaani nakuhakikishia kutoka ndani ya moyo wangu sijawahi kupenda kama nilivyompenda yeye, ila kilichotokea ni hasira kwa sababu waliongea mbaya sana juu ya ukristo wangu
POLE SANA MI NAELEWA SANA HALI YAKO ILIVOONEKANA...YANI UNAONEKANA MUOVU SANA MBELE YA HAO WA IMANI KALI...TENA MAMA NA HUYO BINTI HAWAKUWA NA TATIZO....ANYWAY MUNGU NDIE ANAJUA SISI TUNABEBA DINI T EXTREME KIASI TUNAONA WATU HAWANA HAKI YA KUOA AU KUOLEWA
 
Huu mzimu wa udini unaendelea kuutafuna uzao wa Adam kutoka kizazi hadi kuzazi.
Katikati ya miaka ya tisini kuna bwana mmoja wa karibu sana alikumbwa na hii gharika ya udini. Bwana huyu alikuwa mkazi wa kibaha vijijini kwa sasa ameshatangulia mbele za haki alitengwa na familia ya ukweni kwake kisa kuoa binti wa kiislamu wakati yeye ni mkristo.
Bwana huyu awali alikuwa mwislam safi ila alibadilisha dini baada ya kupigwa injili.
Sasa kwenye harakati za kuoa akajikuta anaangukia kwenye penzi la binti wa kiislam tena baba yake ni sheikh mwenye itikadi kali.
Kimbembe kikaja muda wa kuchumbia, baba akagoma katakata bintiye kuolewa na kafiri kama wanavyowaita.
Binti naye akawa amedata kwa mnyamwezi. Akatoa msimamo wake kuwa yupo tayari kwa lolote hata kubadilisha dini lakini lazima aolewe na jamaa. Mzee nae kagoma.
Binti akaondoka nyumbani kwa nguvu na kwenda kuishi kwa jamaa. Mzee alivyoona binti kashindikana, nae akatangaza jihad, akamkana bintiye, kuanzia leo wewe sio mwanangu, usinijue nisikujue iwe kwa shida ama kwa kheri, usikanyage kwangu na sitokanyaga nyumbani kwako. Nikifa usije kwenye mazishi yangu na wewe kadhalka.
Binti akasema poa, yote kheri na iwe hivyo. Akaenda kwa jamaa na akawa anatimba church kama kawaida. Maisha yakaendelea mwaka 95 akabeba mimba ya kwanza akajifungua fresh.
Mwaka 98 akabeba mimba ya pili lakini wakati wa kujifungua bahati mbaya akakumbwa na mauti lakini mtoto akazaliwa mzima.
Yule mzee alifanya kama alivyo ahidi kwenye maneno yake. Bwana yule akasusiwa msiba na hakuna aliyeshiriki mazishi kutoka ukweni kwake. Aliyafanya yeye na wapendwa wenzie kutoka kanisani. Inasikitisha sana kwakweli.
Kwahiyo mimi naona ulifanya vyema kuangalia ustarabu wako kuliko kukutwa na kama ya huyu bwana. Ni kheri nusu shari kuliko shari kamili.
kwa hiyo huyo mzee alivosusia mazisho ndio anapata thawabu au...? mis use tu of dini..hapo kip[engele cha UPENDO kwakw kakiacha...anyway kazikwa na wapendwa so hakuna tofauti.....mbele za haki tutawajibishwa wote
 
dada alikuwa mtumzimakuamua aolewe na nani na awe dini gani....tatizo watu kushupalia wakiamini wao ndio wanajuaimani zaidi.....mambo ya dini tuyaache tu ila kama wlipendana angeolewa tu walimbanmia bure...hao waliombania wao wana ndoa zao...sasa baadae eti amekubaki...kile walichogoma mwanzo ndio wamekiachia....sasa ndio nini....KWELI HAPO ITS TOO LATE
ni hakika mkuu
 
Dharau zako zimechangia.Wazazi wanamjua mtu yukoje.Kwa mfano hapa tu umetaja kabila "Wamakonde wale"...tabia ni kama ngozi.
Issue siyo dini hapo.
 
Back
Top Bottom