Nakupenda lakini umechelewa

Nakupenda lakini umechelewa

kwa jinsi ninavyochat nae anaonekana yupo kwenye kipindi kigumu sana
Lazima, huenda muda ulipokuwa kimya alikuwa akiwashawishi wazaziwe...

Au kila mchumba alipojitokeza alikuwa akimtakaa kuweka shinikizo kwa wazaziwe...

Sasa kosa la wajombaze haliwezi kusashihika tena, na hapo ndipo kichwa chaweza mpasuka kwa mawazo...

Anyway, it's what it's...
 
nashukuru kwa ushauri lakini malaya na walevi hata huko kwetu wapo, nenda katembelee,uwanja wa fisi,kimboka, dar live,ambiance, kangaroo, samakisamaki, ohio, itigi, kahumba, vibers, kilimani, 84 etc halafu niletee mrejesho kuna wazulu wangapi humo
Ha ha..mbona unalinganisha visivyo,....au bado upo na stress?, nimezaaa na wazulu wawili tofauti..hivyo nawajua vyema...kila la kheri mkuu.
 
Hukumpenda wewe na unaendekeza tamaa! Si ungevuta vuta mda kwanza usikilizie!

Papuchi mpya ushasahau kila kitu, asee mwanaume sio babaako kweli!
yaani nakuhakikishia kutoka ndani ya moyo wangu sijawahi kupenda kama nilivyompenda yeye, ila kilichotokea ni hasira kwa sababu waliongea mbaya sana juu ya ukristo wangu
 
Siku hizi watu wanakutania mitandaoni, wanaanzisha mahusiano mitandaoni na kuachana wanapeana taarifa mitandaoni.

Heko mitandao ya kijamii.
hapana mkuu huyu hata pesa yangu ameitumia yaani nilikuwa namsaidia hata pesa ya ada ni mtu tunaefahamiana a-z
 
Mi nilikua wewe wakike mana ndo majibu yao, anyway kma bahati yake ipo atapata tu. Mana huenda ww si wakwanza kwake pia
 
Hukumpenda wewe na unaendekeza tamaa! Si ungevuta vuta mda kwanza usikilizie!

Papuchi mpya ushasahau kila kitu, asee mwanaume sio babaako kweli!
Kwa hiyo angekaa mwaka mzima ana mbwelambwela tu...
 
Nisiwachoshe wakuu,
Ipo hivi wakati naishi hapo Dar kabla sijaja huku kwa madiba kutafuta maisha nilikuwa na mpenzi, na tulipendana sana na tulikuwa na mipango mingi sana ya kuja kuishi pamoja na kuanzisha familia, na hata baada ya kuondoka hapo mawasiliano yalikuwepo tena sana ilikuwa haipiti siku hatujawasiliana, na mwaka juzi mwezi wa 11 nilimtafutia pasport na alikuja huku na alikaa miezi 2 kisha tukapanga safari ya kurudi bongoland ili nikatoe barua na kutambulishwa ukweni,

Kabla sijaendelea huyu mwenzangu yeye alikuwa ni muislamu na mimi ni mkristo, baada ya kufika hapa home baada kama ya siku tatu mipango ikapangwa barua ikapelekwa ikapokelewa, siku ya tatu mshenga akaitwa akachukue majibu baada ya kufika pale tukakubaliwa vizuri tu,

utata ukaja kwenye dini maana mimi na huyu binti tulikubaliana yeye ndo atabadili dini anifuate mimi, lakini pale wajomba zake wakataka mimi ndo niwe muislamu walivutana sana maana mama yake alikuwa radhi bintiye abadili dini lakini baba na wajomba walikataa, mwisho wa picha mimi ikashindikana,

Binti alilia sana lakini wamakonde wale yaani wajomba zake hawakutaka kumwelewa, na wakasema kuanzia saa ile uhusiano mimi ni binti yao ufe maana hawakujua kama mwanaume mwenyewe ni kafiri kwani wanaume wa imani yake wako wengi na kama kuolewa ataolewa tuna muislamu mwenzake, mimi nilikubali kishingo upande na kuondoka bongo,

kutokana stress nilizokuwa nazo baada ya kufika hapa nikatafuta mwanamke wa kizulu ili niondowe stress,

Sasa mwezi huu yeye ananiambia mama yake amejadiliana na baba yake wamekubaliana kwamba abadili dini awe mkristo ili tuowane,

mimi sijamjibu maana najua yeye yupo humu jamii forum kama atauwona huu uzi namwambia amechelewa kwani nina mwanamke na ni mjamzito mwezi wa 3 nategemea kuitwa baba, nampenda lakini sina jinsi its to late.


Ee bwana kichaa msafi hongera sana kwa kuoa mzulu, nawamind sana mademu wao. Naomba unitafutie contact za Pumza Fihlani, kale kademu nakazimia ile mbaya na kako very bright ile mbaya si kama hawa dada zetu wanaohisi kupost picha za vichupi Ista na facebook ndo umaarufu ama uzuri. Yaani nimewachoka.
 
Back
Top Bottom