Nakupenda lakini umechelewa

Kichaa Msafi

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
1,087
2,133
Nisiwachoshe wakuu,
Ipo hivi wakati naishi hapo Dar kabla sijaja huku kwa madiba kutafuta maisha nilikuwa na mpenzi, na tulipendana sana na tulikuwa na mipango mingi sana ya kuja kuishi pamoja na kuanzisha familia, na hata baada ya kuondoka hapo mawasiliano yalikuwepo tena sana ilikuwa haipiti siku hatujawasiliana, na mwaka juzi mwezi wa 11 nilimtafutia pasport na alikuja huku na alikaa miezi 2 kisha tukapanga safari ya kurudi bongoland ili nikatoe barua na kutambulishwa ukweni,

Kabla sijaendelea huyu mwenzangu yeye alikuwa ni muislamu na mimi ni mkristo, baada ya kufika hapa home baada kama ya siku tatu mipango ikapangwa barua ikapelekwa ikapokelewa, siku ya tatu mshenga akaitwa akachukue majibu baada ya kufika pale tukakubaliwa vizuri tu,

utata ukaja kwenye dini maana mimi na huyu binti tulikubaliana yeye ndo atabadili dini anifuate mimi, lakini pale wajomba zake wakataka mimi ndo niwe muislamu walivutana sana maana mama yake alikuwa radhi bintiye abadili dini lakini baba na wajomba walikataa, mwisho wa picha mimi ikashindikana,

Binti alilia sana lakini wamakonde wale yaani wajomba zake hawakutaka kumwelewa, na wakasema kuanzia saa ile uhusiano mimi ni binti yao ufe maana hawakujua kama mwanaume mwenyewe ni kafiri kwani wanaume wa imani yake wako wengi na kama kuolewa ataolewa tuna muislamu mwenzake, mimi nilikubali kishingo upande na kuondoka bongo,

kutokana stress nilizokuwa nazo baada ya kufika hapa nikatafuta mwanamke wa kizulu ili niondowe stress,

Sasa mwezi huu yeye ananiambia mama yake amejadiliana na baba yake wamekubaliana kwamba abadili dini awe mkristo ili tuowane,

mimi sijamjibu maana najua yeye yupo humu jamii forum kama atauwona huu uzi namwambia amechelewa kwani nina mwanamke na ni mjamzito mwezi wa 3 nategemea kuitwa baba, nampenda lakini sina jinsi its to late.
 
Back
Top Bottom