Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Watu acheni kuongea mambo kwa hisia. Magufuli anafanya mambo mengi kwa mihemuko ya kihisia - na hata anaweza kukutumbua na kukurudisha katika cheo chako ndani ya dakika tano. Lakini kwa hili la kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo hapaswi kulaumiwa.
Na kabla hamjaanza kumlaumu mnapaswa kuelewa alichositisha ni nini hasa - ni ujenzi wa bandari au ni ujenzi wa bandari kwa makubaliano yaliyopo kati yetu na China? Nimesikitishwa sana na udhaifu na umbumbumbu wa Ndugai na Bunge katika hili. Na ningekuwa raisi wa nchi hii, huenda ningemuweka ndani Kikwete kwa kosa la uhaini kwa kukubali masharti kama yaliyopo kati yetu na Wachina kwa ajili ya hii bandari na SGR.
Kumbukeni SGR kwa mfano, makubaliano yalikuwa kati ya Tanzania na China. Magufuli aliingia akaupiga chini na kuanza kuingia makubaliano na Uturuki kwa awamu ya kwanza. Mmejiuliza kwa nini?
Nataka niwatahadharishe Watanzania wenzangu. Wachina huwa sio marafiki kama watu wengi wanavyofikiria. Ni wajanja mno. Afrika kwa sasa inapaswa kutambua kwamba hatari ya uhuru wa nchi zake wa kiuchumi na hata kisiasa kwa sasa hailetwi na mataifa ya magharibi, bali inaletwa na China. Hata siku moja usiingie kichwa kichwa ukiwa kiongozi wa nchi katika mkataba na China kwa sababu wanakuja kama marafiki zetu wasioingilia mambo yetu ya ndani. Utajikuta siku moja sehemu ya nchi yako imechukuliwa na waChina, au kufanywa mtumwa wa kiuchumi na kisiasa wa China kwa mamia ya miaka.
Hata wachina kutujengea Makao Makuu ya AU (African Union) pale Addis Ababa, nimewauliza watu, hivi mna uhakika gani kwamba kila neno mnalosema pale ndani ya hizo ofisi, au document mnayoandika, Mchina hawasikilizi na kujua mmeamua nini kata katika vikao vyenu vya siri? Yaani mnachoona ni msaada tu toka China na kupofushwa kiasi hicho?
Magufuli kuna mengi sana sikuungi mkono, lakini kwa hili la kusitisha huu mpango wa kujengewa bandari na SGR na waChina nakupongeza sana. Kuna nchi za Afrika ambazo ziliingia mikataba ya miradi mikubwa na muda mrefu na Wachina na sasa zinajuta na kulia. Acha turudi mezani na kuona ni jinsi gani tunaweza kujenga bandari Bagamoyo bila kuuza nchi na uhuru wetu kwa Wachina.
Kumbuka, Magufuli hajasitisha ujenzi wa bandari Bagamoyo kwa kuwa hataki kujenga bandari Bagamoyo. Amekataa kujenga bandari hiyo kwa masharti yaliyowekwa na Wachina. Aungwe mkono badala ya kulaumiwa, na alaumiwe kwa yanayostahili yeye kulaumiwa, lakini sio hili la bandari.